Polisi Dar wadai kuua majambazi

Polisi Dar wadai kuua majambazi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limedai kuwa limeua watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, na kukamata silaha moja aina ya bastola

Jeshi hilo limesema kwamba bastola hiyo imefutwa namba na ilikuwa na magazine iliyokuwa na risasi moja.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Jeshi la Polisi Kanda hiyo, watu hao waliuawa juzi saa 7:30 mchana.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika maeneo ya Magomeni katika ufuatiliaji wa wahalifu, ghafla askari Polisi waliokuwa katika doria walishambuliwa kwa risasi na majambazi ambao walihisi kuwa wanafuatiliwa, ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi majambazi watatu kwa risasi.

“Wakati wanakimbizwa katika ya Hospitali Mhimbili kwa ajili ya matibabu walifariki dunia. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa majambazi hao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo ilieleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali wa wahalifu wote wanaofanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jijini, na kuwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Chanzo: Nipashe
 
What if ni mistakes..Nani atawaprove wrong?
 
Juzi Saa saba mchana magomeni? Taarifa inatoka leo? Mhhhhhh haya. Hizi taarifa viporo hadi lini.
 
Hivi kuna mwenye akili timamu anaendelea kuamini upuuzi huu wa polisi?
 
Back
Top Bottom