Gman-lz
Member
- Feb 23, 2015
- 66
- 5
Baba: Kijana wangu utaoa binti ambaye nitakuchagulia.
Dogo: HAPANA.
Baba: Nakuletea Binti wa Rais Kagame
Dogo: Basi huyo poa
Baba anapata nafasi ya kukutana na Kagame. Anamwambia "Kijana wangu anataka amuoe mwanao"
Kagame: Unanitania eeh?! Ntakuweka ndani!
Baba: Nimetumwa na Mshua Jei-Pii-Emu, mimi ni Baba mdogo wa kijana wake, na kijana wake ni Mkurugenzi wa Uchumi IMF, kanda ya Africa
Kagame: Hahaha . . . Sasa kijana mbona hujitambulishi mapema. Basi sawa.
Baba anamfuata Mkurugenzi Mkuu wa IMF, anamwambia ampe Ukurugenzi wa Uchumi Afrika. Anagoma.
Anamwambia kijana wangu ni mtoto niliyezaa na dada ake tajiri namba moja Afrika, Aliko Dangote
Mkurugenzi anakubali. Baba anamfuata Dangote na kumwambia akubali kusema mke wake (Baba) ni dada ake.
Dangote anagoma.
Baba anamwambia Dangote kwamba yeye ni Mwakilishi wa Rais wa Tanzania (Hapo ndo Dangote amekuja kuomba awekeze Tanzania)
Dangote anakubali
HIVI NDIVYO SIASA ILIVYO. MKO POA JAMAN?!