Polisi mtaacha lini Rushwa?

Mzee Chapuuka

Member
Apr 21, 2017
97
243
Salaam wanaJF,

Leo mida ya asubuhi nimekuwepo central kufuatilia namna ya kumdhamini mfanyakazi mwenzangu aliekamatwa Kwa kesi ya madai.

Sasa nimepeleka barua ya kumdhamini toka Kwa Afisa mtendaji.

Kilichofuata hapo nikaanza kuzungushwa ili mradi nitoe fedha jamaa angu aachiwe wakati dhamana ni bure na nlitimiza vigezo vya kisheria.

Jamaa wakanizungusha na kudai niwape angalau elfu 50 ili jamaa yangu wamuachie
Kiukweli nliwakomalia Sana hadi mwisho wa Siku wakamuachia.

Kimsingi rushwa nchi hii haiwezi kuisha hasa Kwa hawa wenzetu wanaolinda usalama wa raia na Mali zao waache kuomba omba rushwa wakati salary wanapokea
Nlienda central saa 2 asubuhi jamaa anakuja kuachiwa saa 8 mchana.

SAY NO TO CORRUPTION!
 
upo sahihi mtoa mada na hali hii inawafanya raia wengi wasiwe na imani na askari wengi ambao wanalichafua jeshi la polisi na kusababisha hata polisi waaminifu waonekane ni walewale
 
Mi sina hamu nao, nilishawahi kushikiliwa kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 12 jioni kwa kesi ya kusingiziwa tu na mazingira yote yanaonekana sikukosa chochote ila walikuwa wanalazimisha rushwa na walikomaa hadi nilitoa 100,000 ndio waliniachia... Yaani hawa watu Mungu anawaona!
 
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni watuhumiwa. Hivyo kwa huu ushahidi wako inatakiwa ukamatwe na kushitakiwa.
 
Si umeona polisi ni wabaya kwako kuliko aliyekusingizia kesi. Sasa aliyekusingizia akikuona mtaani atatangaza polisi ni wala rushwa tu mtuhumiwa wangu wamemuachia sababu ya rushes tu.
 
Pole mkuu jamaa wana njaa za kipuuzi sana
 
Salaam wanaJF
Leo mida ya asubuhi nimekuwepo central kufuatilia namna ya kumdhamini mfanyakazi mwenzangu aliekamatwa Kwa kesi ya madai
Sasa nimepeleka barua ya kumdhamini toka Kwa Afisa mtendaji
Kilichofuata hapo nikaanza kuzungushwa ili mradi nitoe fedha jamaa angu aachiwe wakati dhamana ni bure na nlitimiza vigezo vya kisheria
Jamaa wakanizungusha na kudai niwape angalau elfu 50 ili jamaa yangu wamuachie
Kiukweli nliwakomalia Sana hadi mwisho wa Siku wakamuachia
Kimsingi rushwa nchi hii haiwezi kuisha hasa Kwa hawa wenzetu wanaolinda usalama wa raia na Mali zao waache kuomba omba rushwa wakati salary wanapokea
Nlienda central saa 2 asubuhi jamaa anakuja kuachiwa saa 8 mchana
SAY NO TO CORRUPTION!
Umewaon polisi tu mbona wengin hamsemi ao takukuru ndo hao hao mbona hamsemi yule mhadibu wao
 
Mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni watuhumiwa. Hivyo kwa huu ushahidi wako inatakiwa ukamatwe na kushitakiwa.

Kuna wakati unaona wanakulazimisha na kutaka kukupotezea muda wako wakati una kazi nyingi za kufanya kulijenga Taifa pia familia inakuangalia basi inabidi uwe mpole tu, kwa sababu mimi mmoja wao zaidi ya 2

Na pia muda wote utakaopotea kudai haki naumia mwenyewe kwa gharama nyingi.. nikaona niwape tu yaishe!
 
Si umeona polisi ni wabaya kwako kuliko aliyekusingizia kesi. Sasa aliyekusingizia akikuona mtaani atatangaza polisi ni wala rushwa tu mtuhumiwa wangu wamemuachia sababu ya rushes tu.

Huyo mwenye kesi ndo alishirikiana na hao polisi kunibambikia hiyo kesi.. Pia niliwasikia wakizozana wao kwa wao baada ya kuona sina hatia yoyote ndio wakang'ang'ania niwape hiyo hela kama usumbufu wa kuishughulikia kesi yangu au waipeleke mbele nikashindane nao mahakamani..

Nikaona potelea mbali Funika Kombe Mwanaharamu apite.. Nikawapa tu hiyo hela yaishe!
 
Mimi nishaur tu kitu kimoja ukiona uko sahihi usitoe rushwa lkn nyie wenyw mnawakomvis maasikar kuwapa rush
 
Back
Top Bottom