Polisi wauaji kasulu hatimaye watoroka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wauaji kasulu hatimaye watoroka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwandiga, Mar 6, 2012.

 1. mwandiga

  mwandiga JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 1,447
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  Hii habari niliisikia kama tetesi siku ya ijumaa tarehe 2/3/2012 kwa kuwa nilikuwa nadai vihela vyangu huko Kasulu na niliahidiwa kuzipata Jumatatu nilifunga safari Ijumaa na kufika jioni na kufanya ufukunyunyu wa kujua ukweli wa hii habari. Niliyobaini ni kama ifuatavyo.

  Wale askari kama tisa hivi walioua mwananchi maeneo ya Rungwe Mpya mwaka jana walitoka lock up na kuwa mtaani, baadaye walipata uhamisho wa kwenda Kigoma na Kibondo lakini baada ya Mbunge wa Kasulu Mjini mwalimu Machari na Mhe. Mkosamali kukomalia hawa wauaji wachukuliwe hatua na sio kuhamishwa, uhamisho wao ukasitishwa mara moja ila waliohama kituo cha kasulu ni OCD, OCID NA OCS na tayari wengine wapya wamekuja wawili kati yao nilikuwa nao hapa town kigoma.

  Baada ya uhamisho huo kusitishwa hawa polisi wakawa mtaani tu ila wakapata habari kutoka Kigoma kuwa wanatakiwa wakamatwe. Kilichotokea ni wote kutoroka usiku wa manane wengine wakiondoka na wake zao na wengine wakiwaacha. Wake zao nimeonyeshwa walipo sehemu zao za biashara kwa wale waliobaki.

  Hivi kweli hapa kulikuwa na dhamira ya dhati kuwaadhibu hawa polisi? Ndio maana kila siku wanaua raia na hawachukuliwi hatua wanachofanya ni kulindana tu. Hongera polisi Tabora kwa kuonyesha mfano mzuri wa kuwafunza tabia polisi wenye tabia za kuua ovyo raia
   
Loading...