Polisi na maji ya uchungu: Kipya Kinyemi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi na maji ya uchungu: Kipya Kinyemi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 9, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yaani kero juu ya kero! Sijamalizana na TANESCO kwa jinsi wanavyotufanya mabahau kulipia gharama walizofisadi wao na wakubwa zao huko Serikalini bila kutushirikisha, huku wakitulaza gizani na jotoni. Hivi mtu mwenye akili timamu anaweza kupandisha bei ya bidhaa asiyoweza kuizalisha? Akh! Acha ninyamaze wasije wakapata sababu, lakini bado ninao hadi kieleweke.

  Wakati nilipokuwa nikijiandaa kuendelea kuwagea vidonge vyao, napata mshtuko kuona yaliyotokea kule Arusha. “Polisi wameutawanya mkutano na maandamano ya wana-CHADEMA kwa maji ya uchungu, mabomu ya machozi na risasi za moto”! Mimi nadhani haya mabomu pia yalikuwa ni ya moto kwani kwa ufahamu wangu mabomu ya machozi hayana uwezo wa kuzua milipuko ya kiasi kile na kukata miguu ya watu. Sijui…

  Niliwahi kuzungumza na Polisi hapa kabla ya Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba, 2010. Nilikuwa na wasiwasi na kauli zao za “kuwa fiti kupambana na vurugu za uchaguzi”. Nikawauliza iwapo wanaye kakakuona aliyewatabiria vurugu wakati huo, lakini sikupata jibu.

  Nikasema iwapo uchaguzi utafanyika kwa haki, hakuna kitakachofanya raia waanzishe vurugu. Pia nikawaasa wao wafuatilie kwa umakini namna hesabu za kura zitakavyofanyika na matokeo yake kutangazwa kwa wakati muafaka badala ya kufanya mazoezi ya urushaji wa mabomu. Kilichotokea kilinisikitisha; matokeo yalicheleweshwa katika baadhi ya majimbo na kufanya wafuasi wa baadhi ya vyama kuhisi uchakachuliwaji, na walipoyadai wakajibiwa na mabomu!

  Niliwauliza walinzi wetu hao iwapo wanazingatia mafunzo yao kule Moshi, na nikawakumbusha kuwa kuna “Minimum Force,” “Medium Force” na “Maximum Force” (nguvu ndogo, ya kati nay a juu) katika kuzuia uhalifu na kulinda amani. Huwezi ukaenda kumchukua mtuhumiwa aliyetoa lugha chafu kwa jirani yake ukiwa na lori zima la FFU. Unatakiwa kumfuata ukiwa na kirungu tu na kumtaarifu kuwa anahitajika kituoni kukabiliana na tuhuma zake.

  Akigoma, wewe kama Polisi mwenye mafunzo unatumia Minimum Force kumpeleka. Akitoa panga tumia Medium Force ikiwemo kutoa taarifa Kituoni na kuongezewa Askari. Na iwapo nao wataongezeka wakiwa na silaha za moto basi tumieni Maximum Force. Hilo halina tatizo.

  Wakati wa sherehe za kuuaga Mwaka 2010 na kuukaribisha 2011 mimi nilikuwa katika maeneo ya Tandika. Hali ilikuwa shwari kabisa. Kiasi cha saa 4 za usiku nilishuhudia lori la FFU likitanguliwa na difenda zao lilirandaranda huku na kule.

  Nikajisemea: “Hawa wanasubiri mtu atoke na kigoma chake, wamlipue,” na kweli mida ya saa 6 walifika mitaa ya Mtoni Madafu na kurusha mabomu kutawanya washerehekeaji. Mbaya zaidi waliyarusha mabomu hayo kwenye makazi ya watu ambapo vijana walikimbia lakini watu wazima na watoto wadogo walibubujikwa na machozi na kukohoa hadi kunakucha.

  Sasa kabla hatujakaa na kutafakari tunasikia hili la Arusha. Mimi sidhani kama kulikuwa na sababu ya kuvurumisha kiyama kile kwa watu wasio na silaha yoyote. Kwanza ifahamike kuwa maandamano si jinai, ni njia ya watu wasio na pa kusemea kutoa hisia na mawazo yao kuyafikisha kunakohusika.

  Tumeandamana mara ngapi tangu enzi za kudai Uhuru, kumpokea na kumpongeza Mwalimu hadi Azimio la Arusha bila kupigwa mabomu? Au inadhaniwa kuwa Serikali za Kikoloni ziliyafurahia maandamano yetu?
  Naomba ieleweke kuwa mwanzo wa ngoma ni lele. Haya matukio tunayoyaona kuwa ni madogo yanaonekana ulimwenguni kote, na lazima tutambue kuwa tunao marafiki na maadui pia ulimwenguni. Sasa maadui zetu wakiweza kuwafikia watu wasio na ajira (ambao ni wengi zaidi nchini) watawasaidia silaha za kivita na kuwapa kibarua cha kuandamana kudai hiki na kupinga kile, kisha Polisi muwachokoze na SMG zenu mje mkutane na A.K. 47 za kivita.

  Siombei kabisa hilo litokee, lakini naendelea kuwa na wasiwasi na matumizi ya mbavu za walinzi wetu wa amani. Hivi karibuni mara baada ya IGP mpya kutawazwa, alikuja na sera nzuri sana ya Polisi Jamii na Polisi Shirikishi. Namshauri apitie tena makabrasha yake aone taarifa za matukio yaliyojitokeza tangu amesimikwa hapo na jinsi yalivyozimwa.

  Au yawezekana ni kosa la baba kumpatia mwanae zawadi ya bunduki ya kisasa. Mtoto huyu atahangaika kuisafisha kila siku na kulala nayo kama mkewe kitandani lakini ataona haitoshi.

  Atamtafuta kunguru anayekwiba watoto wa kuku ili amlipue, na akimkosa atamlipua mtoto mwenzie aliyemdhulumu goroli zake. Ni kweli hapo zamani hatukuyajua mabomu ya machozi ya kufyatuliwa na makombora, bali tulikuwa na yale ya kutupwa kwa mkono.

  Pia hatukuwa na magari ya maji ya uchungu. Sasa vitu hivi vimeletwa kwa wakati mmoja na hawa mabwana yaonyesha wana hamu ya matumizi yake pengine kuvinusuru visije kulipuka vyenyewe kama mabomu ya Mbagara!
  Salamu zangu kwako IGP ni kuangalia tena utendaji wa Jeshi lako.

  Mtu asiye makini anaweza kudhani kuwa mna kampeni ya kuishinikiza Serikali yetu tukufu ijiuzulu. Ukumbuke kuwa mdogo anapoharibu na mkubwa akachelewa kumzuia basi mkubwa huomba maji na kunawa mikono yake akisema “Naliepuka janga hili”.
  0713-248943/0682-078000
  nnundumag@gmail.com
   
 2. Darlingtone

  Darlingtone JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni Maji ya Uchungu au maji ya kuwasha?
  Maana nijuavyo mimi Maji ya uchungu ni yale wanawekewa akina mama wakati wa kujifungua
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nikweli maji ya uchungu ni medical ila nafikiri alimaanisha maji ya kuwasha
   
Loading...