Pombe.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pombe....

Discussion in 'JF Doctor' started by GP, Nov 24, 2009.

 1. GP

  GP JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  .....Inasaidia Kupunguza Magonjwa ya Moyo


  Matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni kuhusiana na unywaji pombe umeonyesha kuwa wanaume wanaokunywa pombe kila siku wana uwezekano mdogo wa kupata matatizo ya moyo kulinganisha na wanaume wasiokunywa pombe kabisa. Utafiti uliofanyika nchini Hispania na kuwashirikisha wanaume 15,000 na wanawake 26,000 umeonyesha kuwa pombe inasaidia kupunguza theluthi moja magonjwa ya moyo kwa wanaume wanaokunywa pombe kila siku.

  Hata hivyo pombe haikuonekana kuwa na faida yoyote kwa wanawake wanaokunywa kila siku.

  Utafiti huo ulifanyika nchini Hispania ambako wakazi wake wengi ni walevi huku kukiwa na wagonjwa wachache wa matatizo ya moyo.

  Utafiti huo ulihusisha wanawake na wanaume wenye umri kati ya miaka 29 na 69 ambao walitakiwa kuandika historia yao ya unywaji pombe na kisha kufuatiliwa afya zao kwa kipindi cha miaka 10.

  Aina ya pombe walizokuwa wakinywa washiriki wa utafiti huo hazikuonyesha tofauti yoyote kati yao.

  Jinsi pombe inavyosaidia kupunguza matatizo ya moyo bado haijakuwa wazi ingawa inajulikana kuwa pombe husaidia kuongeza kiwango cha lipoproteins mwilini ambacho huzuia kolestro zinazosababisha matatizo ya moyo kujijenga kwenye mishipa ya kusafirishia damu.

  Hata hivyo wataalamu wameendelea kuonya kuwa unywaji wa pombe uliopita kiwango ni hatari na husababisha matatizo mengi ya kiafya ambayo husababisha vifo vya watu milioni 1.8 kila mwaka.

  wapwa hii mnasemaje??

  source
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,991
  Trophy Points: 280
  Serengeti serengetiii
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Sasa Porjie ndo umeamua wawe wanaenda kulala hukohuko Zer pub au??
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahahaaaa, sio mchezo jamaa hapa wamepruvu kwamba biere ziko poa kwenye magonywa ya moyo, ntazinywa sana!!.
  wapwa wanajua mambo ya chuichui ndio maana tuko fit kiafya, TRY IT AT ANY BAR!
   
 5. bht

  bht JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  chui lazima wakulipe hii 'air time' haki ya nani vile....in cash or 'kind'
   
 6. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Ulevi wangu ni maji ya K'njaro
   
 7. GP

  GP JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hahahaaaaa, naskia tena unachangamka baraaaaa!, itabidi kwenye get tugeza tukuagizie boza zima pale sayansi kwa ajili yako!.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Bia
  bierre
  bira
  bier
  cerveja
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Amen
   
 10. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nakataga chupa 3 za moto napata na kitambi cha gafla.
   
 11. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Utafiti uliofanyika nchini Hispania na kuwashirikisha wanaume 15,000 na wanawake 26,000 umeonyesha kuwa pombe inasaidia kupunguza theluthi moja magonjwa ya moyo kwa wanaume wanaokunywa pombe kila siku

  Kuwa makini na hiyo theluthi moja na sidhani kama utafiti ulihusisha pombe kama zetu hizi , mwisho kumbuka bado haijajulikana jinsi pombe inavyoweza kupunguza magonjwa ya moyo so wakati unalitafakari hili pia ujue pombe ina madhara mengi sio magonjwa ya moyo tu, kunywa kwa afya!!!
   
 12. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Utafiti wenu na uishie kuzimu! Sitakunywa pombe na uwezekano wa kupata magojwa ya moyo kwasababu ya kutokunya pombe haupo!Naamini waliofanya huo utafiti ni maajenti au wajukuu wa shetani
   
 13. GP

  GP JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  karibu sana JF!,
  wewe ni HE/SHE?
   
 14. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Barikiwa ndg yangu,waache hao waendelee kusikiliza uongo wa baba wa uongo (shetani) na maajenti wake ambao wako kazini wakijua wanao muda mchache uliobaki wa kutimiza kazi yao hapa duniani.
   
Loading...