POLITICAL BATTLE MAP: POLEPOLE vs Samia, wanamtandao na wahuni.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,412
POLITICAL BATTLE MAP: POLEPOLE vs RAIS

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Katika hili vita ambavyo Polepole ameianzisha. Acha tuone Tamani ya pambano la kisiasa baina ya Polepole Vs Rais. Tuone njia na mbinu, rasilimali zitakazotumika, na hatma ya pambano hilo. Nani ataibuka kidedea;

Tunaanza na uwanja wa vita;

1. Uwanja wa Vita (Theater of Operations)

a) Uwanja (front) ya Kisiasa.
Katika uwanja wa kisiasa hasa tuna dura zifuatazo(mistari/front hizi)
i) CCM internal politics, makundi ya ndani ya chama yanayowania ushawishi.
Hapa tuna Sukuma Gang Vs wahuni/wanamtandao .
Polepole ni yupo Sukuma Gang sina uhakika na upande wa pili wahuni ni kina nani lakini baadhi yao wameanza kujitokeza. Hivyo tutawajua kadiri siku ziendavyo.

ii) National politics, perception ya wananchi kuhusu serikali ya Samia.
Mtaani watu wanazungumza nini kuhusu utawala uliopo. Huko pia battle lipo. Wapo wasiotaka na wapo wanaotaka.

iii) Front ya Kimaudhui (Narrative space):
Hapa ni maudhui aliyonayo Polepole mwenyewe. Hili nilieleza kwenye post iliyopita. Kuwa Maudhui ya Polepole lazima ayatoe kimkakati na asicheleweshe mashambulizi mazito.

iv)Mitandao ya kijamii (social media front);
Hivi Facebook, YouTube zikitumika. Kama uwanja wa mapambano. Lakini uwanja huu Serikali imetawala na inaudhibiti mkubwa. Hivyo Polepole lazima atafute mbinu za ziada ambazo nitazipendekeza.

v) Media ya jadi (TV, radio, magazeti)
Hivi haviwezekaniki. Ila ni kete kwa serikali kutumia uwanja huu kumshabulia Polepole

vi) Front ya Kihisani (Grassroots & elite alliances):
Wanachama wa chama, viongozi wa mikoa, youth wings (UVCCM) hapa Polepole ahangaike kuteka ushawishi, kutekan Influencers wa kisiasa, wasanii, bloggers n.k.

Vita hivyo vitapiganwa katika viwanja hivyo.

2. VIKOSI NA RASILIMALI (Force Structure)
a) Polepole:
I) Kikosi cha mtandaoni (online guerrilla media team)
ii) Viongozi wa zamani/wastaafu wanaomuelewa

iii) Mitandao ya vijana waliokatishwa tamaa na uongozi wa sasa..

b) Rais, wahuni na wanamtandao
I) State machinery (vyombo vya usalama na dola, media control, sheria za habari)

ii) Inner circle yenye fedha nyingi na access kwenye vyombo vya habari.
Hapa tunazungumzia wafanyabishara na matajiri wanaofadhili na washirika wa serikali.

iii) Digital censorship capability (blocking platforms, surveillance)
Uwezo wa serikali kupambana na mashambulizi ya Polepole kwa njia za kidijitali.

Hii ni kumaanisha katika kipengele hiki Polepole inampasa aongeze Rasilimali watu ili mzani wa ushindi uwe upande wake. Lakini kwa hali ilivyo sasa bado yupo chini ya asilimia 20 katika rasilimali.

3. Mikakati Kuu (Strategic Axes)
Tukija kwenye Mikakati hapa ndipo kiini cha muelekeo wa hili pambano. Polepole lazima azingatie haya;
a) Narrative Control:
Polepole aweke “main story” kwamba anapigania maslahi ya taifa, siyo vita binafsi. Alenge kuamsha hisia za makundi yote katika maudhui yake. Asionyeshe mambo yake binafsi.

b) Njia mbadala wa kusambaza taarifa zake (Information Resilience):
Kuunda njia mbadala za kusambaza taarifa (parallel networks) ili censorship isimmalize. Hapa atafute wahusika wengine wa aina mbili, ambao watajifanya wapo Neutral wanaotoa habari zake lakini wako upande wake ili kum-netraulize adui yake. Pili, ambao ni mahasimu wa serikali. Wote wawe na followers na Wana ushawishi.

b) kuunganisha makundi(Coalition Building):
Kuunganisha makundi yote yaliyotengwa au yaliyovunjika moyo ndani ya chama na jamii.

c) Counter-Intelligence:
Kuepuka mtego wa kuzua kesi za uchochezi kwa kutoa kauli zenye impact bila kuvunja sheria moja kwa moja. Yeye na washirika wake wanaposhambulia waepuke kutoa maneno bila ushahidi. Vita hivi kitahitaji mambo ya kweli na propaganda. So ni muhimu kuwa makini katika kurusha vyuma

e) Timing & Sequencing:
Kuweka mashambulizi makuu (political disclosures) karibu na uchaguzi au pale mgawanyiko unapoongezeka ndani ya CCM. Lakini pia kutumia muda mwingi kushambulia maeneo nyeti kuliko kupambana na maadui wanaojitokeza katikati ya mapambano.

4. Hatua za Utekelezaji (Operational Phases)
Mikakati na mipango kufuatwa na utekelezaji. Utekelezaji upo kwa hatua zifuatazo;
Phase 1: Reconnaissance & Network Building
Kukusanya data, kuunganisha watu, kuanzisha channels salama.
Tayari tunajua Polepole anadata sasa ishu kubwa ni kuunganisha watu na kuanzisha channel salama kwaajili ya kufikia malengo yake. Hii inahitaji umakini mkubwa.

Phase 2: Narrative Deployment
Kutumia influencers na covert accounts kusambaza ujumbe. Hii tumeshazungumza huko juu. Kuwatumia kina Mange Kimambi, Sarungi na watu wengine wenye ushawishi kama Wachungaji na masheikh

Phase 3: Strategic Disclosures
Kutupa mabomu ya kisiasa kwa ushahidi mzito katika nyakati nyeti.
Hili nililisema kwenye posti iliyopita. Vita vya maneno kwenye siasa za kutaka kumuondoa Rais sio vita vya maneno ya wanawake wakichambana, vinahitaji timing na kulega target kwa kuzingatia wakati, mazingira na matukio.

Phase 4: Mass Mobilization
Kushawishi grassroots na kushirikisha makundi ya vijana na wastaafu. Hii akikosea huko juu huku atashindwa kufika. Nafikiri tuliona kwa Mange Kimambi, pia tulio maandamano mengi ya chadema yakifeli

Phase 5: Containment & Protection
Kujilinda dhidi ya counter-attacks kupitia legal shields na public sympathy. Tayari ameshateka ushawishi kwa umma, watu wengi wanakuamini. Hivi kwake pekee itakuwa kinga kumkinga na mashambulizi hatari ya kidola

5. Hatari Kuu (Risk Factors).
Hatari anazoweza kuzipata au zinazotarajiwa;
a) High Risk:
I) State repression (kukamatwa, kufungiwa akaunti, vitisho) hii tumeiona kwa Tundu Lisu na wengineo ambao waliingia katika pambano

ili) Media blackout inayokata visibility.
Kuzuia mtandao au kuzima au kupunguza kasi ya kuperuzi katika mitandao wakati Polepole akizungumza

iii) Infiltration na betrayal kutoka ndani ya timu yake.
Hii ndio hatari zaidi. Hapa kuna usaliti. Kununuliwa kwa baadhi ya watu wake au kuwekewa pandikizi. Huu tumeiona kwa Chadema jinsi ilivyopigwa na vitu vizito kwa mbinu hizi.

b) Moderate Risk:
I) Kutangazwa kama msaliti wa chama na kufukuzwa chama

ili) watu kuchoka na kumzoea Polepole ikiwa ujumbe unajirudia bila matokeo. Hili nimelisema tangu siku ya kwanza.

c) Low Risk:

I) Kujipotezea credibility ikiwa atachokwa na kuonekana kama mtu mwenye chuki binafsi na Rais au wanamtandao anaowatuhumu

UWEZEKANO WA KUSHINDA AU KUSHINDWA;

I) Uwezekano wa kushinda (Win Probability): ~30-40%
Ana nafasi ikiwa atafanikiwa kuunganisha makundi ya ndani ya CCM, kupata media mbadala, na kudhibiti muda wa mashambulizi yake na hapa nazungumzia target na timing na kufuatana na matukio nyeti katika mashambulizi yake.

ii) Uwezekano wa kushindwa (Loss Probability): ~60-70%
Kwa sababu Rais ana control over state apparatus, access ya rasilimali, na uwezo wa information suppression.

Hata kama hatashinda vita ya moja kwa moja, anaweza kushinda narrative war kwa muda mrefu, na kuji-position kwa uchaguzi ujao au machafuko ya ndani ya chama.

Kwa lugha ya political science, hii ni vita kati ya incumbent advantage na reformist insurgency. Kwa lugha ya intelligence tradecraft, hii ni high-risk influence operation ambapo survival inategemea network resilience na timing kuliko nguvu ya moja kwa moja.

Hii ni kumaanisha Polepole pekeake hatoboi!

Acha nipumzike sasa

Nawatakia maandalizi mema ya sabato

Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Andiko zuri, uchambuzi mzuri lakini naamini katika ukuu wa Mungu. Wakati Daudi anawekwa kuwa mfalme hakuna aliyekuwa akilijua wala kulitegemea hilo, na hata kutajwa katika watoto (wa kiume) hakutajwa hadi pale ilipolazimika na kumbe ndiye aliyekuwa kapangwa na mwenyezi Mungu.

Daudi alikwenda kupigana na jeshi kubwa la Goliath na kushinda vita si kwasababu alikuwa na vifaa kuliko vya adui, lah! Alishinda kwasababu alikuwa na Mungu, usaidizi wake ulitoka kwa Mungu.

Mie binafsi namuona Humphrey hayuko yeye mwenyewe, yuko na Mungu ...ana usaidizi wa Mungu na Mungu hajawahi kushindwa.
 
Aliye na Mungu ni yule atakayeshinda Mkuu
 
What if mwenye state yupo na Mwenda pole, lakini anaplay around kuwazuga wahuni/wanamtandao kwasababu anaona yeye peke yake hawawezi, mwisho anajitoa na kumpa kijiti mwingine kuonekana ameshindwa lakini in real sense ameshinda, huku wahuni/wanamtandao wakiwa wamelamba mchanga?
 
Ukipata sababu za kwa nini alibadilisha wakurugenzi wa Tiss miaka 4 DG wa 4 hivi ni vituko
 

Ukiangalia kete zinavyosogezwa Moja Kwa Moja kingi itakayoingia ni Moja ambaye ni Samia.
Hakuna uwezekano wa kete zingine kuingia kingi. Huo uwezekano haupo kulingana na mchezo wa draft uliopo.
 
IA ndio imeandika hapa

USSR
 
Ukuu wa Mungu hauwezi kushindwa na bunduki.
HP ni agizo la Mungu
 
The battle is brutal but still fair
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…