Pombe hizi! Mweee! Kwanini naendelea kuwa mlevi?

Pombe hizi! Mweee! Kwanini naendelea kuwa mlevi?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,677
NIWE mkweli, nilianza kunywa pombe zamani sana wakati ningali bado mdogo. Nimeambiwa awali nilikuwa nanyweshwa na wakubwa kwa kuwa nilikuwa napenda sana kulia, hivyo ili ninyamaze nilikuwa napewa kibakuli cha ulanzi nikinywa tu nalala watu wanaendelea na shughuli zao za kujenga Taifa letu changa bila kelele za kitoto kikilia. Miaka mingi ilipita hatimae nikawa nimehama kijijini kwetu na kuja mjini kuanza kujitegemea na kupata kipato changu mwenyewe ndipo nikakalizimika sasa kununua pombe kwa pesa zangu mwenyewe. .

Nilianza kwa kunywa pombe za kienyeji zenye bei ndogo, na kadri kipato kilivyoongezeka na mimi nikawa nabadili aina ya pombe na kuanza kunywa za kizungu. Kiukweli miaka michache ya kwanza nilikuwa nakunywa na kuwa mtu mchangamfu mwenye hadithi nyingi kwa walevi wenzangu na majirani waliokuwa na muda wa kunisikiliza.

Baada ya muda nikaanza kupata matatizo makubwa, nikawa kila nikinywa pombe naanza kuwa na imani kuwa mimi ni mwalimu wa karate, nikawa najaribu kuwatandika karate wote waliokuwa wanabisha hadithi ninazowahadithia, baadae yoyote aliyepita mbele yangu nilitishia kuwa ntampiga.

Kama unavyojua tena binadamu wa nchi hii, ukitaka kumpiga anajitetea, sasa wengine ni kati ya wale wananchi wenye hasira kali, hivyo mara nyingi niliamka asubuhi nikiwa na manundu na majeraha ya hapa na pale.

Nadhani pombe nilizokuwa nakunywa zilikuwa zinachanganywa na kitu cha ajabu sana, maana baada ya muda si mrefu nikaacha kujiona najua karate ila nikawa najiona mimi ni hendsam sana. Basi nikinywa kidogo tu nilikuwa najaribu kuwashika shika wadada hovyo nikiwa na uhakika wananipenda, hivyo nikawa nadundwa mara nyingi na wanaume wenye wivu, wale ambao hata ukimuangalia bibi yake kidogo, ataanza kurusha ngumi, si unajua kuna wanaume hawanaga subira.

Halafu hata wadada wengine wanapiga utadhani wanaua nyoka. Hakika hii iliniletea shida sana na kulazimika kuhudhuria vikao vingi kwenye ofisi za serikali ya mtaa wakati sijanywa na kunipa wakati mgumu uliojaa aibu. Nakumbuka nililazimika kuhama nyumba moja niliyopanga baada ya kurudi usiku na kugonga kwenye mlango wa chumba cha mama mwenye nyumba niliyokuwa naishi na kutaka afungue nilale kwake.

Mtiti mkubwa uliotokea usiku ule, sasa asubuhi nilipoamka pombe zikiwa zimetoka kichwani, mimi mwenyewe nilihama nyumba bila kufukuzwa.

Mara nyingine huwa nakaa nawaza hivi hii mikasa inasaidia nini? Kwanini naendelea kuwa mlevi? Basi huwa nanunua kachupa ninywe ili akili ikae sawa nifanye maamuzi yenye busara. Chupa moja huita nyingine, na hapo ndipo kwa kweli naanza kupata huruma ya ajabu sana.

Najifikiria hivi kwanini nakuwa mbinafsi? Hivi kwa nini tatizo langu binafsi linataka nifanye uamuzi ambao utaletea watu wengi hasara? Yaani mimi nikiacha pombe ni mimi peke yangu nitakae pata faida lakini Je, familia za watengeneza pombe zitapata wapi kipato kama walevi tutaacha pombe? Kipato chao kitashuka watashindwa kupeleka watoto wao shule, watashindwa kupata fedha za mavazi, wakiumwa watapata wapi fedha za hospitali?

Hapo ndio najiona jinsi uamuzi wangu ulivyo wa kikatili ambao hauzingatii faida za walio wengi. Mara nyingi ikifika hapo huwa huruma kubwa inaniingia na kuona ni heri busara mimi mmoja kuchangia katika uhai wa watengeneza pombe na familia zao.

Kimsingi siku hizi nakunywa kwa kuwa nina huruma.
 
Wewe ni Bujibuji tu sidhani kama hutabadilika utabaki kuwa Bujibuji tu
 
Ha ha haaa
 

Attachments

  • OMG.jpg
    OMG.jpg
    8.7 KB · Views: 1,899
Na huo ndio tunaita upendo wa kweli.

Mpende mwingine kama/kuliko unavojipenda mwenyewe.

Nunua pombe,kuza uchumi wa wazalishaji wa pombe.
 
Nimependa ulivyowakilisha muda mwengine tunalazimika kufanya vitu japo havitakiwi kwa huruma tu
Ukivuta bangi unamrahisishia maisha yule pusha ili watoto wake waongozane chooni na shuleni
 
du ndugu nimecheka sana, mimi nimeamua kwa sasa yatosha, wacha hizo familia ziendelee tu, maana wengine sio maskini ni matajiri, ila pombe hata kwenye biblia inaandika uleta magomvi, mimi nashukuru Mungu manumbu sikupata, il nilikuwa nikinywa lazima nizurule balaa, nihame bar mpaka basi na kuibiwa du imenitia hasara sana na kunifedhehesha. ila sasa yatosha. nimebaki na makovu tu ya ajali mkononi. ila pombe du.
 
Pole sn, kwanza kabisa wewe ni pure an alcoholic na kitaalum ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) HAUNA TIBA (RESEARCH BY World Health Organization (W.H.O) SINCE 1949) pia lazima ufahamu kuwa ULEVI SUGU (ALCOHOLISM) una hatua kuu tatu (YA AWALI, KATI NA YA MWISHO) kwa maelezo yako wewe umefikia hatua ya mwisho yaani LATE STAGE ambayo hakuna jinsi yoyote unaweza kunywa pombe na kubaki salama as a social drinker, njia pekee ya kukusaidia jaribu kutafuta kitu ALCOHOLICS ANOYMNOUS (A.A) MEETING katika eneo lako au waweza kuwasiliana nami kwa +255 789 78 05 29, Email: rnelsontz@yahoo.com kwa msaada zaidi.
 
MiImi pOmbe imEshawahiNifanYa kuA mtumwaa. Ila nilipo oa mke waNgu nikaAamua kumfaNya yy ndo KileVi changu. Yaani niKipata Kiu ya Pombe naMpigia simu kama yuko mbali naMwambia maNeno maTamu kwaMba nimEmmiss na niNataKa papuchi. so NikiToka job jiOni siendi Baa naWaHi nyumBani ilIatulize kiu Yangu.


ushAuRi wanGu: tafuTa kiTu au mtu unaChokipenDa ukIfaNye ndo poMbe yaKo palE kiu iNapokuja unamwamBia akusaidie either kWa usHauri au maHabaaa.
 
Kwa uandishi huu wa kilevi unadhani utaweza kumshawishi nani afuate maoni yako?
MiImi pOmbe imEshawahiNifanYa kuA mtumwaa. Ila nilipo oa mke waNgu nikaAamua kumfaNya yy ndo KileVi changu. Yaani niKipata Kiu ya Pombe naMpigia simu kama yuko mbali naMwambia maNeno maTamu kwaMba nimEmmiss na niNataKa papuchi. so NikiToka job jiOni siendi Baa naWaHi nyumBani ilIatulize kiu Yangu.


ushAuRi wanGu: tafuTa kiTu au mtu unaChokipenDa ukIfaNye ndo poMbe yaKo palE kiu iNapokuja unamwamBia akusaidie either kWa usHauri au maHabaaa.
 
Hapa nilipo Nina kili ya 2 du ni noma
 
Back
Top Bottom