Polisi wamekamata kilo 40 za dawa za kulevya Tegeta, Dar es Salaam

Polisi wamekamata kilo 40 za dawa za kulevya Tegeta, Dar es Salaam

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,111
Reaction score
34,943

Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi bilioni2.

Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.

Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwa kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.

"Ni kweli tukio la aina hiyo lipo lakini watu kama hawa siwezi kusema moja kwa moja ni Mchungaji ndio muhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara hii,"Alisema Nzowa.

Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka hadharani ukweli wa mambo.

Chanzo: MillardAyo
 
Mkiambiwa baadhi ya viongozi wa Dini wanajihusisha na madawa ya kulevya munasema munavunjiwa heshima.......................!!!Kerosini mafuta ya taaaa..................nyambafu
 
Kila kitu ni dili tu sasa hivi, nimeshangaa sana asubuhi napita pale Biafra naelekea kazini nikakuta alama ya Wauza Unga (viatu kutundikwa kwenye waya za umeme) na jirani kuna tawi la CCM na bendera inapepea......pata picha hio sasa
 
Hii title na yenyewe ina utata. Sasa hapo aliyekamatwa ni mchungaji au watu waliokuwa katika nyumba inayomilikiwa na mchungaji?

kwenye uzi wa CHONJI waislam walishambuliwa sana kuwa ndo vinara wa biashara hii,ila biashara hii haina mwenyewe,kwakua haina kodi,haina ushuru haina gharama zozote za kisheria,haya unga umekutwa kwa MCHUNGAJI SASA,Mchungaj anatokaje hapo?
 
Hahahahaaa... basi tufanye sio heroin ni material ya kutengeneza sakrameti takatifu.Aleluyaaaaa!!!

Hebu someni hapa:

Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.
 
Shida haiko kwa viongozi wa dini,shida iko kwa serikali ya ccm inayowalea,maana hao wafanya biashara huifadhili ccm kwenye uchaguzi. Ccm inalea huu ujinga.

Utashangaa hakuna maelezo zaidi ya hayo yatakayotokewa kuhusu hao watu,itaisha kimia kimia. Ccm ni ebola,endeleeni kuilea.
 
Habari IPO kiudaku maana waliokamatwa sio wachungaji.
 
mbona mzee wa upako nayeye kalewa mipombe na kufwatua risasi hovyo river side huku amtishia muuza chipsi yeye nimtu wa systemz,shame on u all mnaoweka dini kama ngao yenu yakufanya maovu.fyuuuuhh
 
Huwa nina mashaka sana na hawa wachungaji wa makanisa mapya makubwa sijui kwanini
 
Hebu someni hapa:

Mbona unatetea sana au na wewe ni mnufaika wa hiyo kitu. Acha kwanza uchunguzi ufanyike, kama hiyo nyumba huyo mchungaji kaipangisha kwa hao watu, kuna uwezekano mkubwa kuwa hahusiki, lakini kama na yeye anaishi humo, hilo dili analijua sana, huwezi kukaa na watu nyumbani kwako unaona mambo yao supper halafu hujui kazi gani wanafanya.
 
Back
Top Bottom