Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Kundi la Polisi Mkoani Kilimanjaro linadaiwa kumpiga mkazi wa Motamburu, Wilayani Rombo hadi kumjeruhi na kumsababishia kifo chake.
Taarifa zimesema kuwa, Aprili 8, polisi hao wakiwa katika operesheni maalumu, walimkuta mwananchi huyo anayejulikana kwa jina la Furajha Mkanza, akinywa pombe kali iliyowekwa katika pakiti za plastiki, maarufu kama viroba, na baadaye kuanza kumpiga hadi kumvunja mguu na kisha kuondoka naye.
Polisi walimbeba na kumwingiza kwenye gari wakazunguka naye wakiendelea na operesheni na baadaye kumuacha Hospitali ya Ngoyoni. “Baada ya kumwacha hapo huyo bwana, aliwekewa POP ‘bandeji ngumu’ na kulazwa hadi Aprili 14 aliporuhusiwa kurudi nyumbani ili aendelee kujiuguza”, alisema mkazi mmoja.
Hata hivyo, Mei 4, akiwa nyumbani hali yake ilibadilika ghafla na baadaye kufariki dunia. Suala hilo liliwafanya ndugu zake wachachamae na kugoma kumzika wakitaka kupeleka maiti yake kituo cha Polisi.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo, alilithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba tayari ameunda kamati ya uchunguzi ili kubaini nini kilitokea siku alipokamatwa na Polisi.
Chanzo: Kwanza Tv