Polisi Zanzibar yataja orodha ya waliokufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Zanzibar yataja orodha ya waliokufa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Oct 10, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Na Mwandishi Wetu

  POLISI Zanzibar imetangaza orodha ya watu saba waliyokutwa wamekufa katika mazingira ya kutatanisha, akiwamo mwanamke aliyeuawa kwa kukatwa shingoni katika Mkoa wa Kusini Unguja.

  Majina ya watu hao yalitangazwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Yahaya Rashid Bughi, alipozungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

  Kamanda Bughi alisema vifo vya watu hao vimetokea katika kipindi cha wiki moja kuanzia Oktoba 2, mwaka huu.

  Aliwataja watu waliokutwa wamekufa kuwa ni Nassor Abdallah Khalfan (53), mkazi wa Kisiwandui, aliyegundulika akiwa amekufa chumbani kwake baada ya kupingwa visu vya tumboni.

  “Mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha makubwa tumboni,” alisema.

  Alisema daktari yaliyefanyia uchuguzi mwili wa Nassor bado hajatoa ripoti, lakini polisi wameshaanza upelelezi wa tukio hilo. Uchunguzi wa awali imebaini Nassor alikuwa ameuawa.

  Mwingine ni Hafidhi Said Kassim (18), mkazi wa Kwaalimsha, aliyekufa baada ya kupingwa kisu cha mgogoni alipokuwa akicheza disko katika ukumbi wa NTRO, Wilaya ya Mjini Unguja.

  Oktoba 4, mwaka huu, uliokotwa mwili wa Akida Hussein Khamis (32), mkazi wa Kisiwandui, ukiwa umetupwa kando ya barabara ya Gongoni.

  Mwili wa marehemu unaonyesha kuwapo kwa dalili za kunyongwa shingo na baadaye mwili wake kutupwa ukiwa uchi katika eneo hilo.

  Orodha ya vifo ya polisi inaeleza Oktoba 2 katika Mtaa wa Magomeni, Wilaya ya Magharibi, Khalfan Hamza Omar (30) alikutwa akiwa amekufa ndani ya chumba chake baada ya kuungua na moto. Hata hivyo, Bughi alisema chanzo cha moto huo ni mshumaa aliokuwa akitumia Omar kabla ya kusababisha kifo chake.

  Katika hatua nyingine, Oktoba 2, Hassan Nyaruguru Mchele (40) amekutwa amekufa katika dimbwi la maji katika eneo la Amani.

  Kamanda Bughi alisema Oktoba 7 mfanyakazi wa Mradi wa Uhifadhi wa Mazingira katika ukanda wa Pwani (MCEMP), Mohammed Abdallah Mwalim (37), mkazi wa Mwanakwerekwe, alikufa baada ya kupigwa jiwe kichwani wakati akiendesha pikipiki.

  Wakati huo huo, mwanamke mmoja huko katika Mkoa wa Kusini Unguja amekufa baada ya kukatwa shingo na kupigwa visu vya tumbo.

  Tangu kujitokeza matukio ya vifo vya kutatanisha, baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Unguja wamekumbwa na hofu na hivyo kushindwa kutembea nyakati za usiku.

  ________________________
  Kwa habari zaidi bofya hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/10/10/habari5.php
   
Loading...