Polisi Arusha kashfa hii haiwaachi salama

Polisi Arusha kashfa hii haiwaachi salama

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Wakati Rais John Magufuli akiwa ziarani Mkoani Arusha ,Polisi nane wakiwemo migambo wa kitui cha Polisi Mbauda wametenda unyama wa kutisha kwa kumpiga risasi na kumvunja mguu mkulima,aitwaye Hwanga Ndaskoi(30) mkazi wa kata ya Oljoro wilayani Arumeru.

Imeelezwa kwamba askari hao ambao waliletwa na baba mkwe wake na majeruhi aitwaye Yohane Palai baada ya kuhitilafiana kifamilia ,askari hao wakiwa na gari la polisi walirubuniwa ili wampige risasi wakati hapa kuwa na ulazima wa kutumia nguvu kubwa kama hiyo.

Inadaiwa kuwa baada ya kumkuta shambani kwake akivuna mahindi akiwa na mama yake mzazi pamoja na Mke wake ,baba mkwe aliwaamuru askari hao kumpiga risasi baada ya baba mkwe kuwahadaa kuwa mtuhumiwa huyo ana sime na angeweza kuwakata.ndipo askari mmoja mwenye sare za jeshi hilo alipomfyatulia risasi na kumvunja mkuu wake wa kulia kama anavyoonekana kwenye Picha.

Baada ya tukio hilo askari hao walimpakia kwenye gari lao na kumpeleka katika hospitali ya Mount Meru ambapo waliwahadhaa Mapokezi kuwa ameanguka na Toyo.

Kamànda wa Polisi mkoani Arusha ,Charles Mkumbo alipoulizwa amesema hana taarifa.

Tukio hilo limetokana na ugomvi wa kifamilia .familia ya majeruhi inaomba msaada wa kisheria juu ya unyama wa tukio hilo


b589791da5153bf912ba74d442063ead.jpg
 
Huitaji FBI kujua aliempiga risasi Lissu, once a killer always a killer
 
Daaaa ukipiga simu kuna majambazi masaa 2 hawaonekani.
Lkn raia wema ndio wanauawa.Ipo siku
 
Kwa hiyo baada madaktari kuambiwa ameanguka na Toyo na waobwaka mtibu kitoyo toyo au? Qakati madao hayo yanaibuliwa yeye alikua kimya tu muda wote?
 
Back
Top Bottom