Polisi walioua kasulu waachiwa huru

Polisi walioua kasulu waachiwa huru

mwandiga

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2011
Posts
1,506
Reaction score
664
Hii sijui imekaaje, ni sheria zetu mbovu au kuna jingine zaidi. Wale polisi waliokuwa wamefungwa kwa kosa la kuua mwanakijiji wa Jimbo la kasulu vijijini wameachiliwa huru huku wakiwa wamekaa gerezani miaka 2 tu. Hii ni sawa? Wenye uelewa wa sheria naomba mawazo yenu, kwani wote 7 wameachiliwa huru.
Cc mbunge kasulu vijijini Ujue hilo maana wewe ndie uliyekuwa mtetezi mkubwa wa hili ukitaka haki itendeke.
 
Waliomuuwa mwangosi wako wapi?

Hii ndio serekali yako kijana ukiuwa unapandishwa cheo
 
Kesi ya mauaji ni serious case na hukumu yake ni kifo,hivyo kisheria unatakiwa ushaidi usio na shaka lolote.Wanasema wanasheria kuwa ni bora kuachia watu 100 waliotenda kosa kuliko kumtia hatiani mtu 1 ambaye hakutenda kosa.Kuthibitisha murder case inataka ushaid wa kutosha sana,kuhusu kukaa miaka miwili magereza mimi kwa maoni yangu walicheheweshwa sana na upelelezi,ilitakiwa hata within 4 month upelelezi uwe umekamilika na jalada liko mezani kwa mwanasheria.Pia kwa taarifa yako hakuna duration inayotakiwa kwa mtuhumiwa wa mauaji kukaa gerezani,hata ingekuwa wiki ni sawa,mbona Lulu alikaa chini ya mwaka hamkusema?mbona alipewa dhamana murder case hamkusema,mbona na mrehemu Ditopile alipewa dhamana Murder case hamkusema.Kumbuka usimtakie mwenzako akae mahabusu muda unaoutaka wewe kwani JUSTICE DELAYED IS JUSTICE DENIED.Pia uaipende kumuhukumu mwenzako kuwa ana hatia achia waliosomea hiyo kazi wafanye maamuzi.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Lulu we ndo ulimshtaki kwa murder au unongea tu? ninachoelewa kashtakiwa kwa manslaughter ambayo ni bailable
 
Lulu we ndo ulimshtaki kwa murder au unongea tu? ninachoelewa kashtakiwa kwa manslaughter ambayo ni bailable

Nawewe ndiye uliyewafungulia kesi hao askari au unaongea tu?
Kama hujaridhishwa na maamuzi/hukumu kama ilitolewa nenda mahakamania au ukakate rufaa.
 
Lulu we ndo ulimshtaki kwa murder au unongea tu? ninachoelewa kashtakiwa kwa manslaughter ambayo ni bailable
Wewe ndiye unayeongea tu ka TABULA LAZA,Lulu alishtakiwa kwa murder ambayo baadae ilikuwa reduced to manslaughter
 
Sijajua unachoongea,unasema alishtakiwa kwa murder then ikawa REDUCED to manslaghter" unachokiongea unakijua kweli? ilo neno ulotumia dhahiri inaonesha huna uelewa wowote wa sheria.
 
Back
Top Bottom