Waziri kivuli
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 2,987
- 3,450
Takribani mwezi mmoja uliopita nilienda kigoma wilaya ya kasulu katika kijiji cha kabanga!
Kulitokea tafrani ambapo mwananchi mmoja aliuwawa na wananchi wenye hasira kal(sitalizungumzia hili)!
Baada ya tukio hilo, waliletwa kikosi FFU na askari wa kawaida kurejesha amani!
Wananchi wengi hasa wanaume walikimbilia mashambani kujificha! Na hapo ndipo polisi hao walopoonesha rangi zao halisi!
Walivamia biashara za watu zilizotelekezwa na kuchukua mali na fedha, walivunja hadi fridge na kubeba vinywaji!
Walivamia nyumba za watu na kupora pesa na simu, kuna rafiki yangu alijificha juu ya paa la nyumba, alishuhudia polisi wakivunja mlango na kupora simu 2 na pesa taslimu sh 300,000!
Walikuwa wanakamata yeyote wanayemuona!Na walipowafikisha kituoni, waliwapiga kabla ya kuwaingiza mahabusu, kuna mzee mmoja alivunjwa mguu kwa kipigo akiwa kituo cha polisi!
Kwanini polisi wanatenda haya? Kama wao ni wezi, nani wa kulinda mali zetu?