Polisi Kitengo cha Dawa za Kulevya Inawashikilia maofisa 2 wa TRA kwa kujihusisha na magendo

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,819
Polisi Kitengo cha kuzuia Dawa za Kulevya Inawashikilia maofisa 2 wa TRA kwa kujihusisha kupisha na kemikali ya precursor kimagendo

=======

Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawashikilia watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuhusika kupitisha viuatilifu vya kutengeneza dawa za kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kamishna wa operesheni wa mamlaka hiyo, Mihayo Msikela alisema watumishi hao walishirikiana na wanaosafirisha dawa hizo kuzipitisha hapa nchini.

Alisema watumishi wengine wawili wanafuatiliwa nyendo zao kabla ya kutiwa nguvuni kwa ajili ya mahojiano.

Chanzo: Mwananchi
 
Polisi Kitengo cha kuzuia Dawa za Kulevya Inawashikilia maofisa 2 wa TRA kwa kujihusisha kupisha na kemikali ya precursor kimagendo




Mkuu,
Tafadhali kama unaweza onesha (Sort)wahusika, maana pichani wapo wengi.
 
Hivi mbowe anaenda lini kuhojiwa?
Muda huu ndio anahojiwa, jasho linamtoka kweli anashindwa hata kujieleza, kumbe Mbowe akiwa anahojiwa na huyu mtu ni mwoga sana! Mkewe anamohoji kwanini asubuhi hakumaliza kikombe cha maziwa alichompatia!
 
WATUMISHI WA TRA WAINGIA KWENYE SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA
Watumishi Wawili Wa TRA wanashikiliwa na vyombo vya dola wakituhumiwa kujihusisha na upitishaji Wa kemikali ambazo hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya Heroin.
Kukamatwa kwa watumishi hao wa umma kumetangazwa leo na Kamishina Wa Operesheni ya Mamlaka Watumishi Wawili Wa TRA wanashikiliwa na vyombo vya dola wakituhumiwa kujihusisha na upitishaji Wa kemikali ambazo hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya Heroin. Kukamatwa kwa watumishi hao wa umma kumetangazwa leo na Kamishina Wa Operasheni ya Mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya Mihayo Msekela.
Tembelea www.habarileo.co.tz kwa habari zaidi
 
Back
Top Bottom