Polisi wapata mafunzo kukanyaga moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wapata mafunzo kukanyaga moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, May 5, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Naibu Kamishna, Suleiman Kova akipita juu ya moto jana jijini Dar es Salaam baada ya kupata mafunzo kutoka taasisi ya Peak Perfomance ya kujengewa ujasiri na uwezo wa ujiamini zaidi katika utendaji kazi wa kila siku. Picha ya Jeshi la Polisi​
  Boniface Meena
  MAOFISA wa ngazi za juu katika Jeshi la Polisi nchini wakiongozwa na Mkuu wa Jeshi hilo (IGP), Said Mwema jana walihitimu mafunzo ya kujijengea uwezo na ujasiri kwa kukanyaga moto.

  Mbali na IGP Mwema, maofisa wengine wa polisi walioshiriki zoezi hilo jana ni Mkurugenzi wa Upelelezi nchini (DCI), Robert Manumba na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

  Mafunzo hayo yanayoelezwa kuwa yataendelea kwa siku mbili mfululizo, yalifanyika katika bwalo la polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Katika mafunzo hayo yanayotolewa na taasisi ya Peak Performance ya jijini Dar es Salaam, maofisa hao wa polisi walipita mmoja baada ya mwingine juu ya moto uliokuwa ukiwaka wakiwa wamevua viatu.

  Mafunzo hayo ambayo yameshirikisha viongozi wa juu wa jeshi hilo kuanzia cheo cha kamishna wasaidizi (ACP) na makamishna wengine, pia yatashirikisha viongozi wengine na askari nchini kote.

  Imeelezwa kuwa mafunzo hayo ni ya kujijengea uwezo na ujasiri kwani kupita kwenye moto ni kuonyesha hakuna linaloshindikana likiamuliwa kufanyika.

  Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa madhununi ni kuhakikisha askari wote wa jeshi hilo wanapatiwa mafunzo ya aina hiyo kwa awamu kulingana na uwezo wa kifedha ndani ya jeshi la polisi.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Polisi wapata mafunzo kukanyaga moto
   
 2. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani 2ngewapa mafunzo ya kurusha ndege au kupambana na wezi wa kisasa, haya ni mazingaobwe
   
 3. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,164
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  This country bwana.Hili nalo linahitaji fedha?kwani hao police hawawezi kukusanya kuni na kuziwasha kisha wakapita juu yake?au huu moto ni tofauti na huu wanaotumia wake zetu na mama zetu kuchemshia mchicha?
  Ebu ngoja niende nikachangie kule kwenye baraza jipya kwanza maana huu uzi unazidi kunipandisha hasira kwa ufisadi wa..............
   
 4. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 476
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Tofauti ya moto wanaotumia wao na ule ambao wako likely kukutana nao kwenye mazingira yao ya kazi ni kwamba huu wamemwaga mafuta na hakuna vitu kama mkaa mkaa au majivu hivyo unapokanyaga moto unazimika maana hakuna hewa unapo nyanyua mguu unawaka tena. Unawashwa na ule uliko pembeni, kama vile moto unavyoweza kuruka kutoka eneo moja kwenda lingine. Mfano wa jiko la tambi linavyoweza kuwashwa na utambi 1 wenye moto. Hii umfanya mtu udhani umekanyaga moto kumbe unapokanyaga unazimika, ukiondoa mguu unawashwa na ule uliokuwa pembeni. Lakini ule unaokuwa na majivu kama ya nyasi au mkaa mkaa unapokanyaga mkaa unang'ang'ania kwenye ngozi chini ya mguu na hivyo kukupa maumivu makali. Hawawezi kupita juu ya moto wenye mkaa mkaa au majivu.
  Japo maumiviu wanayapata na huo ndo ujasiri.
   
 5. M

  Makupa JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,741
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mkuu sii siri haya mafunzo yalikuwa ni zaidi ya mazingaobwe inabidi yatafutiwe jina kazi kwenu wan jf
   
 6. fakenology

  fakenology JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 763
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  badala ya kupambana na rushwa na ufisadi na wezi wa twiga wenyewe wanapambana na wadai haki kwa maandamano na moto wa mazingaombwe
   
Loading...