Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,606
Jeshi la Polisi limemwelekeza aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole afike katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) atoe maelezo na ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii. Jeshi hilo limesema mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo na vielelezo vitakavyothibitisha tuhuma hizo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
Soma majibu ya Polepole kwa Polisi: Polepole: Jeshi la Polisi hamjafanya juhudi zozote za kunitafuta| Mawasiliano yangu rasmi yanajulikana
===
Leo Septemba 15, 2025 Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa lilifungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma mbalimbali ambazo amekuwa akitoa Humphrey Herson Polepole toka Julai 2025.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Jeshi limesema Polepole amekuwa akitoa tuhuma hizo Tuhuma hizo kupitia mitandao ya Kijamii. Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa maelezo/ushahidi na vilelezo vitakavyo thibitisha tuhuma hizo ili kuwezesha hatua zingine za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na ndivyo utaratibu wa kisheria ulivyo.