Polisi wavunja maandamano ya Wanafunzi UDSM; Watawanywa kwa mabomu ya machozi

Hao ni wahuni wachache wanawalazimisha watu kugoma kwa lazima. Daruso na coet wote hawaungi mkono mgo lkn hao daruso hawawaunganishi wale wanaopinga mgomo na wao kuandamana ili wapambane, mie natamani muuwane wenyewe kwa wenyewe watanganyika. Laana za mungu hizo kupitia kwa nyerere.


wewe ni kati ya VIBARAKA WA MAFISADI huna unaloliweza, huna maamuzi, huthamini utu wa mtanzania NDO MAANA UMEKUA RADHI KUNUNULIWA................
 
mkwere anafanya vitu kama mbuni kukitokea tatizo anakimbia au anaficha kichwa ardhini! Hapa nilipo kila siku kuna mgao wa umeme kuanzia juzi wameuongeza tena yaani nina hasira kwa nini cdm au vyama vingine tusiandamane kupinga kutokupatikana kwa umeme? Hakuna umeme, maji ya bomba tushasahau yanavyotoka, bidhaa zote bei juu, elimu inazidi kuporomoka, wazee wa east africa hawalipwi wakati dowans wanataka kulipwa faster, mishahara haiongezwi etc matatizo yako mengi sana nchi hii, kuna watu wanatoa solution kama jinsi ya kupunguza foleni za magari kwa ku built fly over eneo za trafick light na njia za chini lakini hakuna viongozi anaye react. Mpaka watu wagome ndo watawa please hao, then wakitokea wengine wanagoma wakiwa wachache hawasikilizwi. Hivi mkwere & your co mnatutakia nini? Kama hela mnazo maisha ya anasa mnaishi lakini hata kutupa solution za matatizo yetu huwezi? Hivi ukienda ukakopa 2 billion US $ ukaja nazo ukatutengenezea steigler project inayoweza kuzalisha mw 2000 ili tupate umeme wa uhakika, itakuathiri nini ktk anasa zako? Hivi ukimwita Slaa na Mbowe na vichwa vingine mkaunda "think tank" jinsi ya kututoa hapa tulipo ili tusonge mbele itakufanya upungukiwe na nini? Kweli unasema unaanzisha miji ya viwanda wakati umeme hakuna? Watu wa migodi wanatumia ma generator yao wakati tuna eneo lina mw 2000? Hata kama litachukua ten years kuwa ready we will know you have solved the problem. Tuna madini mengi sana ushaenda Zambia ukauliza walifanyaje wakavunja mikataba yenye kodi ya kuwapendelea wawekezaji badala ya wananchi, nenda Botswana kaangalie walivyofanikiwa ktk kuinua pato la nchi kwa kutegemea madini. Kama unawaogopa isije ikawa mambo ya icc kwa nini Zambia waweze sisi tushindwe? Uliunda tume ikakupa majibu lakini wananchi hatuoni kitu. mkwere uwezo wa kututoa hapa tulipo kutupeleka mbele upo na bado ukaendelea na anasa zako, kama huwezi mpe Magufuli awe waziri mkuu kuliko huyo pinda ambaye ni "yes boss" unajua nikitafakari nashangaa ilikuwaje ccm wakakupa u president? Inakuwaje unajibu "hujui kwa nini watanzania ni maskini" hujui! Mi nakushauri weka urafiki pembeni linapokuja swala la taifa, unda "think tank" vikiwemo vichwa vyote Slaa, Mbowe, Magufuli, cuf etc, lets build our tz together.

Daaa! mkuu huyu mkwere angekuwa anapitia post kama hii yako, angevuza kofia na kuachia ngazi.........!:clap2:
 
Mzukaaa!! big up wenzangu na mimi vyuoni, ni kweli boom haitoshi, yan km ingewezekana iyo hali ingehamia vyuo vyote vikuu Tz, kuna vyuo vya porin tangu vianze havisikiki, yan migomo kwao haijulikani sa sijui kama wao icho kiasi kinawatosha. Makumira tupo wote hata kwa kulalamika bt ipo siku nasi tutakuwa barabarani. Washeni moto huo mpaka ikulu nasi twaja nyuma yenu. Ni jana tu hao wakuu wa bodi walikuwa wanatema pumba zao TBC. Washa washa, msiwaogope hao mbwa koko wa kikwete!
 
Serekali ambayo ni vivu kufikiri na isiyo realistic,sh 5,000 kwa maisha ya leo na mifumuko ya bei ya kila kitu unaitumia vipi kwa matumizi ya siku nzima??? Wafanye mgomo usio na kikomo
 
Uncle sawa kabs, lakini kuna kamtego hapo! unajua UE V/S mogomo relationship? frustration na mambo kama hayo, mm naunga mkono kudai haki kwa nguvu pale ninaona sina njia mbadala,!! kama unenisoma pamoja na kuadress ishu ya Shekeli waambatanisha na madai ya tibaya matatizo ya msingi kama kuporomoka kwa maadili ya viongozi, nchi kushindwa kuweka vipaumbele ikiwemo elimu nk. Basi wangegoma leo kuhusu DOWANS kulipwa, Mfumuko wa bei ambao ungeweza kufanyiwa kazi kama serikali ingekuwa makini, serikali kuwajibisha watendaji wabovu nk, halafu baada ta UE wadai hela inayodaiwa

after all 5000 mnasema haitoshi hivi unajua watumishi wanalipwa sh 150,000 per month na wana familia na wanasavaivu, nyie mnaona 5000 ni ndogo, daini kuboreshewa mazingira ya elimu, hostels, maabara, maktaba viendane na viwango vya kimataifa. sasa nyie manadai hela ya kuweka matumboni na kuendea madisco, sisemi wote ila kuna baabdi ya wanafunzi..... think twice

sikilizen wanaJF, umefika wakati tuelewe haki haiji kwa miguu, haki inatafutwa na maisha yamebadilika, wanafunzi Kugoma wako right... Sio mnawaona puuzo, wameandama kumuona mtoto wa mkulima wa mjini kumweleza kero zao zitatuliwe, eti hao maasikari njaa nao wanajifanya wanatuliza ghasia tena kwakutumia nguvu, kwani kunamwanafunzi aliyebeba silaha?...maasikari hawana chamsingi kuwasaidia hata kama wataelezwa kero hzo wao wenyewe wanalia kwenye vijishuka vyao na wake zao "mshahara mdogo,sijui huduma mbovu" The logic ni hv maaskari wakae pemben wawalinde wanafunzi waandamane kwa usalama" sio mtu unatuandikia mambo ya frustrations za UE. Toa mbinu zakuwasaidia wale ni wasomi wakishindwa kujikomboa wao kamwe hawatoweza kuitumikia jamii iliyowatuma. So Aluta-CONTINUER. This is where we fight,this is where they die, this is where we stand.
 
Tatizo la entitlement hilo! Hivi hii tendency ya kutegemea vitu vya bure itaisha lini? Yes, nilisoma mlimani, lakini what I see wanafunzi tunakuwa so simplistic katika madai yetu. Hivi kweli unaweza kugomea bumu? My suggestions: Wanafunzi inabidi waje na hoja zinazoeleweka, bumu is but a small part of the equation. Wakae chini na watawala wajenge hoja za kueleweka. Huwezi kwenda barabarani kudai bumu katika kipindi hiki maisha yamekuwa magumu kwa kila mtanzania. Ndo maana wananchi wengi wanawaona wanafunzi (probably wrongly) kwamba ni wanafiki na wabinafsi. Wagomee mambo ya msingi ambayo yanawagusa watanzania wote. Kwa hili la bumu..hata kama mtaongezewa iwe 10.000.00 believe me you..haitawatosha. Mbona hamjaandamana kupinga kuongezeka kwa gharama za maisha za watanzania, kama umeme, bei za vitu..remember nyinyi ndo wasomi....

Wasomi wetu badilisheni strategies zenu..so far your move doesnt wash! And I hasten to say, you are but so simplistic!
 
Mzukaaa!! big up wenzangu na mimi vyuoni, ni kweli boom haitoshi, yan km ingewezekana iyo hali ingehamia vyuo vyote vikuu Tz, kuna vyuo vya porin tangu vianze havisikiki, yan migomo kwao haijulikani sa sijui kama wao icho kiasi kinawatosha. Makumira tupo wote hata kwa kulalamika bt ipo siku nasi tutakuwa barabarani. Washeni moto huo mpaka ikulu nasi twaja nyuma yenu. Ni jana tu hao wakuu wa bodi walikuwa wanatema pumba zao TBC. Washa washa, msiwaogope hao mbwa koko wa kikwete!
 
Jamanio vyuoni kunazalishwa mambumbumbu na sio wasomi tena, maana huu usomi usomi gani unao angalia ubinafsi kwa kiasi kikubwa namana hii, kuna elimu ya uchumi kubwa kiasi gani kutambua maisha haya ishiki kwa sasa? Mnagoma kutaka nyongeza ya 5000/- alafu kesho? Embu ulizeni kama elimu yenu mnaitumia sawa sawa, au mnasoma kujibu mitihani tu? Kama manataka kuandamana basi ingepaswa kuandamana kwa kupinga uongozi wa serikali katika kusimamia rasilimali zetu, yani umepanda umeme bei, hata kama tuko gizani hakuna aliye andamana, lini vyuoni kuta andaliwa maandamano yakupinga kupinga uongozi mbovu ulio madarakani ambao hauwezi kusimamia rasilimali za taifa hili? Au ubinafsi ndo kitu cha kwanza? Hawaoni kwa kuandaa ma andamano ya kutaka wasomi kushirikishwa katika kutatua au kuttoa mapendekezo ya nini kifanyike katika taifa letu walau kupunguza ugumu wa maisha kuliko ilivyo sasa, wmana siasa na tajiri ndo mwenye sauti, nyinyi mna andamana kwa 5000/- tafuteni heshima yenu ya usomi na mchango wenu ktk taifa walau kwa haya mnayo ona ni mazuri yani maandamano kwa kutetea taifa kwa jumla na si ubinafsi, kwanza lazima mjue impact ya hiyo nyongeza ya 5000/- leo wanao kosa mikopo ni wengi sana, nyinyi mmepata, sasa mnataka nyongeza, msiwe kama bajeti ya tz kila mwaka kila kitu kinapandishwa bei, tumieni elimu yenu, alah!!!!!!!!!!! Shabashssss
 
Tunataka updates za maandamano na siyo poroja za kweli boom alitoshi, vijana wetu wako wapi sasa?
 
Walipofika mlimani city wakaona vidume wa polisi waandamanaji wachache na wa kulazimishwa wakiongozwa na watu wasiojulikana maana daruso wamekana kuunga mkono, wametawanyika wenyewe. Waislam andaeni maandamano na nyie tuoneshe upinzani wetu dhidi ya hawa walevi wachache wanaotaka kutupotezea mda na malengo.
 
Hii migomo ni kiboko, maana hata wazazi wanachochea watoto kugoma. tofauti na zamani wazazi walikuwa wanatupinga tukigoma. Sasa wazazi nao wameona kuwa serikali ni longolongo.
 
Baada ya Boom em tuandamane kwa ajili ya kupanda kwa bei ya vitu,maisha na umeme coz tusipofanya hivo itakuwa ni sawa na kujaza maji ndani ya gunia! Anyday tena tutajikuta tunaandamana kwa ajili ya hilo tena, ndo hapo raia hawatotuelewa wataanza kuwa na mashaka na sisi.
 
Haki elimu wana ujumbe wao unao walenga wanafunzi wa elimu za secondary probably na za msingi, ujumbe unaonyesha wanafunzi walivyo watukutu wakati Mwalimu anafunzisha simu ya mwanafuzni ina inaita, tena anaonyesha lile nia jambo dogo sana, wengine wanacheza kamari, nina wasiwasi saaaana kwamba kwamtu makini atakuwa na tafsiri zaidi ya moja juu ya ujumbe kama huu, Wasekondari wanafanya haya, wa vyuo?????? wao wana andamana, utatofautisha nini na matangazo hayo?? HAKUNA UBUNIFU WA KUTATUA MATATIZO KWA VIONGOZI, KWA FAMILIA, KWA WANAFUNZI TENA MI NAOGOPA SASA KUWAITA WASOMI, AU LABDA WASOMI WA MAGAZETI TENA YA UDAKU, MAANA MTU MSOMI ANATUMIA ELIMU YAKE VIZURI, LINI KUNDI LA WASOMI LITATETEA NAFASI YA KULIKWAMUA TAIFA HILI??? TENA TAKWIMU ZINAONYESHA WANAFUNZI WENGI HATA KURA HAWAKUPIGA........!!! SASA HAO UTAWAITA WASOMI??? SI NI WANAFUNZI TU WAKAWAIDA HATA KM WAPO VYUONI NDO HAO HAO WANAO ELEZEWA NA HAKI ELIMU.
 
Tunataka updates za maandamano na siyo poroja za kweli boom alitoshi, vijana wetu wako wapi sasa?
Vijana wamesambaratishwa na FFU, barabara zote zilifungwa wakaingiza defenders kama tano hivi na tankers za maji ya kuwasha mbili kupitia huu upande wa chuo cha ardhi/Mlimani City. Ila sasa hivi defenders zimeshaondoka, kuko shwari
 

Wadau tujuzeni hali ikoje huko?
Naskia wanafunzi wamepanda mabasi wanaenda kukutana mbele ya safari.
Nimeona difenda zimebeba watu wamejikoki utadhani wanaenda kuingia kwenye msitu wenye wanyama wakali
 
Si bure hapa pana jambo, haiwezekani kila leo migomo tena kila kona ni dalili kwamba mambo mengi yapo hobela hobela.
 
Back
Top Bottom