Polisi wamefanya aibu ya mwaka Arusha

Polisi wamefanya aibu ya mwaka Arusha

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
4,019
Reaction score
2,930

RAFIKI yangu Kalasinga wa kule Njiro, Mrenyii wa kituo cha mabasi na Mrema wa pale kituo cha Vifodi Arusha ndio walionituma leo niulize kama askari walisoma kanuni za maadili za Jeshi la Polisi ukutani kabla ya kwenda kumkamata Godbless Lema?

Kanuni hizi zipo kila kituo cha polisi, kama kuna wengine hawazisomi huko naomba wasome hapa. Kanuni za maadili za Jeshi la Polisi Kamanda wa Polisi wa Arusha anazijua, Mkuu wa Polisi wa wilaya anazijua, na Mkuu wa Upepelezi ambaye kwa namna ya pekee alinikasirikia nisihojiane naye bila shaka naye anazijua.

Haya si maneno yangu, ni ya baadhi ya wakazi wa Arusha, pamoja na hao ambao nimewataja hapo juu. Wanahoji utendaji wa Jeshi la Polisi jijini Arusha lilivyojiaibisha. Lilivyotumika kisiasa bila kutumia akili yake.

Sisi askari wa upande wa polisi jamii wenye nia na mapenzi mema kwa nchi yetu turudie kuzisoma kanuni hizi na maadili yao.
Kanuni hizi zinasema: "Nikiwa ofisa wa polisi nina wajibu wa kutekeleza sheria, wajibu wangu ni kuwahudumia watu, kulinda maisha na mali.

"Kuwalinda wasio na hatia dhidi ya udanganyifu, dhaifu dhidi ya ugandamizaji au vitisho na utulivu dhidi ya vurugu au fujo, kuheshimu haki za kikatiba za raia wote katika uhuru usawa na haki.

"Nitatunza heshima yangu binafsi kama mfano kwa wote, kuwa jasiri wakai wa utulivu na wakati wa hatari. Sitakuwa na dharau au dhihaka, kuwa na uvumilivu na kujali ustawi wa wengine.

"Nitakuwa mwaminifu kimawazo na kimatendo katika maisha yangu binafsi na ya kijamii. Nitaonyesha mfano wa kufuata sheria za nchi na kanuni ya idara yangu. Chochote nitakachoona au kusikia ambacho ni siri au ambacho nimeaminiwa kutokana na wadhifa wangu kitakuwa siri isipokuwa tu pale itakapobidi kufichuliwa katika kutekeleza wajibu wangu.

"Sitaingilia au kuruhusu hisia binafsi, chuki, uhasama au urafiki viathiri uamuzi wangu, sitakubaliana na uhalifu. Nitatekeleza sheria kwa heshima na inavyopasa bila woga au upendeleo, uovu au nia mbaya.

"Sitatumia kamwe nguvu za ziada bila sababu, ninatambua kuwa beji yangu ni ishara ya uaminifu wangu kwa umma, nitakuwa mwadilifu kwa umma na kwa maadili ya kazi za polisi. Nitajitahidi muda wote kufikia malengo hayo na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, kwa chaguo la kazi ya kutekeleza sheria."

Polisi ambao hadi leo sijapata jibu kama wamemkamata aliyeua mwanachuo kuile Arusha, ndio walioamua kutokulala, kwenda kukesha nyumbani kwa Mbunge wa Arusha mjini, Lema kwa bunduki, mabomu, mbwa na kuwekeza kila aina ya mbinu eti kumkamata.

Nimeombwa niulize huyu Lema alifanya kosa gani kubwa ambalo angesubiriwa kesho yake asingeonekana?
Je, mbunge huyu angeweza kutoroka kwa sababu ya kauli ya kumwambia Mkuu wa Mkoa kuwa anakuja kama anaenda kwenye "Send Off"? Kama mbunge anakamatwa kwa vitisho hivi, hizo kanuni tunazotaja hapo juu zilizingatiwa?
Maneno haya kwamba: "Sitaingilia au kuruhusu hisia binafsi, chuki, uhasama au urafiki viathiri uamuzi wangu, sitakubaliana na uhalifu.

"Nitatekeleza sheria kwa heshima na inavyopasa bila woga au upendeleo, uovu au nia mbaya. Sitatumia kamwe nguvu za ziada bila sababu" nimetumwa niwaulize nguvu waliyotumia kumkamata Lema kweli ilihitajika?

Je, hapa kulikuwepo na chuki au uhasama katika maamuzi yaliyofikiwa katika kumkamata mbunge huyo?
Kwanini jeshi letu litumike kwa mambo ya aibu hivi? Jeshi letu linazidi kushuka hadhi siku hadi siku sio kwa kuwa kanuni zao ni mbovu, kanuni zao ni nzuri isipokuwa hazifuatwi, na viongozi wakubwa wa jeshi ndio viongozi wa kuvunja kanuni hizi.
Nimeombwa niulize hivi polisi hawakujua suala hili? Kama Lema alikosea sana wakati akiwa Chuo cha Uhasibu kwanini Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) na makachero wote hawakumkamata pale pale? Alifanya kosa hilo baada ya kuondoka?

Kama alifanya vile kwanini aliachwa ili aende na kuja kutafutwa baadaye? Maneno ya Lema yalionekana kuwa kosa baadaye wakati wanafunzi wametawanyika na mbunge huyo akaenda zake?

Hakuna uwezekano wowote kukubali kuwa jeshi letu halitumiki vibaya. Kila tendo lina gharama zake, hili la kumkamata Lema limegharimu heshima ya Jeshi la Polisi. Huo ndio ujumbe niliotumwa niwaambie. Si maneno yangu, mtapima kama mpo tayari kubadilika au la.
 
Mkuu you made my day. Ungekuwa karibu ningekupa mkono umeongea facts tupu. Ningependa zemacopolo aige kutoka kwako logical thinking na jinsi ya kupresent hoja. Hapa ndo Naelew problem cannot be solved my the same level of thinking that created them
 
Well said mkuu.
Yapo mapungufu mengi tu lkn ni nani alie tayari kurudi nyuma na kusahihisha makosa, simuoni.
 
Sio mimi niliyeandika haya. Habari hii nimeitoa Tanzania Daima ili wote tuweze kuisoma.

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
Hawa polisisisiem siyo hawajui sheria hapana ni wanatekeleza amri tu ya kiapo ila hata wao wanalijua hili!
 
Mkuu Dingswayo nchi yetu haina jeshi la polisi bali kuna jeshi la Magamba ndiyo maana madudu ndani ya jeshi hilo ili kuhakikisha CCM inatawala milele yanaongezeka kila siku iendayo kwa Mungu.
 
Last edited by a moderator:
Tanzania hakuna jeshi la polisi kuna ccmpolisi na ndo maana wanafanya kazi wanazotumwa na ccm mafisadi na si wananchi.
 
Kilichofanyika Arusha mtu yeyote mwenye akili timamu anajua ni ulevi na umbumbumbu wa madaraka. Ni utumiaji mbovu wa hela za walipa kodi.
 
Wakae wakijua CCM haitaweza kutawala MILELE ni keshokutwa tu hapo watu wanakomboa TANZANIA yako kwa HIARI au LAZIMA...maana hakuna aliye tayari kuona wanaendeleza tabia ya kuongoza pasi na kuchaguliwa a.k.a KUCHAKACHUA.
 
Jamani ccm ndo ivyo tena wapiga kura wameamua kuwakataa kwa upuuzi huu uliofanywa na mkuu wa mkoa wa arusha kupitia polisi.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hivi kwa taratibu za majeshi aamri ikitolewa, hakuna uwezekano wa kumshauri aliyetoa amri hiyo, kama ndivyo tunahitaji viongozi wenye hekima na busara na wanaojua maadili na mio ya kazi otherwise ipo siku askari ataamlshwa na yeye kwa kwenda kama robot kitafanyika kituko cha ajabu!
 
kumbuka mbowe alivyobebwa na dege la kivita kupelekwa arusha.nchi hii haishi shows za ajabu na kweli.
 
swali la kujiuliza ni, hivi hii kauli mbiu ya utii wa sheria bila shuruti inawahusu raia pekee? kwa nini hili lisingeanzia ndani ya jeshi la polisi kwanza..wakazitii sheria na taratibu zinazowaongoza kutimiza majukumu yao kwanza ndipo warudi kwa raia? to some extent wangeweza kufanikiwa,kinachofanyika ndani ya hili jeshi leo ni kama wametoka kwenye ethics za utaalamu wao na kulifanya kuwa la kienyeji,linatimiza majukumu yake kwa influence zaidi, leo hii polisi wamekuwa ndo vinara wa kukiuka sheri na taratibu za nchi na walizojiwekea pia kama jeshi ili kutimiza majukumu yao..hii nchi inahitaji viongozi na sio watawala ili haya yote yaishe vinginevyo tuendelee kuvumilia tu kama taifa
 
Arusha mnataka nchi yenu chini ya Lema? Uchochezi ni maneno au vitendo vinavyosababisha hasira. Nchi haitawalika iwapo yeyote ataamua kwenda kwa watu wenye matatizo bila suluhisho isipokuwa kuongeza maumivu yao. Lema afanye kazi Serikali,
 
Naamini ARUSHA italeta mafanikio makubwa tz na dunia nzima ucjarib kumdangany mtu yeyote atokae jj hli utaumia...we mtu c mzaliwa wa hapa unapewa ukuu wa mkoa c unapelekwapelekwa na mwajr wako...jk jifunze.PEOPLE'S
 
hiii ndio tanzania sheria kwenye makaratasi tu utekelezaji hamna,
Ila mm siwalaumu wale askari kwasababu wale wote nimaboss wao jamaaa anamkopo banki akifikria mtoto anadaiwa ada hawezi kugoma kuendeshwa kama robot minaomba tu polisi wote tanzania wagome siku moja kutokana nakulazimishwa kufanya mambo yasiyo na tija zaidi ya kuumiza na kutesa raia
:teeth::teeth:
 
Back
Top Bottom