Polisi traffic Tabora bado wanaomba rushwa

KIPUMPUSWA

Senior Member
Jul 16, 2011
106
35
Pamoja na bajeti ya kambi rasmi ya upinzani bungeni ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi kulitaja jeshi la polisi kuwa ndio taasisi inayoongoza kwa kuomba na kupokea rushwa na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara hiyo, jana majira ya saa kumi na mbili jioni maeneo ya hospitali ya mkoa kitete nilisimamishwa na askari wa usalama barabarani .Chombo changu cha usafiri hakikukaguliwa wala sikuombwa leseni ila nikaombwa mchango wa kukaa viti virefu jioni. kwa hali hii vita dhidi ya rushwa safari bado ni ndefu.
 
unaposema polisi wa tabora BADO wanaomba rushwa,unamaanisha wa mikoa mingine hawaombi? pole kwa kukamuliwa mchango wa bia, ungewaambia ww mdogo wake kakobe
 
Nilichokiandika humu ndio kuripoti kwenyewe. usiwe na mawazo finyu sio lazima kila hoja kupelekwa ofc husika.
 
Waache wale rushwa bana tz is free corruption zone hao kina chenge, rostam, lowasa, kalamagi, sitta, jk na mafisadi wote wanakula na kupiga michongo daily hakuna hatua sembuse trafic? Jairo
pole mkuu nawewe utapata tu hata mh. Wenje anafahamu hivyo
 
Nxt time mwambie kama ni bia aje anywe nyumbani kwako huku mnapiga stori
 
Back
Top Bottom