MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
Polisi Tanga Wavunja Shughuli Ya Harusi!
29 June 2009 90
Tukio lisililo la kawaida limeripotiwa leo kupitia TBC 1 kwamba polisi mkoani Tanga wameingilia kati na kuvunja shughuli ya harusi kwenye moja ya vijiji vya mkoa huo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, polisi wameingilia kati kwa vile ndoa hiyo ilihusu msichana wa miaka 17 na aliyekatishwa masomo yake kuolewa na bwana wa umri wa miaka 50.
Polisi waliingia mahali hapo wakati Bi. Harusi, ndugu na wengine walioudhuria walipokuwa wakimsubiri Bwana harusi afike na baadae Shehe wa kufungisha ndoa. Naam. Harusi ikawa imevunjika na vijana wa eneo hilo wanaripotiwa kusikitikia zaidi kuikosa pilau iliyokuwa ikiandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo!
Imetoka KwanzaJamii