Polisi Arusha wawekwa mfukoni na Lowassa na Monaban

Polisi Arusha wawekwa mfukoni na Lowassa na Monaban

Joined
Aug 20, 2014
Posts
8
Reaction score
8
Wadau,

Wengi wanaweza wakadhani ni siasa, lakini ndiyo ukweli, kwamba Jeshi letu la polisi chini ya RPC, RCO wamekuwa wakitumia nafasi zao vibaya kinyume na wanavyotakiwa kuwa. Jeshi hili la polis limegeuka kuwa wajumbe waaminifu kwa CCM hasa Lowassa na Saiteru (Monaban) kwa kutekeleza maagizo wanayopewa kuvuruga mikutano ya chadema Arusha.

Ni hivi karibuni polisi wadogo wamekuwa wakilalamika juu ya matumizi mabaya ya madaraka ya RCO, RPC na OCD kuzuia mikutano halali ya CHADEMA kwa maslahi ya Lowassa.

Fedha za Lowassa na Monaban zimefikia hatua ya kukandamiza sauti za wanyonge ambao wangependa kusikia kutoka wale wanaowasemea, wale wanaowasaidia kilio chao kifike mbali. Habari za ndani kutoka kwa nzi wetu zinaeleza kuwa baada ya CHADEMA kutangaza kufanya mikutano maeneo mbali mbali hapa Arusha, Arumeru na Monduli, polisi wamekuwa wakimwagiwa fedha na Monaban ili kuzuia mikutano ya CHADEMA.

Mbaya zaidi polisi wamekuwa wakitoa sababu kuwa hawataruhusu CHADEMA kufanya mikutano kwakuwa viwanja waliyoomba vimeombwa kufanya mikutano ya kidini. CHADEMA walifanya uchunguzi wakagundua hakuna mikutano yoyote ya dini inayofanyika kwenye viwanja vilivyoombwa, na kwamba fedha za Monaban ndizo zinatumika kuzuia mikutano halali ya CHADEMA.

Ikumbukwe kuwa huyu Monaban ni yule fisadi aliyechukua eneo la reli la zaidi ya ekari 13 kwa kisingizio cha mkataba wa mwaka moja, ambapo baada ya Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kupata taarifa alilalamikia uhuni ule na kusababisha Monaban kuzuiwa kuendelea na ujenzi wa ukuta mkubwa unaozunguka eneo hilo.

Lakini kwakuwa jeshi la polisi limewekwa mfukoni mwa Monaban, baada ya muda ujenzi wa ukuta uliendelea chini ya ulinzi wa jeshi na usalama wa taifa, kwakuwa Monaban naye anafanya kazi ya Lowassa.

Hata hivyo, pamoja na zuio hilo la mikutano ya CHADEMA, bado CHADEMA wataendelea kufanya mikutano yao kama kawaida, na bila vurugu yoyote katika kata za jiji la Arusha na maeneo mengine.

Jeshi la polisi wameamua kujidhalilisha kwa kufanya kazi kutoka kwenye mfuko wa mafisadi wa ccm
 
Na jambo lingine la kuwa makini sana kwa wana wa Arusha, siku za karibuni wametokea watu wanalazimisha Ole Millya awe mbunge wa kumrithi Lema. Sikatai mabadiliko ya mmbunge kwani hilo ni sehemu ya demokrasia, lakini kila mtu anajua connection iliyopo kati ya Millya na huyo Lowassa. Watu wa Arusha muwe makini sana hasa na viongozi wanaotoka ccm, wote tumeona tabia za Shibuda. Ni vizuri cdm mjitungie kanuni angalau mtu kabla ya kugombea udiwani, ubunge, urais ndani ya cdm isipungue miaka mitano toka kujiunga na aonyeshe jitihada zake za kukuza chama mpaka wakati wa kuomba kuchaguliwa kushika madaraka.
 
Eti mkataba wa mwaka moja, halafu unajenga ukuta wa zaidi ya bilioni 2 usanii mtupu
 
Na jambo lingine la kuwa makini sana kwa wana wa Arusha, siku za karibuni wametokea watu wanalazimisha Ole Millya awe mbunge wa kumrithi Lema. Sikatai mabadiliko ya mmbunge kwani hilo ni sehemu ya demokrasia, lakini kila mtu anajua connection iliyopo kati ya Millya na huyo Lowassa. Watu wa Arusha muwe makini sana hasa na viongozi wanaotoka ccm, wote tumeona tabia za Shibuda. Ni vizuri cdm mjitungie kanuni angalau mtu kabla ya kugombea udiwani, ubunge, urais ndani ya cdm isipungue miaka mitano toka kujiunga na aonyeshe jitihada zake za kukuza chama mpaka wakati wa kuomba kuchaguliwa kushika madaraka.

James Ole Millya anakwenda kukomboa Simanjiro
 
Watu hawajui tu...lakini upepo wa mageuzi ikifika itwavurumisha tu................
 
Back
Top Bottom