Polisi wahaha wizi wa mil. 150/-

Polisi wahaha wizi wa mil. 150/-

Jangakuu

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2012
Posts
513
Reaction score
221
TUHUMA ya askari polisi kukimbia na fuko la fedha zinazokisiwa kufikia sh milioni 150 zilizoibiwa na majambazi eneo la Kariakoo mapema wiki hii, limechukua sura mpya baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuwataka askari wanaodaiwa kuzipora kuzisalimisha ndani ya siku saba.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Seleman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa amelazimika kuunda jopo maalumu la kuchunguza kutoweka kwa fedha hizo ambazo ziliporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston, jijini Dar es Salaam, juzi.
Kova alisema jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli upatikana ili wananchi wajulishwe matokeo.
Kauli hiyo imekuja siku moja tu baada ya kamanda huyo kukanusha vikali tuhuma za kuhusika kwa askari waliopambana na majambazi hao, kukwapua mfuko unaodaiwa kuwa na kiasi hicho cha fedha.
Katika maelezo ya juzi, Kova alisema wakati askari wanamkamata jambazi huyo, kwa bahati mbaya hakuwa na mfuko wowote wa fedha kama inavyodaiwa.
Lakini kauli yake ilipingwa vikali na mashuhuda wa tukio hilo ambao walisema polisi walipofika katika eneo hilo kukabiliana na majambazi hao, jambazi aliyekuwa na mfuko huo aliuangusha chini kwa lengo la kijisalimisha.
Mashuhuda hao walisema baada ya kuangushwa, walimuona askari mmoja akiuokota na kuingia nao ndani ya gari ambalo hawakuweza kulitambua namba zake na kisha kuondoka kwa kasi katika eneo hilo.
“Zile fedha zimeondoka na askari mmoja kibongekibonge hivi, sasa tunashangaa kusikia kuwa hazijapatikana sisi tulikuwa karibu pale Columbia ambapo ndipo zilipochukuliwa,” alisikika mmoja wa mashuda hao.
Hata hivyo, jana Kamanda Kova alisema jeshi hilo limeamua kufanya uchunguzi makini na wa kina na kwamba lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake.
Alisema tukio hilo halikubaliki, hivyo kila askari aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni lazima ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane haraka kuondoa shaka kwa wanachi.
Kova alimtahadharisha Kamanda Msangi kuwa endapo atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi atambue itabidi awajibike, kwa madai kuwa jeshi hilo litapata sifa mbaya na kupoteza imani kwa wananchi.
“Pamoja na kumkabidhi kazi hiyo Msangi, mimi sitakaa kimya bali nitalifuatilia kwa karibu ili mradi tuwapatie wananchi ukweli, ” alisema Kova.
Alibainisha kuwa hawezi kupinga kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo viovu, bali suala hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo ni vema wananchi wenye ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana fedha hizo.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe bila kushirikisha wadau wengine kwa madai kuwa eti litatii sheria zote bila kwenda kinyume.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Polisi wahaha wizi wa mil. 150/-


na Shehe Semtawa na Flora Laanyuni


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
source : Tanzania daima
 
Hawana haja ya kuhaha bali kuzirejesha hizo milioni. Wamejitia aibu. Maana kwa sasa sitofautishi kati ya majambazi na polisi wa Bongo. Huenda walikuwa wakiiba kwa siri sasa wameamua kufanya kweli hadharani. Kweli unaweza kuficha ugonjwa lakini si tabia. Hao ndiyo polisi wetu wanaolinda chama cha mafisadi wakati nao ni majambazi! Bado hawajaanza kurusha risasi na kuwamwangosi watu wasio hatia. Je hapa tuna polisi au hasara?
 
Aibu bongo Father of All? Amiri jeshi wao tu hana aibu. Polisi ndo wezi namba moja na wanawajua karibu wezi wote wa mjini. Hiyo tume itawapunguzia mgao waliozioetea tu. Mazingaombwe yanaendelea, utii wa sheria bila shuruti.
 
Last edited by a moderator:
Umesahau kuwa Mwema ni alawa na ameoleana na ****** mr Dhaifu? Bongo hatuna polisi bali mibaka na mijambazi ya kawaida iliyovaa magwanda. Nilifurahi ilipouawa kule Ngara so to speak.
Aibu bongo Father of All? Amiri jeshi wao tu hana aibu. Polisi ndo wezi namba moja na wanawajua karibu wezi wote wa mjini. Hiyo tume itawapunguzia mgao waliozioetea tu. Mazingaombwe yanaendelea, utii wa sheria bila shuruti.
 
Ni kweli wa mekwiba hao polisi. Maana hawa jamaa hata mia tano wana iba.
 
Na hii njaa ya town hapo sijui kama zitarudi..na hata kama zikirudi watadai kiasi kingine ni kile majambazi walichomwaga wakati wanakimbizwa!
 
Sasa alichokimbilia kukanusha ni nini kama alijua wananchi wanahitaji majibu sahihi, huku kukurupuka kwa polisi kutaisha lini? hata hivyo sitegemei majibu tofauti na aliyotoa awali!
 
Hizo tayari zimesha ingia kwenye mzunguko na wengine tayari wamesha ongeza mpaka wake unacheza na sikukuu hii na pesa ilivyo ngumu
 
Safi sana POLISI,ikitokea pesa hizo zikarudishwa ntawashangaa sana askari waliochukua,hiyo ni fursa nzuri ya kumfikishia ujumbe Rais wenu kuwa mshahara haukidhi mahitaji ya watumishi wake,Endeleeni kukomaa mpaka mwisho wa Game,na mkijidanganya kurudisha mtambue pia kuwa hamna kazi tena,msiogope na vitisho vya KOVA,alishalewa na pesa za kuzuia maandamano huyo.
 
TUHUMA ya askari polisi kukimbia na fuko la fedha zinazokisiwa kufikia sh milioni 150 zilizoibiwa na majambazi eneo la Kariakoo mapema wiki hii, limechukua sura mpya baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuwataka askari wanaodaiwa kuzipora kuzisalimisha ndani ya siku saba.
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Seleman Kova, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa amelazimika kuunda jopo maalumu la kuchunguza kutoweka kwa fedha hizo ambazo ziliporwa na majambazi Mtaa wa Mahiwa na Livingston, jijini Dar es Salaam, juzi.
Kova alisema jopo hilo litaundwa na watu watano, likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu, Ahmed Msangi, atakayehakikisha kwamba muda mfupi inavyowezekana, ukweli upatikana ili wananchi wajulishwe matokeo.
Kauli hiyo imekuja siku moja tu baada ya kamanda huyo kukanusha vikali tuhuma za kuhusika kwa askari waliopambana na majambazi hao, kukwapua mfuko unaodaiwa kuwa na kiasi hicho cha fedha.
Katika maelezo ya juzi, Kova alisema wakati askari wanamkamata jambazi huyo, kwa bahati mbaya hakuwa na mfuko wowote wa fedha kama inavyodaiwa.
Lakini kauli yake ilipingwa vikali na mashuhuda wa tukio hilo ambao walisema polisi walipofika katika eneo hilo kukabiliana na majambazi hao, jambazi aliyekuwa na mfuko huo aliuangusha chini kwa lengo la kijisalimisha.
Mashuhuda hao walisema baada ya kuangushwa, walimuona askari mmoja akiuokota na kuingia nao ndani ya gari ambalo hawakuweza kulitambua namba zake na kisha kuondoka kwa kasi katika eneo hilo.
"Zile fedha zimeondoka na askari mmoja kibongekibonge hivi, sasa tunashangaa kusikia kuwa hazijapatikana sisi tulikuwa karibu pale Columbia ambapo ndipo zilipochukuliwa," alisikika mmoja wa mashuda hao.
Hata hivyo, jana Kamanda Kova alisema jeshi hilo limeamua kufanya uchunguzi makini na wa kina na kwamba lina mfumo wake wa kuchunguza askari wake inapotokea amejihusisha katika matukio yanayokwenda kinyume na maadili ya kazi yake.
Alisema tukio hilo halikubaliki, hivyo kila askari aliyepewa jukumu la kulifuatilia ni lazima ahakikishe kuwa anafanya kazi kwa ufasaha ili majibu yapatikane haraka kuondoa shaka kwa wanachi.
Kova alimtahadharisha Kamanda Msangi kuwa endapo atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha basi atambue itabidi awajibike, kwa madai kuwa jeshi hilo litapata sifa mbaya na kupoteza imani kwa wananchi.
"Pamoja na kumkabidhi kazi hiyo Msangi, mimi sitakaa kimya bali nitalifuatilia kwa karibu ili mradi tuwapatie wananchi ukweli, " alisema Kova.
Alibainisha kuwa hawezi kupinga kama askari wanaweza kushiriki katika vitendo hivyo viovu, bali suala hilo bado linahitaji ushahidi zaidi hivyo ni vema wananchi wenye ushahidi wakatoa ushirikiano utakaosaidia kupatikana fedha hizo.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza jopo hilo linaundwa na polisi wenyewe bila kushirikisha wadau wengine kwa madai kuwa eti litatii sheria zote bila kwenda kinyume.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Polisi wahaha wizi wa mil. 150/-


na Shehe Semtawa na Flora Laanyuni

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
source : Tanzania daima
MWISHO WA UCHUNGUZI KUTAKUWA NA FINDINGS ZIFUATAZO,
1.Majambazi walikuwa zaid ya wanne,
2.Inaonekana jambazi aliyekuwa na mfuko wa mil 150 aliondoka eneo la tukio kabla ya polisi kufika.
3.Polisi hawahusiki na upotevu wa pesa kwa namna yoyote

NB: JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA UCHUNGUZI WA KINA

CHEZEA TANZANIA WEWE!
 
Good idea, lakini japo zipite siku ishirini ili wananchi wasahau halafu ndo waje na hiyo ripoti:
 
mwisho wa uchunguzi kutakuwa na findings zifuatazo,
1.majambazi walikuwa zaid ya wanne,
2.inaonekana jambazi aliyekuwa na mfuko wa mil 150 aliondoka eneo la tukio kabla ya polisi kufika.
3.polisi hawahusiki na upotevu wa pesa kwa namna yoyote

nb: Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa kina

chezea tanzania wewe!

hizo pesa zilipigwa na kitu kizito kisichojulika kimetoka wapi
 
Back
Top Bottom