Pombe ilitaka kuniharibia mahusiano yangu, sasa nimeamua kuacha

Pombe ilitaka kuniharibia mahusiano yangu, sasa nimeamua kuacha

Kijana leo

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
2,860
Reaction score
812
Habari za asubuhi wanandugu.

Nimeamua rasmi kuacha kutumia kileo/pombe, baada ya kuwa mtumwa kwa zaidi ya miaka 12, pombe ina athari nyingi sana wanandugu, si nzuri kiafya, kijamii, na kiuchumi pia, pombe imesababisha kutokuwa na mahusiano mazuri na mchumba wangu, japokuwa nina kipaji kizuri cha kujali na kumtumikia Mungu.

Lakini pombe imekuwa tatizo kubwa sana,sasa hatimaye nimeamua kuacha na kurudisha mahusiano yangu na Mungu, familia na mchumba wangu tuishi vizuri. Maana huu utumwa yatosha sasa, nimepoteza vitu vyangu vingi sana sababu ya pombe, sura ilishaanza poteza uhalisia wake wa ukijana, nimeshapata ajali lakini Mungu akaniokoa.

Nahaidi sasa kutumika kwa Mungu na nafasi zangu zote ambazo Mungu amenipa nitatumika kwa roho na kweli, baada ya kuahidi kuacha zaidi ya mara 20, nimeshapewa muda wa kubadilika ili tufunge ndoa lakini kila muda inashindikana, kwaherini marafiki walevi,live band zote hamtanitaja tena sasa yatosha.

Kwenye semina ya mwakasege nitaudhuria ili nikue kiroho na nina imani Mungu amenisamehe na nimekuwa kiumbe kipya, tazama ya kale yamepita yamekuwa mapya.

Muwe na mihangaiko mema wandugu.
 
kila jambo ukifanya kwa ulafi lina madhara ....
ukifunga ndoa ukakuta yaliyo hayamo.. usiasahahu kipenzi chetu POMBE ...... huyu yupo leo na hata milele....

ubarkiwe amani ya Bwana iwe nawe
 
Habari za asubuhi wanandugu,
nimeamua rasmi kuacha kutumia kileo/pombe, baada ya kuwa mtumwa kwa zaidi ya miaka 12, pombe ina athari nyingi sana wanandugu, si nzuri kiafya, kijamii, na kiuchumi pia, pombe imesababisha kutokuwa na mahusiano mazuri na mchumba wangu, japokuwa nina kipaji kizuri cha kujali na kumtumikia Mungu, lakini pombe imekuwa tatizo kubwa sana, lakini sasa hatimaye nimeamua kuacha na kurudisha mahusiano yangu na Mungu, familia na Mchumba wangu tuishi vizuri. Maana huu utumwa yatosha sasa, nimepoteza vitu vyangu vingi sana sababu ya pombe, sura ilishaanza poteza uhalisia wake wa ukijana, nimeshapata ajali lakini Mungu akaniokoa. Nahaidi sasa kutumika kwa Mungu na nafasi zangu zote ambazo Mungu amenipa nitatumika kwa roho na kweli, baada ya kuahidi kuacha zaidi ya mara 20, nimeshapewa muda wa kubadilika ili tufunge ndoa lakini kila muda inashindikana, kwaherini marafiki walevi,live band zote hamtanitaja tena, sasa yatosha. na kwenye semina ya mwakasege nitaudhuria ili nikue kiroho. na nina imani Mungu amenisamehe na nimekuwa kiumbe kipya, tazama ya kale yamepita yamekuwa mapya.
Muwe na Mihangaiko mema wandugu.

huyu atakuwa na yake.. Mbona mababu zetu walikula mond sana na wameoa na kuzeeka wakiwa na mafanikio kibao... Mbona jamii ya kichagaa inakunywa sana pombe na bado shule inapiga na bado ndio wanaoongoza kwa maendeleo? hii kasumba ya kusema pombe inarudisha maendeleo nyuma napingana nayo asilimia elfu moja.. Pia hii dhana ya kusema mahusiano yaliyo imara ni yale ya wasiotumia kileo chochote pia napingana nayo...

ATTITUDE YA MTU NDIO KIGEZO KIKUBWA ..KAMA MTU ALIKUWA MCHEPUKAJE AKIWA AMELEWA BASI ATAJUA KUWA UKILEWA UTACHEPUKA WATU WAMEKUWA WAKITUMIA MIFANO YA MAKUZI YAO KUREKEBISAH YA WENZAO KITU AMBACHO SIYO SAHIHI..
 
Safi, nina imani kama una hofu ya mungu Kila jambo lina mpango wa mungu.Kila mtu anakimbiza matukio ili historia ikamilike sasa unajuwa nje ndani Kuhusu pombe.God bless you.
 
wewe ndo ulikuwa tatizo,,, mpenzi pombe wala hajawahi kukufuata kwenu,,,, ulafi wako ndo uliokuponza.....anywy hongera.... ulikuwa unatukera sana ... we hujui tu...kila la kheri....
 
Inategemea ulikuwa unakunywa aina gani ya pombe,hata maandiko katika mithali 31 yanasisitiza unywaji pombe kwa kusema ''mpe masikini kilevi asahau shida zake''
 
Inategemea ulikuwa unakunywa aina gani ya pombe,hata maandiko katika mithali 31 yanasisitiza unywaji pombe kwa kusema ''mpe masikini kilevi asahau shida zake''

Mtu apendae anasa atakuwa maskini
Apendaye mvinyo na mafuta hatakuwa tajiri metahli 21:17
 
kila la kheir uendako uliitumia vibaya pombe ngoja wazoefu tuendelee.
 
kila jambo ukifanya kwa ulafi lina madhara ....
ukifunga ndoa ukakuta yaliyo hayamo.. usiasahahu kipenzi chetu POMBE ...... huyu yupo leo na hata milele....

ubarkiwe amani ya Bwana iwe nawe
amina mtumishi, najua utanimisi sana, ngoja kwanza niangalie upepo mwingine.
 
huyu atakuwa na yake.. Mbona mababu zetu walikula mond sana na wameoa na kuzeeka wakiwa na mafanikio kibao... Mbona jamii ya kichagaa inakunywa sana pombe na bado shule inapiga na bado ndio wanaoongoza kwa maendeleo? hii kasumba ya kusema pombe inarudisha maendeleo nyuma napingana nayo asilimia elfu moja.. Pia hii dhana ya kusema mahusiano yaliyo imara ni yale ya wasiotumia kileo chochote pia napingana nayo...

ATTITUDE YA MTU NDIO KIGEZO KIKUBWA ..KAMA MTU ALIKUWA MCHEPUKAJE AKIWA AMELEWA BASI ATAJUA KUWA UKILEWA UTACHEPUKA WATU WAMEKUWA WAKITUMIA MIFANO YA MAKUZI YAO KUREKEBISAH YA WENZAO KITU AMBACHO SIYO SAHIHI..

mwanandugu nisome vizuri utanielewa, sijasema pombe hurudisha maendeleo nyuma, ila kuna athari kiuchumi, wapo walevi na bado wanamaendeleo yao, na wala si kwamba mahusiano ya walevi ni ovyo, ila mimi nimeamua kubadilika na kuamua kuishi maisha mengine ili kuboresha mahusiano yangu na Mungu, familia na mchumba pia. hata nilipokuwa nakunywa nilikuwa nawajali sana, ila ni kuamua kusimama imara.
 
Joshua 1:9

Have I not commanded you? Be strong and courageous. Do not be afraid; do not be discouraged, for the LORD your God will be with you wherever you go."
asante mwanandugu, nitakuwa hodari na moyo wa ushujaa, sitaogopa, wacha sasa nimtumikie Mungu, maana Mungu ananihitaji niwe mtumishi wake, nina nafasi mbalimbali usharikani, na nyingine karibuni itakuja, Mungu anahitaji niwe wake.
 
Jambo jema mkuu bado sigara na zenyewe acha mara moja
 
Inategemea ulikuwa unakunywa aina gani ya pombe,hata maandiko katika mithali 31 yanasisitiza unywaji pombe kwa kusema ''mpe masikini kilevi asahau shida zake''

hata mimi nilipokuwa mlevi nilikuwa nautumia huo mstari na mingine zaidi ambayo ipo katika agano la kale, lakini baada ya agano jipya kuja mistari mingi ilikataa kilevi, na hata kwenye hiyo mithali kuna mstari unasema pombe uleta magomvi. kwahiyo mwanandugu kila jambo na wakati wake.
 
Back
Top Bottom