Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,028
Hili ni moja kati ya matukio 1000 yanayofanywa na askari wa jeshi la polisi.
Iko hivi, kuna jamaa nilipata kusoma naye kitambo na sasa ni polisi kitengo cha FFU.
Juzi polisi huyu kaniambia kuwa, huwa anakodisha silaha yake kwa majambazi wakati wa lindo usiku (hasa akipangwa bank) na asubuhi hurejeshewa silaha yake na kitita cha laki mbili mpaka tatu kutoka kwa majambazi hayo.
Hakuishia hapo, polisi huyo alizidi kunidokeza kuwa wanapoishiwa na pesa za matumizi huwa wanachukua silaha wakati wa lindo mida ya jioni na kuvaa makoti makubwa kama raia na kuvamia maduka makubwa ya biashara za jumla wakati wa kufunga na kutishia kwa silaha hizo za jamuhuri na kupora fedha kutoka ktk duka husika.
MY TAKE:
Polisi wetu wakiwa huko mafunzoni hufundishwa utii wa uwoga na wanapewa treatment mbaya sana kiasi cha kuwafanya kuwa na roho mbaya na ya kikatili badala ya kuwa waaminifu na watii wa sheria.
Mafunzo ya ukatili wanayofundishwa askari wetu yanawafanya walinzi hawa wa usalama wa raia na mali zao kukengeuka na kuwa majambazi kwa kujaribu kujikwamua kwenye umaskini kwa kutumia ukatili uleule waliofunzwa huko CCP.
Swala la mafunzo ya askari na malipo yao litazamwe upya.
Askari anayelipwa laki mbili unusu kwa kazi ya kulinda bank yenye billions of money lazima awe mwizi.
Kwa kifupi polisi ndo wezi hapa tanzania.