Polisi waua raia

Kauli ya PM!

Piga tu! Pig tumechoka! Uawa! Na ndiyo inaendelea kwa matendo sasa!
 
Usitetee uovu wa polisi wewe.
Polisi risasi siku hizi wanapiga risasi ovyo hata sehemu isipohitajika kufanya hivyo.

umefanya utafiti lkn? zamani hata wakiua hakuna aliyekuwa anawahoji, ni mara chache sana, lkn siku hizi kila mtu mwandishi wa habari ukifanya lolote tayari limerushwa hewani. polisi naamini wako makini zaidi ukilinganisha na zaman
 
mimi niliwahi kumpeleka mwizi wangu polisi na vidhibiti vilikuwepo kabisa kilichotokea tukaishia kupigwa tarehe kila mara mpaka tukachoka huku mwizi akiwa na mawasiliano ya karibu sana na huyo polisi. tukienda tunaambiwa mwizi kapata matatizo atakuja siku ingine. Kifupi mwizi aligeuka kuwa bosi wa polisi na sisi walalamikaji. nikaona muda wangu unazidi kupotea tukaachana nao. Inaonekana polisi wanajua kuwa watu hawako tayari kupoteza muda wao hivyo huanzisha mazingira ya kuzungusha mpka mlalamikaji anachoka.
 

mimi niliwahi kumpeleka mwizi wangu polisi na vidhibiti vilikuwepo kabisa kilichotokea tukaishia kupigwa tarehe kila mara mpaka tukachoka huku mwizi akiwa na mawasiliano ya karibu sana na huyo polisi. tukienda tunaambiwa mwizi kapata matatizo atakuja siku ingine. Kifupi mwizi aligeuka kuwa bosi wa polisi na sisi walalamikaji. nikaona muda wangu unazidi kupotea tukaachana nao. Inaonekana polisi wanajua kuwa watu hawako tayari kupoteza muda wao hivyo huanzisha mazingira ya kuzungusha mpka mlalamikaji anachoka.
 

yeah, mbinu hizo wanazo pia, lkn ni rahisi kuzidhibiti. mfano, ukienda kwa bosi wake, ukatoa malalamiko, utabadilishiwa mpelelezi. mimi nishabadilisha wapelelezi kwa ujinga kama huo, lkn kila akinizingua naenda kwa oc cid au ocd kulalamika, mwisho wa siku kesi ilipelekwa mahakamni na jamaa alihukumiwa miaka 3.

Polisi ni waajiriwa wetu, sie ndo tunawalipa mishahara kwa kodi tulipazo, kuwasimamia ili watimize majukum yao, ni jukum letu pia. inakuwaje tuwalipe sisi lakini tusiwasimamie? tukikaa pembeni na kulalamika vijiweni, wataendelea kutuchezea
 
ww una akili kweli mtuhumiwa yuko mikononi mwa polisi ww unataka umwadhibu?. Safi sana polisi
 

Polisi hana mamlaka ya kuua. Ndiyo maana nchi za wenzetu polisi akiua huwa uchunguzi kuhakiki. Haki huwa inatendeka. Kwa Tanzania hii kitu haipo. Ndiyo maana polisi wanakuwa na mabomu ya machozi, au "hand grenade" za kujilindia. Hizi "hand grenade" huwa maalumu sanasana zinajeruhi tu.

Leo hii ukishikwa na polisi ukataka kutoroka atakulima risasi ya mgongoni. Wakati anapaswa kutumia nguvu kukudhibiti na ikishindikana, kama una silaha, anapaswa kukulima risasi ya mguu, mkono, au popote ILA ASIKUUE.
 

Polisi kutokuvaa vifaa vya kazi yake nani alaumiwe? Mwananchi? Unadhani ni kwanini Polisi wa Tanzania si watu wema? Zamani tulikuwa tunakimbilia polisi. Siku hizi, ukishitaki polisi ishu ambayo ni ya hatari, wanaenda kumwambia muhusika, au akikamatwa anaachiwa.

Leo hii Polisi wakifanya msako nyumbani kwako, lazima watakuta "bangi" japokuwa wewe si mshiriki wa hiyo kitu. Sasa jiulize hiyo "bangi" imetoka wapi?
 

kwani we kwa mtazamo wako unadhani polisi analenga kuua? lengo ni kukudhibiti usitoroke, sasa katika kukudhibiti, risasi inaweza kupita sehem siyo. mfano, polisi analenga miguu, lkn wkt risasi inatoka, anayekimbia akawa anataka kudesh down, risasi badala ya mguu hupitia kichwa.

Lakini kwa mtu anayejitambua, kwa nini uanze kufukuzana na polisi? jambo gani halimaliziki jamani tanzania hii? Liyumba si huyo kashinda kesi? woga wako kifo chako. kwa msataarabu yeyote hawezi kujaribu kutoroka polisi ili hali amesha wekwa chini ya ulinzi, kujaribu kufanya hivyo inaashiria nia yako si njema.
 

ningefaham kwanza umri wako, wewe unayesema kuwa zamani ulikuwa unakimbilia polisi. huu ni uongo. watoto wamekuwa wanaambiwa utapelekwa polisi wewe, akifanya kosa mtoto anaambiwa atapelekwa polisi. hii ilisababisha kukuwa kwa uelewa kuwa, polisi si mahali pazuri pa kwenda. ukiangalia mkakati wa jeshi sasa hivi, wanakwambia wanapambana na kufuta uelewa huo. Enzi zile polisi akikatiza kijijini basi hata aliyekuwa anaelekea sokoni anabadili njia, haendi tena. sijui unasema zamani ipi wewe.

Leo hii ukiongea na askari, wapo wanaomlaum IJP mwema kuwa kaharibu jeshi, hoja zao nyingi ni kuwa, raia hamwogopi tena polisi. kwa hiyo, wakati zamani polisi aliogopwa, leo hii polisi haogopwi tena, ndio maana hadi baadhi ya watu wanapinga sera za jeshi za polisi jamii (community policing) inayowalazim polisi kuwa karibu na wananchi. kufanya kazi kwa ubia
 

ni kosa la mpiga kura kuchagua viongozi wezi. maana kama ni kodi zinakusanywa, lkn kwenye bunge la bajeti utaambiwa kasungura kadogo
 
ww una akili kweli mtuhumiwa yuko mikononi mwa polisi ww unataka umwadhibu?. Safi sana polisi

hapo sasa!!!! kwa nini wasingejipanga kumtolea ushahidi mahakamani? tena kwa kuonesha kiwango cha juu cha ukaidi, eti walitaka kumnyang'anya toka mikononi mwa polisi. watu bado hatujielewi. halafu katika matukio kama hayo, mtu aliyeibiwa hata hayupo, sasa ambaye hajaibiwa ndo anajifanya ana uchungu kuliko aliyeibiwa.
 

Ashakum si matusi, nadhani ntamaholo unahitaji shule ya "balistic science"...

Risasi iliyofyatuliwa kutoka kwenye AK47 inachukua "dakika" ngapi kufikia kusudio (target) umbali wa mita 300-400? (Mwendokasi wa AK47 ni 710 mita kwa sekunde).

Maelezo yako hayana mashiko!
 
Last edited by a moderator:

hujawahi kuona actors kama Jckie Chen wanakwepa risasi? ule ni mchezo wa kuigiza lkni hayo mambo huwa yanatokea.

sek moja hyo wewe unafikiria hivi, mwenzio anafikiria vingine. inawezekana kabisa.

Lakini wewe unasapoti sisi wananchi kuanzisha mapambano na polisi?
 
umefanya utafiti lkn? zamani hata wakiua hakuna aliyekuwa anawahoji, ni mara chache sana, lkn siku hizi kila mtu mwandishi wa habari ukifanya lolote tayari limerushwa hewani. polisi naamini wako makini zaidi ukilinganisha na zaman

Zamani zama zipi? Kama mliyafanya hayo zamani basi kwa wakati huu technology itawaumbua sana.
Rushwa polisi
Ujambazi polisi
Kuua raia polisi
Kubambikia kesi polisi
Hivi wakoje hawa viumbe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…