Pombe ,wanawake mpaka akamuua mkewe

beco

JF-Expert Member
May 7, 2013
1,339
782
Hbr
Kuna mzee mmoja mtaani alikuwa mlevi sanaaaa ,alibahatika kupata mwanamke mpole ,mcheshi mkarimu saaana watu wengi mtaani walimpenda ,yule mdada alikuwa around 28 hazidi 32yrs
Mwanaume alikuwa na hela mno ila alikuwa mtu wa matumizi espicially pombe na wanawake ,nakumbuka kuna siku tulikuwa nje usiku arnd saa 8 yule mzee alikuwa anatoka bar usiku yupo na mwanamke wanatembea nae walipokuwa wanaipita ile nyumba aliyokuwa anakaa mzee akawa anasema kumwambia yule barmaid kuwa ongea taratibu nakaa nyumba hii na manyani yangu yamelala.
Kila akirudi usiku lazima atafute sababu ya kumpiga yule mkewe kwa 7bu ambazo ni nonsense
Mchana yule mwanaume ni mtu usiku ni bondia wa kumdhalilisha mkewe kuna wakati alikuwa akimpiga mpaka kumvua nguo hadharani na asubuhi yule mwanamke alikuwa anakuwa bize kwa ajili ya mumewe kumuandalia huwezi jua kama usiku kulikuwa na purukushani
Kipigo ,kurudi saa 10 yalikuwa ndo maisha ya wawili hao ,nyumba yao na yetu zilikuwa zimepakana maeneo ya kinondoni bibi yangu aliwaita mara nyingi kumtaka mwanaume abadili tabia alikuwa akikiri makosa mpaka analia ikifika usiku km kawa kma dawa
Hali imeenda mpaka yule mbaba akapata ukimwi na kibaya zaidi akajigundua na akawa anatumia dozi kwa muda mrefu bila ya kumuambia mkewe ambae nae alikuwa ameupata baada ya kuwa magonjwa nyemelezi hayamuishi kuna shemeji yake akamchana live kuwa nenda kajiangalie maana mwenzio kaathirika
Kwenda hosp kweli akajikuta anao kwa shock ya ugonjwa akafariki in 3days akaacha watoto 2 , wote wakiume mkubwa was 11yrs na mdogo 9yrs
Mzee nae maisha ya kamvuruga baada ya kifo cha mkewe akawa km chizi kuna jirani akamchukua mtt 1 na bibi akamchukua mmoja maana ndugu za marehemu nao walipotea mwaka 2014 yule mzee alifariki kifo dhalilishi sana na huyu dogo mkubwa ndo amemaliza masterz ya finance na pia ni muajiriwa ktk moja ya audit firm kubwa hapa bongo na yule dogo mwengne mungu amemfungulia ana supply vifaa vya simu toka dubai amekuwa mfanya biashara mzur sana
 
Karibia story ifanane na Passed like a Shadow ya Bernard Mapalala... pole kwa familia
 
Pombe + wanawake ..

Ukiviendea kwa Pupa ...Umasikin na kifo umevisogeza karibu mile kadhaa za pumzi na maendeleo yako.
 
Wakiambiwa tulieni na wake zenu jibu kwani kakuzaa yeye pesa ninayo kwanini nijibane matokeo yake kuaacha watoto yatima upuuzi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom