Polisi watawanya msafara wa Mbowe Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi watawanya msafara wa Mbowe Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Jan 25, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Polisi watawanya msafara wa Mbowe
  Na Mussa Juma

  MSAFARA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana ulivunjwa wa polisi kwa madai kuwa ungesababisha vurugu.


  Tukio hilo lilitokea jana saa 12.00 jioni baada ya Mbowe kumaliza kuhutubia mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa udiwani wa Kata ya Kati, Seif Simba uliofanyika katika eneo la YMCA.


  Mbowe mara baada ya mkutano huo aliamua kutembea kwa miguu kwenda katika ofisi cha Chadema zilizopo karibu na Stendi Kuu ya mabasi mjini hapa.


  Mbowe ambaye alikuwa akisindikizwa na wafuasi wengi wa chama hicho mara alipofika katika eneo la Stedi ya mabasi polisi waliokuwa na mabomu ya machozi wakiwa katika magari matatu, waliwaamuru watu waliokuwa katika msafara huo watawanyike na mbowe apande gari lake aondoke.


  Hata hivyo, Mbowe alipinga amri hiyo na hivyo polisi walitishia kuwapiga mbomu ya machozi watu hao, hali ambayo iliwafanya watawanyike.


  Mbowe naye aliingia katika gari lake na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na magari hayo ya Polisi akielekea katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


  Hata hivyo, Polisi hao walilishikilia kwa muda gari la matangazo la chama hicho aina ya Fuso kuwa lilikuwa likisababisha mikusanyiko ya watu.


  Awali akihutubiua mkutano huo aliwataka wanachama wa chama hicho leo kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kwamba mara baada ya kupiga kura wasiondoke kwenye vituo vya kupigia kura kulinda kura zao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 25, 2009
 2. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mbowe atamba kuibuka na ushindi leo  na Mwandishi Wetu, Arusha
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ametamba kuwa chama chake kitaibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani wa Kata ya Kati, katika Manispaa ya Arusha.

  Mbowe ambaye aliwasili mjini hapa juzi, aliweza kubadilisha hali ya upepo wa kisiasa, tofauti na siku zote ambazo kampeni hizo zimekuwa zikifanyika katika Manispaa ya Arusha.

  Akihutubia mamia ya wananchi wa mji huo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara, juzi na jana katika kata hiyo, Mbowe alisema chama chake kitaibuka na ushindi kwenye uchaguzi huo na chaguzi nyingine nne zinazofanyika kata nyingine hapa nchini.

  “Nimekuwa hapa tangu jana, nimefarijika mno na mapokezi na jinsi watu mnavyojitokeza katika mikutano yangu naomba hali hii iwepo hadi kesho (leo) sote tujitokeze na kumpa kura mgombea wetu wa CHADEMA, Self Simba,” alisema Mbowe.

  Alisema wakati umefika kwa wakazi wa Manispaa ya Arusha kubadilika sasa na kuelewa kuwa nchi yao inaliwa na wajanja huku hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na wahusika.

  Mbowe alisema CCM inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete inapaswa kuondolewa madarakani, imekuwa haionyeshi nia njema huku baadhi ya viongozi wamelenga kujinufaisha kwa kujiuzia nyumba za serikali kwa bei poa.

  Aliwataka Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyao kuelewa kuwa umefika wakati wa kuungana ili kutetea masilahi ya taifa na kwamba jambo hilo linawezekana na kuwa njia pekee ya kuing’oa CCM madarakani.

  “Nawaambia bila kujali vyama vyetu vya CUF, CCM, TLP, CHADEMA na hata UDP na vingine, Watanzania wenzangu tuungane tukombowe nchi yetu inamalizwa na mafisadi ambao wamewasahau ninyi wavuja jasho,” alisema Mbowe.

  Mbowe alitarajiwa jana jioni kufunga kampeni za udiwani Kata ya Kati, huku CHADEMA ikichuana vikali na mgombea wa CCM, Abdul Tojo.
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Zenji hayo ya mambo ya mabomu na washawasha yashazoeleka na hivi sasa wameanza kujiandaa kwa msimu ujao wa 2010 ,naona waTanganyika sasa kazi wanayo ila mji wenu ni mkubwa mnaweza mkasimama na polisi kisha mkatokomea kusiko julikana ,Zenji ni ndogo sana haina pa kukimbilia.mkizingirwa mmebanwa mnakula marungu.
  Tena huko hata mashine za kivita mnaweza mkazipata kutoka nchi jirani mkarushiana nao marisao ,ikiwa majambazi wanarushiana nao risasi na polisi wakaingia mitini,kwani wao hawaogopi kufa.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Jan 25, 2009
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Lakini mkuu mwiba unapenda vurugu bwana,

  Man umenichekesha sana
   
Loading...