Tanzania Mpya
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 253
- 144
Siwaelewi hawa polisi wanapoingia ktkt ya barabara na kuanza kuongoza magari wakati taa nazo bado zinawaka. Kuna siku nilikuja speed nawahi taa za kijani lkn nilipokaribia kuvuka ndipo nikamuona polisi yupo pale anaita magari ya upande mwingine. Kuna dada alimgonga polisi alipoingia ktk junction kwa kuruhusiwa na taa bila kujua kwamba pale ktk kulikuwa na polisi anaongoza magari!
Hivi hakuna namna ya wao kuzizima hizi taa kabla ya kuingia na kuongoza kwa mkono? Hii ni hatari sana, ni kutaka kuingizana ktk matatizo. Naomba Polisi waliangalio hilo, tunatuchanganya sana na wao pia wanajiweka hatarini. Kama taa zinawaka, waache tufuate taa, na kama wanataka kuongoza kwa mkono watafute namna ya kuzizima kwanza.