Polisi afia baa baada ya kulewa sana

Polisi afia baa baada ya kulewa sana

Huyo marehemu hana akili. Badala ya kufia kwa kimada yeye anafia bar. Ujinga gani huu
 
ASKARI Polisi mkoani Ruvuma, amekutwa amekufa kwenye baa ya Friend's Pub iliyoko katikati ya mji wa Songea huku ikielezwa kuwa alikuwa amekunywa pombe kupindukia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Marwa, alimtaja askari polisi aliyekutwa amekufa kuwa ni Konstebo Donald Motoulaya (29), ambaye ni askari katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa. Alisema ilidaiwa kuwa siku ya tukio hilo, juzi majira ya saa 4:15 asubuhi, Jaibu Nyoni (26) ambaye ni mhudumu wa baa hiyo, alitoa taarifa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi kuwa askari Donald amelala kwenye kochi na amejaribu kumwamsha lakini imeshindikana.

Kamanda Marwa alifafanua zaidi kuwa baadaye askari waliongozana na daktari kwenda eneo la tukio ambako walimkuta askari huyo akiwa amelala kwenye kochi ambalo liko ndani ya baa hiyo. Marwa alisema katika uchunguzi ilibainika kuwa askari huyo alifika kwenye baa hiyo Machi 12, majira ya saa 4:30 usiku akitokea katika baa nyingine iitwayo Mtini Pub ambako alikuwa akinywa pombe.

Alisema mtoa taarifa alieleza kwamba wakati askari huyo anaingia Friend's Pub, aliteleza na kuanguka kwenye ngazi na baadaye alimwinua na kumtoa nje kisha askari huyo alirejea na kukaa kwenye kochi wakati huo mhudumu akiendelea kuhudumia wateja.

“Ilipofika majira ya saa 4:15 asubuhi jana (juzi), wahudumu wakiwa wanafanya kazi za usafi, ndipo walipomwona PC Donald akiwa kwenye kochi wakidhani amelala lakini walipojaribu kumwamsha hakuamka ndipo walipotoa taarifa polisi. Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Ruvuma,

Dk. Hassan Lumbe, alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, alisema mwili wa askari huyo ulifikishwa hospitalini hapo na watu ambao hawakujitambulisha na ulipokewa na mganga wa zamu.

Dk. Lumbe alifafanua kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kitabibu ilionekana kuwa askari huyo ameshafariki dunia muda mrefu uliopita na kwamba uchunguzi huo ulionyesha hakuwa na mchubuko wowote isipokuwa kulikuwa na mchubuko mdogo kwenye shavu la kushoto.

Alisema baadaye walipohojiwa watu waliomleta walidai kuwa alikuwa amekunywa kiasi kikubwa cha pombe, hivyo uchunguzi wa kitaalam wa sababu ya kifo chake ni kwamba alikuwa amekunywa pombe kwa kupindukia.


IPP
Mwanadam atafufuliwa juu ya kile alichofia
Ameangamia, Kweli ameangamia
 
Huyo inaonekana hakufa kwa pombe walipoingia bar aliteleza (kanuba style) akajipiga chini wakamuinua ndio akaenda kwenye kochi inawezekana kuna mshipa wa fahamu ulikuwa unavujisha damu slow na ndio mauti ikamkuta hapo
 
Mbinguni hakuna bia, acha tunywe bia na ukifa rafiki zako wanaendelea kunywa bia. Acha nimwage bia chini kukumbuka
R.I.P Kamanda
 
TUKISEMA POLISI NI MBWA MNAKATAA ULAFI GANI HUO ?SI AJABU POMBE ZENYEWE NI OFFER ZA WATUHUMIWA WA UONGO
Hivi kweli unaamini ktk huyu Mungu au unamini miungu!! Usitumie lugha chafu kwa binaadamu mwenzio.

5/5
 
hakuwa na mchubuko wowote lakini alikuwa na mchubuko mdogo kwenye shavu////
 
Dk. Lumbe Alisema baadaye walipohojiwa watu waliomleta walidai kuwa alikuwa amekunywa kiasi kikubwa cha pombe, hivyo uchunguzi wa kitaalam wa sababu ya kifo chake ni kwamba alikuwa amekunywa pombe kwa kupindukia.


IPP

Dah hapo doctor Lumbe tayari kamaliza uchunguzi wa KITAALAM!

Kweli bongo nyosso sana!!!

***Abhasubhi twemanye***
 
Yan hz pombe watu wanakunywa ila n hatar juzi jamaa mdogo tu kafa kimasiala yan na so kwamba alikuwa anakunywa sana ila sku hyo sijui n pepo gan alikunywa akapitiliza hkohko yaan ndan ya mda mfupi alishakuwa marehemu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuwahamasishe polisi wanywe sana.
Mwakani kuna uchaguzi
 
Back
Top Bottom