Polisi: Marufuku Waandishi na Wananchi kukusanyika Polisi watuhumiwa wakiitwa kuhojiwa

Haya maagizo kwa mujibu wa sheria ipi?

au kauli ya polisi nayo ni sheria?

Waandishi wairuhusiwe kuchukua habari?
Sa si ndiyo hapo!!!! Yaani ni Rais akisema kitu basi wao wanakurupuka kurupaka tu bila kutafakari sasa habari wataandika wao? NONSENSE POLISI.
 
Katika hili nakubali kabisa acha iwe hivyo , maana kilichofanyika pale central ni kuonesha ulimwengu kuwa hakuna vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania.

Hivyo, acha sasa ieleweke kuwa serikali ina mkono wa kukumata na ina macho ang'avu sana kukuona popote pale ulipo japo, pana nyakati serikali hujifanya kama vile haioni ila inazo taarifa za kila mmoja wetu na tukifanyacho.

Kama , kweli sisi watanzania tungekuwa wazalendo tusinge furahia kile kitendo cha kwanya na washabiki wa mpira kwenda kufanya vitimbwi pale kituo kikuu cha Polisi (central)

Hata, waliokuwa zamu Mwenyezi Mungu, aliwashangaa sana kwa kuwasamehe wale walioenda kufanya kwaya na vihoja pale kituoni.

Maana huyo Mungu, wanaemuimbia ni wa utaratibu na siyo wa fujo kama walizozifanya kwa kelele pale kituoni.

Mimi ni mwamini ila kwa hilo, lilofanywa walipaswa hata kupata kifungo cha chini kama cha miezi 6 hivi ndiyo wajielewe kuwa serikali siyo Kanisa au uwanja wa mpira.


Pia, naona Taifa watu wamengawanyika sana kwa sababu hawaelewi tena misingi ya utaifa wao.

Ila, Rais Magufuli ataweka misisngi ambayo daima tutaelewa na kukumbuka kuwa Rais Magufuli alifanya mambo makubwa sana kwa nchi yetu.

Ieleweke kuwa , sitetei mtuhumiwa hapa, ninachosema ni kuwa ... "wapambe wa watuhumiwa walifanya makosa makubwa pale central"... ila watuhumiwa itajulikana hatima yao.

Ila kwa vitendo vile acha Polisi na vyombo vingine vya ulinzi vifanye kazi zao.

Hamna namna tena, maana haiwezekani serikali ikafanywa kama mwanasesere na kila mtu.

Ikiwa hivyo, hatutafika wala hatutakuwa salama tena.

Ahsanteni.
Ni serikali za kikoloni tu ndizo zilizokuwa na mtizamo huu. Bahati mbaya uhuru wetu na elimu zetu hazijatusaidia kabisa kutatua changamoto halisi za maisha. Kudhani kwamba eti watu wameonyesha dharau kwa vyombo vyetu vya usalama ni mtizamo tu ambao hauna msingi wowote, believe me.
 
Hiyo ni hatua nzuri maana kama walitegemea watapata kazi ya kulinda viwanda wameula wa chuya, hadi sasa miezi 16 hakuna hata kiwanda kimoja kimejengwa na hii serikali ya awamu ya tano. Milioni 50 kila kijiji nazo hakuna kwa hiyo polisi hata kazi ya ku escort hela wanaikosa. Bora wafanye siasa tu

Kama unawafahamu Nyumbu hutauliza kuna viwanda vingapi vimejengwa toka JPM aingie madarakani
 
Acha kuwaonea walimu, niambie ni kundi gani la watumishi wasiokuwa waoga hapa Tz! Tumeshuhudia nyongeza ya mishahara ikisimamishwa kiholela, madaraja, ajira, uhamisho n.k. Je ni kundi gani ukiacha hao walimu limesimama kidete na kupinga uonevu huo? Mi si mwl, lakini naomba tuwe katika hili.

Mkuu, Bila shaka u mwalimu
 
waandishi wa habari wanaruhusiwa hadi sehemu yenye vita wanavalishwa nembo ya mwandishi hao wa nyunga utadhani sijui ni vitu gani mnavitafutia umaarufu tu ambao hauna hata maana..
 
Hiyo ni hatua nzuri maana kama walitegemea watapata kazi ya kulinda viwanda wameula wa chuya, hadi sasa miezi 16 hakuna hata kiwanda kimoja kimejengwa na hii serikali ya awamu ya tano. Milioni 50 kila kijiji nazo hakuna kwa hiyo polisi hata kazi ya ku escort hela wanaikosa. Bora wafanye siasa tu
 
Jamani bila waandishi wa habari tutapataje habari kwa muda muafaka, Naweza kukubaliana na kauli ya Generali Ulimwengu kuwa kwa sasa tumeisharudi nyuma kama miaka 50 nini maana yake sasa, bado Watanzania hawajapata uhuru hadi sasa.
 
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania ACP Advera Bulimba ametoa agizo la kuzuia ukusanyikaji wa watu katika vituo vya polisi wakati wa kuhojiwa watu/watuhumiwa maarufu.

Agizo hilo ni kwa waandishi wa habari, vikundi vya watu na wananchi wa kawaida.

Kufuatia agizo hili la polisi,lililotolewa 14/02/2017 na Makao Makuu ya Polisi, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaokiuka agizo hilo.

Agizo hili linaanza kutekelezwa mara moja katika vituo vyote vya Jeshi la Polisi Tanzania bara na visiwani.

Taarifa hii inakuja siku kadhaa baada ya Rais Magufuli kukemea hali ya wanakwaya wa kanisa la Ufufuo na Uzima kukusanyika na kuimba mapambio wakati wakimsubiri Askofu wa kanisa lao akihojiwa kwa tuhuma za midaharati, huku wafuasi waliokuwa wamevalia sare za klabu moja maarufu ya mpira, nao wakikusanyika na kusubiri mustakabali wa kiongozi wa klabu yao.
Polisi hawa hamani!
Sasa hawaoni wanaua ile tabia yao ya kuita waandishi kuwaomba wasambaze taarifa kuhusu wahalifu na kuwaomba wananchi washirikiane damdam?
 
Haki ya kupashana habari?, na siku hizi hata nikiwa na ka simu nachukua all necessary info . By the way muda c mrefu tutazoea kuwa kila kinachofanywa na serikali ku jidistance na wananchi!

kama una sababu za msingi unaruhusiwa kwenda polisi, nilivyoelewa ni kwamba kukusanyika bila sababu ya msingi nji marufuku. waandishi hawakusanyiki, waandishi wanafuata habari na kuondoka hivyo wanasababu ya msingi ya kwenda kituoni.
 
Back
Top Bottom