Polisi waua mtuhumiwa ujambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi waua mtuhumiwa ujambazi

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Jul 29, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  Wakamata wengine wanane
  [​IMG]
  Kamanda Suleiman Kova  [FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuua mtuhumiwa wa ujambazi na kuwakamata wengine wanane akiwemo askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) MT 75826 ACP Julius Abdaham (32).[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Jeshi hilo lilidai kwamba mtuhumiwa aliuawa wakati wakirushiana risasi katika eneo la Manzese.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Miongoni mwa watuhumiwa hao wa ujambazi yupo mwanamke aliyetajwa kwa jina la Beatrice Charles (31), mkazi wa mjini Arusha ambaye amekuwa akitumiwa kufanikisha uporaji wa mali za wananchi.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda wa kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema jana kuwa, kati ya watuhumiwa hao wanne walifikia katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Bismark ya Manzese Midizini wakitokea mikoa mbalimbali nchini.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema watuhumiwa wengine walikamatwa Sinza na maeneo mengine baada ya kutajana.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema awali waliwakamata watuhumiwa wawili ambao walikuwa wamejificha eneo la Sinza. Alisema watuhumiwa hao ambao hakuwataja majina yao, baada ya kukamatwa waliwataja wenzao wanne ambao walikuwa wamefikia Manzese kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema polisi walipofika kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni, mmoja wa watu hao aliyetambuliwa kwa jina moja la Jumanne, mkazi wa Dodoma, alianza kuwafyatulia risasi askari.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]"Mtuhumiwa huyu ambaye ni marehemu kwa sasa, alipogundua kuwa wamezingirwa na makachero, alitoka ndani ya chumba alichokuwa na wenzake na kupanda juu ya paa la nyumba hiyo na kuanza kuwashambulia kwa risasi polisi," alisema[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kova alisema katika majibizano hayo ya risasi, mtuhumiwa huyo alizidiwa baada ya kufyatuliwa risasi ya kifuani na alikufa wakati akikimbizwa hospitali ya Mwananyamala.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema jambazi huyo alikuwa akitumia silaha aina ya SMG yenye namba 5620116238 ambayo ilikutwa na risasi 22 tu kati ya 60 ambazo awali zilikuwemo kwenye magazine yake.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Kova aliwataja watuhumiwa waliokamatwa katika tukio hilo ni askari wa JWTZ Koplo Julius (32) maarufu kama Kwayo ambaye yupo katika kikosi cha 303 KJ mkoani Arusha, Blasiusy Kiga maarufu kama Nyembea (33) mkazi wa Kariakoo na Beatrice.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Kamanda Kova alisema katika msako wa kuwakamatwa watuhumiwa wengine, ulifanikisha kuwatia nguvuni watu watatu wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 281 ABD aina ya Toyota Mark 11.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Aliwataja watu hao kuwa ni Peter Juma (32), Mkazi wa Kinondoni Moscow, Julius Mwita (28) mkazi wa Yombo Vituka na Julius Chacha (32) mkazi wa Msang'o.[/FONT]


  [FONT=ArialMT, sans-serif]http://www.ippmedia.com/
  [/FONT]
   
Loading...