Kama kawaida yao nguvu nyingi akili kidogo.
Polisi wilayani Kaliua mkoani Tabora wamempiga risasi na kumuua raia mmoja aliekua miongoni mwa kundi la wananchi waliokua wanakabiliana na polisi hao.
Wananchi walikua wanawataka kuwaadhibu wezi wa mifugo waliokua mikononi mwa polisi.
Note-kama unajipenda kaa mbali na polisi ukirusha mchanga wanarusha risasi.
Kumbe jiwe haliuwi enhee? Wacheni kuharibu amani kwa kuendekeza ujinga
Kwa hyo ulitaka muue kisha mseme polisi wamesimamia mauaji? Kwa nini walipotaka kumwokoa nyie mkaamua kukabiliana na polisi? Pumb. Vu zenu
Mimi na wewe hatukuwepo, lkn melezo ya mleta mada yanaashiria principle hyo ilitumika. We mtu anadiriki kuandika "tunakabiliana na polisi". Mpaka kukabiliana tayari tayari wamepewa onyo
Polisi sikuhizi wanafundishwa kulinda wahalifu na kuua raia na sio kudhibiti uhalifu.
Polisi huwa na vifaa vingi sana na mbinu za kukabiliana na Raia. Sioni sababu yao kutumia silaha moto. Kwanza wanakuwa wamevaa vifaa vya kujilinda kimwili. Pia raia anakuwa hawana silaha moto.
Watasema huyo mwananchi alikuwa na Silaha na alitishia usalama wa polisi.
Yaani raia mwenye jiwe anatishia usalama wa askari mwenye mguu wa kuku!
Kwa akili zako,kufa jambazi na kufa raia mwema kipi kina afadhari? Crazy typ.
Kwanini Polisi nao wasiokote mawe wawapige hao waliobeba mawe? Siku wananchi wakipata silaha (kama za polisi), amani itatoweka nchini. Hali itakuwa kama ya Congo, Sudani, CRA n.k.
raia kuua raia mwenzake kwa tuhuma ambazo hazijathibitishwa naye ni mhalifu.
na kwa mjibu wa viapo vya askari, ukiangalia sheria iliyounda jeshi hilo, kulinda watu na mali zao, kulinda watuhumiwa na wahalifu wenyewe ni kazi ya polisi kufanya hivyo, kuhakikisha watu wote wanakuwa salama.
Na sheria zinaruhusu matumizi ya nguvu katika kuokoa maisha.
tuanzie hapo, kwa nini mtuhumiwa anakamatwa na baadae kuachiwa?uko sahihi mku ila tatizo hapo kila mmoja kakosa imani na mwenzake. lkn pia raia hujichukulia sheria mkononi hasa pale wanapowapeleka wahalifu polisi kisha wanaachiliwa na kuanza kuwatishia maisha wale waliowapeleka polisi. hali hii huwakatisha tamaa wananchi au raia na kuamua kujichukuliaa sheria mkononi. Kiukweli haukutakiwa kuwa hivyo.
tuanzie hapo, kwa nini mtuhumiwa anakamatwa na baadae kuachiwa?
kwani wananchi hawana silaha hizo? si polisi kila siku wanauwawa kwa risasi? halafu chukulia wako polisi wawili, ndio wanataka kuokoa maisha ya mtu anayetuhumiwa kufanya kosa, lakini wananchi wanaotaka kuua mtuhumiwa wapo 20 hadi 50. polisi atachukua mawe mangapi kukabiliana na watu 50? tumia akili wewe
Rushwa ndio tatizo.