PreGE2025 Polisi: 'Wachokonozi' Jackson na Joseph wamekamatwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mtandao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
221
Reaction score
659
Tutafika Oktoba tukiwa tumechoka sana!

====

WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa inayosambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza juu ya watu wawili kukamatwa na watu wasiojulikana huko katika maeneo ya Maji ya Chai, wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Akitoa ufafanuzi kuhusiania na tukio hilo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi Juni 20 mwaka huu na kuwataja kuwa ni Jackson Kabalo (32) na Joseph Mrindoko (37) wote wakiwa ni wajasiriamali, wakazi wa Maji ya Chai wilayani Arumeru kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao.

Soma Pia: Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

Kamanda Masejo amebainisha kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea na pindi utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitafuata.

Jeshi la Polisi Mkoani humo limetoa onyo kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika jamii hasa zile za kuzusha kuwa watuhumiwa wamekamatwa na watu wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli.

Pia soma: Polisi Arusha: Ni kweli tunawashikilia Wachokonozi kwa makosa mbalimbali

1750540635265.png
 
Jeshi la Polisi Mkoani humo limetoa onyo kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika jamii hasa zile za kuzusha kuwa watuhumiwa wamekamatwa na watu wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli
Sasa kama ndugu na jamaa tukae kimya masaa zaidi 24 kuwasubiri nyinyi?!
 
Mtoto anakuelewa Chief PM Nini Sanaa tuu.
Enjoy laifu mwanawane.
Usizile ingoma tvala simakurubhas ukisakala Makuma.
Chakula kikiletwa mm nakula tuu, kwan dyudyu nimepewa la nn kama sio kusokomeza nyama ndani huko 😂
 
Tutafika Oktoba tukiwa tumechoka sana!

====

WAWILI WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO.

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa inayosambaa kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza juu ya watu wawili kukamatwa na watu wasiojulikana huko katika maeneo ya Maji ya Chai, wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.

Akitoa ufafanuzi kuhusiania na tukio hilo leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi Juni 20 mwaka huu na kuwataja kuwa ni Jackson Kabalo (32) na Joseph Mrindoko (37) wote wakiwa ni wajasiriamali, wakazi wa Maji ya Chai wilayani Arumeru kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mitandao.

Soma Pia: Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

Kamanda Masejo amebainisha kuwa upelelezi wa tukio hilo unaendelea na pindi utakapokamilika hatua zaidi za kisheria zitafuata.

Jeshi la Polisi Mkoani humo limetoa onyo kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika jamii hasa zile za kuzusha kuwa watuhumiwa wamekamatwa na watu wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli.

Pia soma: Polisi Arusha: Ni kweli tunawashikilia Wachokonozi kwa makosa mbalimbali

Polisi hkuna cha taharuki, bali sema hamtaki anya posts ambazo zinamkosoa samia. had it not been for the compromised judiciary, hakuna kesi mgelishinda!
 
Lengo lilikuwa kuwakamata au kuwateka?

Kwanini walichukuliwa kwa style ile kama kweli lengo lilikuwa kuwakamata?

Kelele safari hii zimesaidia.
Wewe ndie umesema nilichowaza ukiangalia namna walivyochukuliwa haikua ukamataji , haya mtu anaenda kukamatwa na kupekuliwa bila viongozi wa mtaa wala warranty ya mahakama?
Walipoona makelele yamezidi ndio ghafla wakabadili gia angani 😮‍💨😮‍💨😮‍💨
 
Mtawakamata mpaka mtashindwa. Watu wakiamua kupaza sauti zao, ni kazi sana kuwadhibiti wote.
 
Daa! huyu Jackson Kabaro ni kama ninamfamu.
Nadhani kama atafanyiwa vitimbwi vilivyo zoeleka kwa wakamatwaji(watekwaji) ambavyo sio vya kiutu, rasmi nitapata allergy ya kudumu na wenye kufurahishwa na kuratibu matukio ya poteapotea.
 
Hii sheria ya mitandao hii kuna haja ya sisi maraia kuipitia kwa kweli maana tofauti na hapo tutakuwa tunakamatwa tuu kama kuku kila siku.
 
Back
Top Bottom