Polisi jamii iendane na elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi jamii iendane na elimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rimbocho, Jan 14, 2010.

 1. r

  rimbocho Member

  #1
  Jan 14, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Polisi jamii ni ile hali ya maisha ya usalama wa raia kwa ushirikiano baina ya polisi na raia (ambao ndio wanalindwa na polisi). Elimu ya kujiunga na jeshi hilo isiwe kuanzia kidato cha nne, naomba angalau form six, kwani hawa jamaa uelewa wao wa mambo huwa ni mdogo sana ndio maana hata uchunguzi wa kesi nyingi huwa na mashaka na watuhumiwa wanaachiwa hata kama kweli walihusika na tukio hilo. Hebu fikiria majuzi nilikuwa na drive kuelekea ofisini, nikakutana na askari wa usalama barabarani akaniambia eti sina BIMA ya gari, ukweli ni kwamba BIMA ilikuwepo ila ilikuwa haisomeki vizuri, akaniambia nimpe cover note nikawa sina iko nyumbani, basi huyu jamaa kanikomalia nikamwambia twende kituoni tukaenda basi ikawa nongwa kufika tu ananiambia niingie rupango, tukabishana mkubwa wake mmoja alikuwa na kama nyota 3 hivi akamuuliza huyu jamaa mbona husemi kosa lake? akaanza kung'ata meno, mimimnikaongea mwenyewe namna alivyonikamata mpaka kufika pale yule bosi akamwambia mwache aende zake maana hilotatizo si la kumleta mtu hapa kwani kilichofutika ni tarehe na namba ya gari lakini no. ya insurance ipo, chamsingi huyu bwana atembee na cover note ilikuthibitisha hiyo BIMA ni halali. Basi mie nikatoka ingawa nilishachelewa kazini. Je huyu bwana najua umuhimu wa bima kuliko mwenye gari? hivi kweli nitembee na gari bila bima nikipata matatizo itakuwaje? Angeweza kufikiri kidogo angenipa maelezo kama ya bosi wake na ningeendelea na safari yangu.
  Jamani mi nasisitiza elimu iende sambamba na polisi jamii, Hivi kweli hiyo rupango kazi yake ndio hiyo?
   
 2. R

  Rikab Mikail Member

  #2
  Jan 14, 2010
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Karibu bongo
   
 3. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana alitaka kitu kidigo hapo ila wee ulimbania.

  Angekupeleka kwa Vehicle inspector walikague gari kila kitu kuanzia fire sticker, Triangles, fire extinguisher n.k
  Kila kosa 20000.
   
Loading...