Ponda aigharimu Serikali milioni 10/-

Ponda aigharimu Serikali milioni 10/-

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
[h=2][/h]

*Usafiri wa helikopta waitafuna dola mara 71 ya gharama ya gari
ULINZI wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, akiwa gerezani na anapopelekwa mahakamani, umeanza kuvitesa vyombo vya Dola. Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, zinaeleza kuwa serikali juzi ilitumia kiasi cha shilingi 10,682,031 kama gharama za usafiri wa helikopta za kumpeleka na kumrudisha kiongozi huyo mahakamani mkoani Morogoro.

MTANZANIA Jumatano kupitia vyanzo vyake vilivyoko ndani na nje ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 hadi saa moja ni dola za Marekani 3,000 hadi 3,300 ambazo ni sawa na shilingi 5,341,032.85 .

Hivyo gharama za kwenda na kurudi kwa saa jumla yake ni dola za Marekani 6,600 ambazo ni sawa na shilingi 10,682,031.

Akithibitisha hilo, Kamanda wa Kikosi cha Anga wa Jeshi la Polisi, Antony Mwami alisema gharama za kurusha helikopta kwa dakika 45 ni dola 3,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni tano.

Katika uchunguzi wake gazeti hili limebaini kuwa gharama hizo zilizotumika kwa siku moja tu, zingetosha kumsafirisha Ponda kwenda Morogoro na kurudi mara 71, endapo ungetumika usafiri wa gari wa kawaida.

Gazeti hili limebaini kuwa kwa usafiri wa kawaida wa gari, gharama za kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hazizidi shilingi 150,000.

Juzi Jeshi la Polisi kwa kutumia helikopta yake inayodaiwa kuwa na uwezo wa kubeba watu wanane, lilimsafirisha Sheikh Ponda hadi mkoani Morogoro ambako alipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na kusomewa mashtaka ya uchochezi yanayomkabili.

Sheikh Ponda aliwasili kwa helikopta hiyo na kutua kwenye uwanja wa gofu, Morogoro akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi na alipakiwa tena kwenye gari maalumu ambalo liliongozana na mengine matatu ya polisi kuelekea eneo la mahakamani.

Baada ya kumalizika kusomwa kwa kesi hiyo, msafara ule ule ulimrejesha uwanja wa gofu saa sita mchana na kupandishwa tena kwenye helikopta kurejea jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, gharama hizo zinazozidi shilingi milioni 10 ni zile za helikopta tu, mbali na nyingine zikiwemo posho pamoja na magari yaliyotumika kumsafirisha wakati alipotua na kurudi katika uwanja wa gofu.

MTANZANIA Jumatano limedokezwa kuwa ndani ya Jeshi la Polisi, rubani anayerusha helikopta kwa muda wa saa moja, hulipwa kuanzia shilingi 100,000.

Kwamba helikopta iliyotumika kumbeba Ponda, hubeba watu wanane kwa maana ya marubani wawili na abiria wengine sita.

Hata hivyo gazeti hili limedokezwa kuwa, kwa askari ambao wanasindikiza mahabusu kama watalala wanakokwenda, hulipwa posho na kama hawalali hawalipwi.

Katika tukio la kumsindikiza Ponda hawakulala, hivyo hawakulipwa chochote.

Wakati hayo yakijitokeza, Gazeti hili kupitia vyanzo vyake vya habari vilivyoko ndani ya Jeshi la Polisi, limedokezwa kuwa hatua ya Ponda kusafirishwa kwa helikopta ilitokana na uamuzi wa baadhi ya viongozi wa juu wa Jeshi hilo walioko Dar es Salaam na wale wa Morogoro.

Inaelezwa kuwa viongozi hao walifikia uamuzi huo, baada ya kudai kuwapo kwa taarifa za kiintelijensia za kuwapo kwa tishio la usalama wa nchi endapo Ponda angesafirishwa kwa njia ya kawaida.

Juzi Ponda alianza kwa kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kufutiwa mashtaka ya uchochezi yaliyokuwa yakimkabili, baada ya kusomewa mara ya kwanza Agosti 14 mwaka huu akiwa kitandani katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kumshitaki.

Alidaiwa kutenda makosa hayo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano kati ya Juni 2 na Agosti 11 mwaka huu.

Ponda alifikishwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na baadaye alipandishwa kizimbani na kufutiwa kesi hiyo baada ya Wakili Kweka kuwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA).

Baada ya kufutiwa mashtaka hayo, alichukuliwa na kupelekwa Morogoro ambako pia alisomewa mashtaka ya uchochezi.
 
Duh kama helicopter garama yake ni kubwa hivyo dakika 45 tu ni milioni 5 basi CDM watakua wako fiti sana kifedha manake hiyo helicopter wakati wa campain waliirusha sana let say 12hrs *30days *10,682,031=3,845,531,160 yaani kwa mwezi mmoja CDM walikua wanatumia 3.8billions aisee sasa CHADEMA itabidi mbadilishe mtindo wa campain hiyo hela mnayotumia kwa kurusha helicopter katika campain muwapelekee maendeleo vijijini kwa kujenga visima kuwaletea maji wananchi watawapeni kura tu badala ya kuchoma hela angani muwe mkitumia magari
 
Kama kwenda kurudi milion kumi.. ile ya chadema sijui itakuwa shilingi ngapi... au ndio msaa wa mafuta watoka cdu?
 
Duh kama helicopter garama yake ni kubwa hivyo dakika 45 tu ni milioni 5 basi CDM watakua wako fiti sana kifedha manake hiyo helicopter wakati wa campain waliirusha sana let say 12hrs *30days *10,682,031=3,845,531,160 yaani kwa mwezi mmoja CDM walikua wanatumia 3.8billions aisee sasa CHADEMA itabidi mbadilishe mtindo wa campain hiyo hela mnayotumia kwa kurusha helicopter katika campain muwapelekee maendeleo vijijini kwa kujenga visima kuwaletea maji wananchi watawapeni kura tu badala ya kuchoma hela angani muwe mkitumia magari

kazi ya kujenga visima ni kazi ya serikali iliyoko madarakani ....kwa kuwa ndio inayokusanya kodi na hayo mambo ya kujenga visimi ni kazi ya serikali
 
ukweli unadhihiri, wakosa ni wao wanamlengea ponda, tanzania ni yt sote hakuna mwenye hati miliki tusinyanyaswe waislam
 
Kweli CDM kiboko, kwani kila kitu SI unit ni CDM. Hivi mnpokimbilia kuona kuwa CDM ilitumia gharama kubwa mmejiuliza kwanza haya?
1. Hivi ule msafara wa magari ulikouwa unatumiwa na JK, ukijumlisha gharamna ya mafuta na p/diem za watu wote aliokuwa anafuatana nao mnajua gharama yake?
2. Je mnajua kwamba upande wa manunuzi, watumishi walio wengi wa Serikali na idara zake wanapandisha gharama? usije shangaa, helicopter kama hiyo CDM wanaweza kuirusha Dar to Moro, kwa gharama huenda nusu ya hiyo.
3. Suala kama la Ponda kusafirishwa kwa helicopter au ilivyotokea kwa Kileo kusafirishwa kwenda Tabora kwa helicopter ni mwendelezo wa matumizi yasiyo ya lazima. Haya mambo kama ya Ponda yasingefikia hapa kama si udhaifu wa Serikali
 
Kenya mbali na gharama nyingine, walitumia $ 600,000 kukodisha ndege iliyomrudisha Sheikh Abdullah Faisal kwao Jamaica!...hivyo ndivyo mfumo kristo unavyofanya kazi.
 
Serikali yetu inaangaika sana,,,,kwanini hizo pesa wasiwaboreshee makazi hao police? Maana hata mrema alisema wanakaa kwenye vibanda vya bati ambavyo hata ukimuweka nguruwe hazai,,,serikali ijipange,,jeshi letu lina washauri wabaya
 
[QUOTE3. Suala kama la Ponda kusafirishwa kwa helicopter au ilivyotokea kwa Kileo kusafirishwa kwenda Tabora kwa helicopter ni mwendelezo wa matumizi yasiyo ya lazima. Haya mambo kama ya Ponda yasingefikia hapa kama si udhaifu wa Serikali[/QUOTE]

NAKUBALIANA NA WEWE KWA ASLIMIA 100
 
Kwa utete wa hali anayoizalisha kwa Taifa la watu mil.45 To hell with 10M, acha sheria ichukue nafasi.
Pesa makaratasi hasara roho.
 
Serikali yetu inaangaika sana,,,,kwanini hizo pesa wasiwaboreshee makazi hao police? Maana hata mrema alisema wanakaa kwenye vibanda vya bati ambavyo hata ukimuweka nguruwe hazai,,,serikali ijipange,,jeshi letu lina washauri wabaya

mrema pia aliwah kuwa waziri wa mambo ya ndani,alijenga nyumba NGAPI????AKAUJIUGUZE HUKO
 
Poor DPP,unamfutia mashtaka y ulimfungulia,na katka hil akitoka naondoa shiling kwenye Serkali ya JK II,huyu mtu ujana wake alikuwa wapi?mpaka aje aibukie uzeen ndo ajifanye mttezi,*u*k
 
Kweli CDM kiboko, kwani kila kitu SI unit ni CDM. Hivi mnpokimbilia kuona kuwa CDM ilitumia gharama kubwa mmejiuliza kwanza haya?
1. Hivi ule msafara wa magari ulikouwa unatumiwa na JK, ukijumlisha gharamna ya mafuta na p/diem za watu wote aliokuwa anafuatana nao mnajua gharama yake?
2. Je mnajua kwamba upande wa manunuzi, watumishi walio wengi wa Serikali na idara zake wanapandisha gharama? usije shangaa, helicopter kama hiyo CDM wanaweza kuirusha Dar to Moro, kwa gharama huenda nusu ya hiyo.
3. Suala kama la Ponda kusafirishwa kwa helicopter au ilivyotokea kwa Kileo kusafirishwa kwenda Tabora kwa helicopter ni mwendelezo wa matumizi yasiyo ya lazima. Haya mambo kama ya Ponda yasingefikia hapa kama si udhaifu wa Serikali

Kama CDM wanatumia 3.8billions kwa mwezi kwenye MC4 kwa mwaka watakua wanantumia 45.6billions kwa mwaka hiyo hiyo ni usafiri tu wakati wananchi masikini wanankufa njaa hebu waoneeni huruma wananchi bana muwasaidie mutumie magari hiyo balance mfanye maendeleo vijijini wananchi watawaamini zaidi na kuwapa kura
 
🙂 kuna askari wangapi wanadai pesa za likizo, uhamisho na posho bila kupewa kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa fungu lakini mbona la Ponda limepatikana?
 
mbona huo ni mwanzo tu kwani mpaka sasa zimebaki milioni 90 kati ya zile milioni 100, kwani vitengo wameanza kuneemeka mapeeema. kama huamini ona itavyokuwa inahairishwa mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom