Polisi wampiga Risasi kijana na kumuua kituoni Arusha

Jiwe huwa hajui madhara ya Kauli zake..
Lumumba nao Uzi kama huu hawatokei kutoa pole/kukemea Wanajaa kwenye nyuzi za Lissu tu..Maana wanajua Maagizo ya Mwenyekiti wao yanatekelezwa..
 
Rais John Magufuli ametaka askari wa Jeshi la Polisi kutoshtakiwa kutokana na makosa yanayojitokeza wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwamo kutuhumiwa kuua wahalifu.Akizungumza jana wakati wa sherehe za kufunga mafunzo kwa askari wa jeshi hilo katika Chuo cha Taaluma za Polisi, Kurasini jijini hapa, Rais Magufuli huku akiahidi kuwa nao bega kwa bega alisema askari wanafanya kazi kubwa ya kuimarisha usalama wa nchi.
(hii ilikua december 28, 2018)
 
Tuache kukurupuka, tungoje ushahidi kami, kituoni kuna watu wengi, na sio rahisi kumpiga mtu risasi, ingekuwa mbali na hapo ni rahisi.

Tuutafute ukweli, hata hao polisi ni watanzania , tuwape haki zao, juu ya mapungufu yao mengi.
Kwa mujibu wa M-blog kichana mmoja huko Arusha amepigwa Risas mikononi mwa polisi mbele ya kaka yake siku ya alhamis na mwili wake kupelekwa hospital ya Mount Meru.

Wakati mahojiano yanafanyika na wazazi, ndugu na jamaa pamoja viongozi wa ENEO anapoishi mkoani Arusha wote wamekiri kwamba kijana huyo Hana tabia mbaya kwenye jamii na hata angekuwa na tabia mbaya awakutegemea apatwe na mauti kwa sababu alikamatwa nyumban na alifungwa mikono na kupelekwa kituoni.

Kaimu kamanda wa polisi Arusha alipoulizwa ameeleza kwa kujiamini kuwa kijana huyo ni mualifu na kwamba alipigwa risas wakati anamnyang'anya Askari bunduki kituoni. Anadai kwamba kijana huyo amekuwa akituhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Hii taarifa ina pande mbili moja ikidai marehemu ni mualifu na nyingine ikidai marehemu ni mtu mwema kwenye jamii.Je , Kati ya RPC na viongozi wa Kijiji pamoja na wanakijiji nani anajua tabia za raia? Je, Kama kweli anatuhumiwa kwa makosa flani anatakiwa kuuwawa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom