GE2025 Polisi Tanga waahidi kuwalinda waandishi wa habari wakati wa uchaguzi

GE2025 Polisi Tanga waahidi kuwalinda waandishi wa habari wakati wa uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Jeshi la Polisi Mkoani Tanga limesema litaendelea kushirikiana na waandishi wa habari,ikiwemo kuangalia usalama wao wanapokuwa kazini hasa kwa muda huu wa uchaguzi.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi kwenye mdahalo wa ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari wa mkoa huo ulioandaliwa na Klabu ya waandishi wa habari Tanga kuelekea uchaguzi mkuu, na kusema kuwa waandishi wanachotakiwa ni kuzingatia kanuni na taratibu za kazi.

Amesema jeshi la polisi linatambua na kuheshimu kazi za waandishi wa habari,hivyo limejipanga kuhakikisha waandishi wanatekeleza majukumu yao katika hali ya usalama hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga,(TPC) Lulu George amesema wataendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari,ili kuweza kufanyakazi zao kwa weledi,hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa kushirikiana na wadau wengine.

Aidha Afisa Program msaidizi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Edmund Kipungu amesema bado ipo changamoto ya waandishi wa habari,kutishwa na kunyimwa kutoa habari hivyo kuomba mamlaka zote kutoka ushirikiano wa kuwa na mahusiano mazuri na waandishi ili kufanyakazi zao bila bughuza.

Baadhi ya washiriki nao walipongeza mdahalo huo kwa kuwapa uelewa wa mambo mbalimbali,huku wakitoa mapendekezo ya kupewa elimu ya mara kwa mara kuhusu mambo ya waandishi kama ilivyofanyika


 
Inategemeana na habari anazoziandika mwandishi, kama anaandika habari zisizo za kichawa na zenye kuidisi serikali atashughulikiwa tu hata kama habari hizo zina ukweli, hatalindwa
 
Back
Top Bottom