Polisi,Mahakama na rushwa.

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Kila unapofanyika utafiti na asasi mbalimbali basi utakuta Jeshi la Polisi
linaongoza kwa kuomba na kupokea rushwa. Kibaya zaidi wanapenda
kuwabambikizia watu fake kesi. Hivi sasa kuna watu wako magerezani
kwa kubambikiwa kesi na hawa jamaa. Yaani ukijifanya unajua sheria na
ukakataa kuwapa kitu kidogo'basi ujue imekula kwako,lazima wakukomoe.

Nafasi ya pili kwa kuomba na kupokea rushwa ni Mahakama zetu za kata
(mahakama za mwanzo na wilaya) yaani huko ni hatari bin kutisha! wana
omba rushwa kama karanga.Yaani ukiwa ndani ya viwanja hivyo unavuta
hewa na harufu ya rushwa tu. Hawajali mlalamikaji wala mtuhumiwa,wao
wanaangalia pesa tu. Ukiwa mkono wa birika basi ujue sheria inapindishwa
fasta na inakula kwako.
Je, tukiwa kama wananchi tufanyenini ili kukomesha manyanyaso haya?
Hasa hasa polisi, yaani wanakera sana kwa kutuonea jamani!.- Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom