Naunga mkono hoja, Scotland Yard waitwe kusaidia, hata BOT ilipoungua, polisi wetu walishindwa hivyo Scotland Yard waliitwa. Na rushwa ya Rada ya BAE pia tulishindwa Waingereza wenyewe wakafanya kila kitu, hadi aliyehonga akakiri kuhonga ila akaomba asitoe majina bali alipishwe tuu faini kwa non disclosure na ndio hiyo cheji ya rada.
Hata kampuni ya Kagoda iliyokwapua bilioni 40 za EPA tumeshindwa kuichunguza hadi kesho, hivyo ni kweli tuombe msaada watusaidie na hata suala la MV Bagamoyo wanaweza kusaidia!.
Paskali
Sawa Kaka
Haya maridhiano, kutaka kufanyike uchunguzi wa hili na lile kwa mtazamo wangu;
Nitarudia........-Kichaka cha maridhiano yataficha na yatawaficha wahusika wa kijinai Tanzania yetu.
Yaani I am so convinced hiki kitu kinachoitwa 'maridhiano' hakitakuja kutoa Haki na Ukweli kitu ambacho kimaandishi ndicho kinavyodai....Unasikia minong'ono Ati Tume ya haki na ukweli kama kile cha Desmond Tutu(R.I.P).
Wakati ukweli ni kuwa Jinai ilitumika katika kukandamiza juhudi za Mwafrika kule Afrika ya Kusini wakitumia mbinu zote vitabuni mpaka kuuwa, Makaburu walipewa kichapo cha kiganja cha mkono ikiwa ni matokeo ya tume hiyo.l Na waliondoka wakipumua kwa uhafueni ule....
Ukweli ni kuwa chombo kile kilianzishwa just so kuwa protect Makaburu na Wazungu waliwasaidia kuwepo madarakani, kwani walihofia kuwa udhalimu wao utakuja kulipizwa kisasi na Waafrika ambao walikuwa wanatarajiwa kushika Dola na sheria ambazo zilitumiwa kufanya Udhalimu wao, kugeuzwa na kutumiwa dhidi yao....That was their main concern! Period.
Naamini kwa namna moja au nyingine CHADEMA wana mkono wao katika mambo mengi yaliofanyika kuchafua taswira ya Siasa pamoja na Serikali awamuni kwa kutumia mbinu zote vitabuni ili kuleta mabadiliko wanayotaka. Na kati ya mbinu hizo nadhani ni pamoja na kutumia njia zisizo sahihi na zinazovunja na kukejeli Dola na sheria kijinai! wakiwa na washauri wa nje! Sasa kutokana na mabadiliko ya mazingira ya Kisiasa kufanyika(badiliko la uongozi) walikuwa hawana budi ila ni kutubu na kusamehewa, na kwavile wanajua hakuna atakaye kaa kimya milele kwa kutaka ukweli na haki utendeke(pande zote) kujua yaliyojiri kama yalivyotokea South Afrika ( Serikalini na CHADEMA )basi umuhimu upewe wa kuanzisha Tume kama ya Afrika kusini alimradi kunakuwepo na 'forgivness' fulani ambao Mbowe tayari ana enjoy wakati wapo wengine ambao wanaona their grieverance hazifanyiwi kazi.....au pamoja na Waalikwe wachunguzi kutoka nje(not independent) bali mbadala wa Vyombo vyetu(watu wetu weusi) na hapo ndipo ulipo msuguano wa majabali wa CHADEMA hapo ndimo kunakokuja kufunikwa jinai za wazungu hapo ndipo kunaonekana uwepo wa mapungufu ya uchunguzi wa kina wa matukio yote, na hapo hapo ndipo naona hakuna umuhimu wa kualika wachunguzi wa nje kwani haya yote ni matokeo ya Tamaduni na mila zetu za Ukarimu na Amani ni matokeo ya kukubali uonevu kutoka kwa waonevu wetu wazungu kwani madhara yake yanaonekana kupeleka kuonyesha mapungufu ya vyombo vyetu vya Usalama katika kutatua Ufisadi, Jinai, Rushwa n.k zinazohusishwa na Viongozi nchini na wale walio nje (wazungu-mabeberu)Wakati ukweli ukifunikwa! Kwani ukitazama mlolongo wa visa alivyovitaja Kaka Pascal utaona karibu vyote vilifunikwa na wahusika kwa namna moja au nyingine kuwa kuna watu nje ya nchi wamehusika na masuala hayo.
Hayo juu ni maoni yangu na yametoka na vianzo humu humu