Jamaa kapoteza mali zoote na akawa masikini wa kutupwa sababu ya ulevi, siku moja akapita karibu na jalala akaona chupa za bia. Akashika ya kwanza, akaipasua, kwa sababu yako nimeachana na mke wangu, akapasua ya pili: kwa sababu yako nimeshindwa kusomesha wanangu, akapasua ya tatu kwa hasira: kwa sababu yako nimefukuzwa kazi
akapasua ya nne: kwa sababu yako nimeuza mali zangu zote hadi nimefilisika. Akachukua ya tano akakuta haijafunguliwa imejaa bia akasema: we kaa pembeni, kwanza huu ugomvi haukuhusu tutaongea baadaye inaelekea huna tabia mbaya kama wenzako........
CHEZEA BIA WEWE?