Jeshi la polisi mkoani Kigoma,linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mkazi mmoja wa kijiji cha Herushingo,tarafa ya Makere,wilaya ya Kasulu. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kamanda wa polisi mkoani humo,Fraisser Kashai,alisema tukio hilo lilitokea Decemba 25,mwaka huu,saa nne usiku katika kijiji hicho.
Aliwataja askari hao kuwa ni D.8622 CPL,Peter na G.1236 PC Sunday wa kituo kidogo cha Rerushingo ambapo wanadaiwa kumshambulia Bw.Gasper Mussa (36),ambaye ni mkulima katika baa waliyokuwa wanakunywa na baada ya kumpiga,walimfikisha kituoni hapo. Alisema Decemba 26 mwaka huu,mkuu wa kituo hicho alitoa taarifa kituo cha polisi kwa SP Sospeter kunguru kuwa mtuhumiwa alikuwa mgonjwa lakini alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kasulu.
"Chanzo cha ugomvi ni baada ya marehemu kushindwa kulipa vinywaji alivyokunywa ndipo askari walipoanza kumshambulia na kumsababishia maumivu yaliyosababisha kifo chake," Alisema kutokana na tukio hilo,askali hao wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo hasa cha ugomvi huo na kama itabainika walihusika moja kwa moja watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.
Chanzo cha Habari:Gazeti la Majira la Desemba 28,2012,habari hii inapatikana ukurasa wa 3.
My Take Kadri siku zinavyozidi kwenda, mmomonyoko wa maadili kwa askari wetu unazidi kukuwa.Askari wetu wamejenga tabia ya kuchukua sheria mkononi (Instant justice).Hii pia imezoeleka hata kwa sisi raia,utasikia mtu anakwambia "unauliza makofi polisi" yaani anamaanisha askari ana haki na kuchukua sheria mikononi pale anapojisikia kufanya hivyo.Tabia hii ni mbaya na inaenda kinyume na kaki za binadamu.Kuna haja ya kufanya uchunguzi yakinifu, ili kujua kama askari wetu huwa wanafundishwa nini kwenye vyuo vya polisi,inawezekana huwa kuna mafunzo maalumu wanaopewa ambayo yanakinzana na haki za binadamu.