Polisi apata kichapo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi apata kichapo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Michael Amon, Apr 1, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  POLISI mmoja kati ya watatu waliokuwa kwenye doria, amepigwa na kujeruhiwa na mtuhumiwa walipokwedna nyumbani kwake (mtuhumiwa) kumkamata.

  Tukio hilo lilitokea saa 1:00 usiku wa kuamkia jana Mtaa wa Mbagala Mlandizi, wilayani Kibaha, mtuhumiwa aliyempiga askari huyo anadaiwa kulawiti alifuatwa kupelekwa kituoni cha polisi.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema askari aliyejeruhiwa ni E. 4420 Sajini Dady, huku mtuhumiwa akitajwa kuwa ni mkazi wa Mbagala, Mlandizi.


  Mangu alisema wakati wa ukamataji huo, mtuhumiwa alikataa kutii sheria na kusababisha vurugu zilizopelekea kumjeruhi kichwani polisi kwa kitu chenye ncha kali.


  Alisema askari aliyejeruhiwa alipelekwa Hospitali Teule ya Tumbi, alipatiwa matibabu na kuruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.

  Hata hivyo, polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituoni na kwamba, zaidi ya kulawiti amefunguliwa kesi nyingine ya kumjeruhi askari wakati akitekeleza majukumu yake.

  E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jamaa inaonekana ni shababi, ngoja nae akapigwe kitu jela.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  walimwonyesha kitambulisho? Halafu mambo ya kukamatana usiku usiku,labda alijua ni majambazi!

  Ila acha akatumikie mvua yake,jitu zima linalawiti!
   
 4. chumvichumvi

  chumvichumvi JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: May 6, 2010
  Messages: 1,050
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  pole zake
   
 5. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Jamaa sio mzima. Mimi nahisi atakuwa na mapepo tu. Mbona mademu wapo wa kumwaga. Imekuwaje hadi alawiti?
   
 6. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Halafu anakamatwa na bado anakuwa mbishi.
   
Loading...