Polygraph: Kitambua uongo

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Wasalaam Wakuu.

Imeandikwa Katika Vitabu Vitakatifu kuwa Usiseme Uongo. Usimdanganye jirani yako. Uongo usemwe pale tu patakapokua kwa ajili ya Kuokoa Maisha. Lakini jamii sasa imebadilika, Uongo umekubuhu kulikopitiliza. Wengine hutumia Uongo huo kwa ajili ya Manufaa Binafsi.

Ndipo hapo, Mwaka 1921 Johnson August Larson akagundua kifaa maalum chenye uwezo wa kutambua kama mhusika anasema Uongo. Mwaka 2003 kiliwekwa katika Encyclopedia , kama moja ya ugunduzi Mkubwa sana kupata kutokea.

Kifaa hiki pamoja na Mapungufu yake, endapo kitatumika ipasavyo na Wataalamu haswa, kina uwezo wa kutambua kama Mhusika nasema Ukweli ama Uongo kwa zaidi ya Asilimia 90.

Kitambua Uongo 'Lie Detector', ni maarufu sana katika maswala ya Usalama hasa katika Nchi za Marekani, Canada, Australia, India pamoja na nchi nyinginezo. Kifaa hiki hutumika zaidi katika kuonyesha kama watuhumiwa wa makosa ya Jinai wanasema kweli ama Uongo. Majibu ya kifaa hiki yanaweza kutumika kama kidhibiti Mahakamani kwa baadhi ya nchi.

Nchini Marekani hutumika sana katika kuwapata vijana watakaojumuishwa katika taasisi za kijasusi hasa FBI pamoja na CIA. Mwenye nia, pamoja na kupitia hatua mbalimbali, sharti lazima apitie katika Kitambua Uongo ili kuonyesha ni kwa jinsi gani majibu aliyoyatoa yana Ukweli. Hivyo, kabla ya hatua zaidi za kupata mafunzo ya Ujasusi na Ushushu ni lazima Mhusika afanye Polygraph test na majibu yawe ya kuridhisha kwa kiasi kikubwa kuwa hadanganyi. Baada ya hapo hatua zaidi hufuata.

Hatua.
Kuna hatua tatu za kufata ili kuweza kupata majibu juu ya Ukweli au Uongo asemao Mhusika.
1. Pre Test
2. In test
3. Post Test

Hatua ya Kwanza ' Pre Test Phase'
Hapa Mhusika hupewa Elimu kuhusu kifaa husika. Jinsi kinavyofanya kazi. Haki zake za Msingi, na kwa namna gani Majibu ya Kifaa hicho yatakavyotumika. Mhusika pia huulizwa maswali ya awali kabisa na kupaswa kuyatolea Ufafanuzi na baada ya hapo hupewa ayapitie kama kilichoandikwa kipo sahihi. Yeye pia ana haki ya kuuliza swali na kujibiwa vilivyo. Huambiwa pia maswali yote atakayoulizwa kipindi atakapokuwa kwenye Mashine.

Ni katua hatua hii ambayo Mhusika (examinee) hufungwa vifaa kadhaa mwilini ili kufanikisha zoezi zima. Kuna vifaa takribani sita ambavyo hufungwa mwilini kwa Mhusika. Baadhi ya Vifaa ni kama vifuatavyo;
a) Mikanda miwili maalum ambayo moja hufungwa kifuani na chini kidogo ya tumbo. Mikanda hii ni maalum katika kupima pumzi.

b) Sensors mbili ambazo hupachikwa katika vidole viwili vya Mkononi vya Mhusika. Hii husaidia katika kupima jasho litokalo katika mwili.
c) Kifaa maalum ambacho hufungwa Mkononi mwa Mhusika ili kupima msukumo wa Damu, pressure, mapigo ya moyo na kadhalika.
 

Attachments

  • rcrm_a_1060080_f0003_oc.jpg
    rcrm_a_1060080_f0003_oc.jpg
    25.6 KB · Views: 45
Hatua ya Pili 'In test phase'
Hii ni hatua Muhimu zaidi kupita zingine. Hatua hii ndiyo hutoa majibu. Baada ya yote ya hatua ya Kwanza, Mhusika huunganishwa katika mashine hiyo Maalum kwa vifaa vilivyofungwa. Mashine hii huchora graph mbalimbali ya kutokwa kwa Jasho, msukumo wa Damu, mapigo ya moyo pamoja na mengineyo pale ambapo Mhusika atakapokuwa anaulizwa Maswali.

Huweza kufanyiwa majaribio (tests) tatu mpaka sita. Na kila jaribio huchua dakika tatu mpaka tano. Baada ya hapo Mhusika hupewa dakika Walau mbili za kupumzika kila mwisho wa jaribio. Huku Examiner akiyatafakari majibu na graph zilizochorwa na mashine husika.

Kumbuka maswali yanayoulizwa ni kujibu 'Ndiyo' au 'Hapana'. Hakuna kujielezea, yaani no narrative questions/ answers.

Kupanda zaidi kwa mapigo ya moyo, muongezeko wa msukumo wa damu, kutokwa kwa jasho pamoja na kuongeza upumuaji husababisha graph kupanda na huenda ikatafsiriwa baadae kuwa unasema Uongo.

Baada ya hapo ni katika hatua hii, msimamizi (examiner) hutoa hitimisho baada ya majaribio yote. Majibu mengi huwa ya aina tatu;
i) Uongo umehisiwa
ii) Uongo haujahisiwa
iii) Kutojitosheleza (kwamba Kuna Uongo ama La)
 

Attachments

  • rcrm_a_1060080_f0001_oc.jpg
    rcrm_a_1060080_f0001_oc.jpg
    26.2 KB · Views: 28
Hatua ya Tatu 'Post test Phase'
Hapa ni hitimisho katika zoezi zima. Hapa msimamizi ataeleza majibu kwa mhitaji (polisi, vyombo vya Usalama) juu ya Ripoti iliyopatikana katika zoezi zima. Kisha ripoti hiyo kama itakuwa na uhitaji iitakabidhiwa kwa uhitaji kwa matumizi mengine ya Baadae. Na zoezi zima linaishia hapo.

Binadamu ni Viumbe wa ajabu sana, pamoja na yote mashine haidanganyi lakini binadamu hudanganya. Binadamu anaweza kufanya hila yoyote na mashine kuonyesha kuwa hadanganyi.

Njia mojawapo ni kutumia kilevi kabla ya kufanya zoezi hilo au kutumia baadhi ya vidonge ambavyo vitasaidia kuipumbaza mashine.

Na katika hilo, huruhusiwi kutumia kilevi au baadhi ya madawa siku moja kabla ya kufanyiwa jaribio katika mashine husika.

Kwa utaalamu wa wengine, huweza kuongoza miili yao isionyeshe mabadiliko yeyote wanapokuwa katika jaribio hilo zima kama wanasema Uongo ama la.

Katika kitabu cha "Tutarudi na Roho zetu" kilichoandikwa na Ben Mtobwa, Mhusika Mkuu Joram Kiango alimfundisha mpenzi wake (jina nimemsahau) jinsi ya kuipumbaza hiyo mashine punde watakapopimwa nchini Afrika Kusini.

Pamoja na yote, mashine hiyo pia huweza kutoa majibu ndivyo sivyo. Mhusika anaweza kuwa anasema Ukweli lakini kutokana na hofu, majibu yakatoka ndivyo sivyo.

...........
NB: Kwa Msaada wa Mtandao.
 
Waache kwanza kuingia mikataba ya mangungo kwenye madini yetu, then ndio waje na hizo tantariraaa zao.
 
Kwenye kipindi cha Forensic Files ambacho hurejelea matukio halisi ya mauaji, ni wazi wapo watu ambao wanaweza kukizidi kete kifaa hiki. Ma-social paths, ma-sadists na jamaa wengine ambao hawana emotions za kawaida wanaweza kukidanganya kifaa hiki bila shida yo yote. Na kwa vile hakiwezi kutoa matokeo ambayo ni ya kweli kabisa kabisa kwa asilimia 100 kwa mara zote, ndiyo maana matokeo yake hayakubaliki kama ushahidi mahakamani.
 
Ingawa mtoa mada amejikita sana katika masuala ya uhalifu au usalama, kifaa hiki pia kinatumika na menejimenti za makampuni mbalimbali ili kuabgalia maadili ya mameneja katika shughuli mbalimbali za kampuni. Sio ajabu kwa mfano kukuta katika kampuni za afrika ya kusini kwa mameneja kupitishwa kila mwaka katika ukaguzi kama huu.
 
Siyo kipimo tosha cha kuhitimisha matokeo kuwa ni kweli, kuna cases nyingi ambapo majibu yanayopatikana uwa siyo ya kweli mfano mtu inaweza onyesha kadanganya wakati hajadanganya au ikaonyesha anaongea ukweli kumbe kadanganya.
I am addicted to IDx na mara kadhaa nimeona hili kitu.
 
Hiyo nayo sidhani kama majibu yake yanaweza kuaminika moja kwa moja.....mtu wa kawaida kuona unavalushwavalishwa yale ma mikanda..mara sijui vidoleni, nyaya hizo za umeme etc....lazima upanick tu....hiyo njia yenyewe inapanikisha tayar.....
 
Back
Top Bottom