Polisi Kagera waua watu 5 kwa kuwapiga risasi!

Polisi Kagera waua watu 5 kwa kuwapiga risasi!

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Posts
1,043
Reaction score
759
Taarifa ambazo zimefika kwenye vyumba vyetu vya habari hapa Bukoba ni kuwa polisi mkoani hapa wamewaua watu 5 wanaodhaniwa kuwa majambazi kwa kuwapiga risasi katika wilaya ay Biharamulo.

Mtapata update muda mfupi.

byabato
 
Mmmhh wanajenga mazingira ya kuwauwa CDM kesho, washindwe na walegeee
 
Kama kweli ni majambazi, well done POLICE FORCE maana eneo la Biharamulo na Ngara majambazi wanasumbua sana usalama wa raia. Itakuwa njia ya kuwatia hofu wengine wanaopanga kutumia eneo hilo kufanya uhalifu
 
wanasumbua mno, nahiyo sio kazi yakufanya japo maisha nimagumu.
 
Inteligensia yao iwe imefanya kazi kwa majambazi wa kweli tu.
 
kama kweli ni majambazi wacha tu wauwawe,maana wao huwa hawana huruma na wanaokwenda kuwaibia,iweje wewe uwe na huruma juu yao?
 
Biharamulo, Ngara na Karagwe (Pori la Kimisi) huwa usalama wake ni tete. Lakini wawe wanawakamati ili wajue mtandao wao.
 
Confirmed: Ni kweli watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa na Polisi wilayani Biharamulo.

Kwa takriban wiki mbili sasa umekuwepo mfurulizo wa utekaji magari hasa yale madogo ya abiria maarufu kama michomoko. Alhamis hii waliteka tena jamaa walokuwa wanakwenda mnadani Lusahunga.

Baada ya msako, Polisi wakiwa na raia walianza msako katika pori la Lusahunga na wamefanikiwa kupambana na majambazi hao. Hatimaye waliweza kuwaua WATANO kati ya sita. Mmoja wao amefanikiwa kukimbia.

Walouawa yasadikika walikuwa raia wa Burundi na huyo mmoja aliyekimbia alikuwa ni Mtanzania. Miili ya majambazi hao iko mortuary ya hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo.

SOURCE: mimi mwenyewe niko likizo fupi Biharamulo ndo kwetu nyumbani!
 
Huwezi kuuwa mtu kwa kudhani! Hili ni jambo la hatari sana. Wote wanaoshabikia jambo hili siwaungi mkono hata kidogo.
Moyo wangu uko pamoja na wale waliopoteza ndugu zao ambao hawakuwa na hatia lakini walidhaniwa kuwa ni wahalifu na wakauawa. Mateso wanayopitia ni Mungu peke yake ambaye atawanusuru na kuwalipia kisasi.
 
sio vizuri kuuwa mtu hata kama ni jambazi,jambazi anatakiwa akamatwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.Tunalea mapolisi wenye vitambi hawana mbinu yoyote ile ya kukamata wahaini zaidi ya kujua kufyatua risasi na kama inabidi kuwapiga basi wawapige risasi miguuni sio kuuwa tutakuwa tunauwa tu ovyoovyo.Kwakuwa eneo hilo la msitu mkubwa imekuwa tishio kwa miaka mingi sana nashauri eneo hilo pajengwe kambi ya jeshi la ulinzi ndo dawa pekee ya kuwasaidia watanzania wenzetu wanaotumia njia hiyo tuhamishe vikosi vilivyopo mijini kabisa vinginevyo hawa warundi watatumaliza-
 
Confirmed: Ni kweli watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa na Polisi wilayani Biharamulo.
Walouawa yasadikika walikuwa raia wa Burundi na huyo mmoja aliyekimbia alikuwa ni Mtanzania. Miili ya majambazi hao iko mortuary ya hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo.
SOURCE: mimi mwenyewe niko likizo fupi Biharamulo ndo kwetu nyumbani!
Inaonekana Polisi waliwafahamu toka mwanzo kutokana na habari hii. Huyu Mtanzania alikuwa 'Agent Provocateur'?? Kwa nini walinuia kuwaua? Hapa ndipo umuhimu wa sheria ya 'Inquest' inapoonekana.
 
Huwezi kuuwa mtu kwa kudhani! Hili ni jambo la hatari sana. Wote wanaoshabikia jambo hili siwaungi mkono hata kidogo. Moyo wangu uko pamoja na wale waliopoteza ndugu zao ambao hawakuwa na hatia lakini walidhaniwa kuwa ni wahalifu na wakauawa. Mateso wanayopitia ni Mungu peke yake ambaye atawanusuru na kuwalipia kisasi.
Kama wewe ni Askari uko doria porini, mara unakutana na watu wenye siraha wanaoingia kwenye majibizano ya risasi na wewe, je utasubiri mahakama ije eneo la tukio iwatie hatiani ndipo na wewe ujibu mashambulizi? Man, be serious! Officers' survival first!Pia, mimi ni shahidi, maeneo mengi ya mkoa wa kagera ni hatari sana kwa ujambazi! Wengi wa Majambazi wanatoka kwenye inchi za Burundi, Rwanda na pengine Uganda zinazouzunguka mkoa huo!
 
Back
Top Bottom