Nikiwa natokea zangu asubuhi kutoka maili moja nikiwa kwenye IST yangu na kamvua kananyesha kwenda viwanja, kufika maeneo ya Kwa Yusufu Mbezi nikakutana na barrier ya trafic wakikagua magari yalikuwa yakipita.
Ilinipa mawazo kwa kuwa taa ya mkono wa kushoto mwa gari yangu imevunjika, baada ya trafic kukagua gari akagundua hilo kosa.
Basi nikashuka nikaongee asiniandikie faini,
nikatoa elfu 5 nikamwambia mkuu shika hii ya kubrashia viatu, acha acharuke unanipa rushwa!
Nikamwambia hapana hata mh. mtukufu Rais alisha sema elfu 5 hizi si mbaya mchukue za kuburashia viatu, kwa hasira ameamua kuniandikia faini.