Polisi 16 wakamatwa Dar

Polisi 16 wakamatwa Dar

TIQO

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2011
Posts
13,786
Reaction score
2,102
na Abdallah Khamis

HATIMAYE Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limewatia mbaroni askari 16 wanaohusishwa na tuhuma za uhalifu.

Kutangazwa kwa taarifa hiyo kunakuja siku chache baada ya Tanzania Daima kuandika habari juu ya polisi hao kwa kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuunda mtandao wa kihalifu.

Taarifa ya kukamatwa kwa askari hao zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Kova alisema askari hao wanatuhumiwa kuunda mtandao wa kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru wa serikali.

Licha ya kuweka wazi idadi hiyo kamanda Kova aligoma kuyataja majina ya wahusika bila kuweka wazi kwa nini ameamua kufanya hivyo.

Kova pia alitumia muda huo kuilaumu Tanzania Daima, kwa kuandika habari za uhalifu huo juzi ikiwa ni baada ya uchunguzi wa zaidi ya wiki moja tangu kukamatwa kwa askari hao.

Alisema kabla ya gazeti hili kuandika habari hizo kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, jeshi hilo lilikuwa limeshawakamata askari wake wanane kutokana na tukio hilo.

Mei 10, Tanzania Daima ilimuuliza kamanda Kova juu ya habari hizo lakini alikataa kuzitolea ufafanuzi kwa madai angelizungumza na waandishi wengi.

Bila kujali jitihada za Tanzania Daima kuipata habari hiyo kamanda Kova alijinasibu kuwa angelizitoa kwa utaratibu aliojiwekea yeye na wala si kwa kuulizwa na gazeti moja moja.

"Si kwa kuwa gazeti moja liliandika na ndiyo tumesukumwa kuwakamata wahalifu hawa; tulianza taratibu hizi mapema na tukawa tunasubiri muda muafaka wa kuweka mambo yote hadharani," alisema Kova.

Hata hivyo Kova jana alishindwa kuweka wazi yalikopelekwa magari yaliyokamatwa kwenye uhalifu husika.

Wakati akishindwa kutaja kama kuna magari yaliyokamatwa, baadhi ya askri waliozungumza na gazeti hili wameshangazwa na hatua hiyo na kumtaka DCP Kova awe mkweli juu ya sakata hilo.

Askari hao wamehoji hatua ya Kova kuwakamata wenzao walioonekana katika picha za video za mnato na kushindwa kuyakamata magari yaliyokubali kushiriki katika uhalifu huo.

"Mnapaswa kujiuliza kama askari wameshafika 16 halafu hakuna gari hata moja lililokamatwa, hao watakuwa wanapelekwa mahakamani kwa ushahidi wa namna gani na kwa nini hayo magari hayakuweza kuchukuliwa katika hizo picha au ni siasa za mzee wetu zimewafanya mkashindwa kuhoji hilo?" alisema mmoja wa askari.

Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliandika juu ya kuwepo kwa mtandao unaowashirikisha askari wa vyeo mbalimbali kutoka jijini Dar es Salaam na baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) wakiwa wamejiundia mtandao wa kukusanya pesa kutoka kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa ushuru.

Mtandao huo unadaiwa kufanya kazi kwa takriban miezi sita kabla ya kujulikana na kuchukuliwa kwa hatua dhidi yao.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Tanzania Daima, mbinu inayodaiwa kutumiwa ni kwa askari hao kuwasaidia wafanyabiashara kuingiza bidhaa kupitia bandari bubu ya Mbweni, kisha kuzipakia kwenye magari makubwa kwa ajili ya kutawanya bidhaa hizo katika masoko ya jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya bidhaa zinazodaiwa kuingizwa kwa wingi ni runinga, redio, pasi za umeme na kompyuta mpakato.

Tanzania Daima
 
Kuna baadhi ya askari polisi ni wahalifu sugu wanaofanya uhalifu wakitumia mavazi ya serikali. Shame on them!
 
hawa polisi maisha magumu sana mungu awasaidie
 
Angalau wamejisikia aibu, niliwahi kuandika humu kuna mfanya biashara ana duka kubwa la jumla lipo karibu na kona ya barabara ya Tandale hospitali na Kwamtogole uwa anashusha mafuta ya kula ya dili, siku ya kushusha fuso inakuja huku inasindikizwa na landcruiser za blue za polisi na wakifika dukani tu utashangaa polisi wanamiminika kutoka kila kona wengine kwa bodaboda, taxi au difenda kama kunguru wameona mzoga wanachukua chao mapema bila kificho, yaani ni aibu sana na huyo mfanyabiashara sijui anapataje faida labda kama anawapa bukubuku.
 
Kuna askari wanne wa kituo cha Mabatini nao ni washiriki. Kuna Fuso mbili kila siku zinaingiza mafuta ya kupikia kupitia huko huko mbweni hawa jamaa huwa wanachukua chao kila kukicha. hiyo Fuso zinapitia ubungo, mabibo kigogo kwenda kariakoo.

Muda ni kati ya saa mbili na saa tano usiku.
 
ni haki polisi na walimu kuiba au kufanya uhalifu wowote kutkana na hali duni walionayo!!!sioni kosa lao ila pia wanatutesa sana raia mtaani kila kitu kwao ni kosa ,unakuta askari anakuambia indicator ya gari lako imepinda lipa fain.
 
hawa polisi maisha magumu sana mungu awasaidie

Hurka tu, kwani wao wanatumia maduka na masoko tofauti na watu wengine kama waalimu, wauza kahawa, wapanga nyanya, mabar maid nk? Ukizingatia wao wana unafuu wa lunch allowance katikati ya mwezi, wameshaona rushwa ni sehemu ya haki zao za msingi.
 
Kuna baadhi ya askari polisi ni wahalifu sugu wanaofanya uhalifu wakitumia mavazi ya serikali. Shame on them!

basi kuna siku moja nilikuwa nimechelewa sana kutoka ukumbumbi wa NSSF Waterfront kwenye harusi ya mdogo wangu, na nilikuwa narudi home Bunju mida ya saa tisa usiku nilikutana na Landcruser moja ya polisi ikisindikiza Loli tena lenye Tera wakiwa wanaingia vinjia vya mtaani usiku hule nikahisi tu kuna jambo baya nchi yangu inafanyiwa, sijui kama tutafika
 
ni haki polisi na walimu kuiba au kufanya uhalifu wowote kutkana na hali duni walionayo!!!sioni kosa lao ila pia wanatutesa sana raia mtaani kila kitu kwao ni kosa ,unakuta askari anakuambia indicator ya gari lako imepinda lipa fain.

Ndugu yangu, usiharalishe uhalifu.
 
Kuna askari wanne wa kituo cha Mabatini nao ni washiriki. Kuna Fuso mbili kila siku zinaingiza mafuta ya kupikia kupitia huko huko mbweni hawa jamaa huwa wanachukua chao kila kukicha. hiyo Fuso zinapitia ubungo, mabibo kigogo kwenda kariakoo.

Muda ni kati ya saa mbili na saa tano usiku.
Watakua wanaaagiza kutoka nchi gani hayo mafuta mkuu Kichakoro
 
Last edited by a moderator:
Polisi wanaotumia landcruiser za blue mkonga ni zaidi ya majambazi kova na mwema lifanyien kazi hili.
 
Kuna baadhi ya wabunge kazi yao ni kuwachafua wenzao na mate wakilitetea jeshi la polisi bila kufuatia mwenendo wao wa kazi
 
Angalau wamejisikia aibu, niliwahi kuandika humu kuna mfanya biashara ana duka kubwa la jumla lipo karibu na kona ya barabara ya Tandale hospitali na Kwamtogole uwa anashusha mafuta ya kula ya dili, siku ya kushusha fuso inakuja huku inasindikizwa na landcruiser za blue za polisi na wakifika dukani tu utashangaa polisi wanamiminika kutoka kila kona wengine kwa bodaboda, taxi au difenda kama kunguru wameona mzoga wanachukua chao mapema bila kificho, yaani ni aibu sana na huyo mfanyabiashara sijui anapataje faida labda kama anawapa bukubuku.
kumbuka kwamba huyo mfanyabiashara halip KODI
 
huoni kosa hapo???hawa polisi wala rushwa sio wakuwatetea ipo siku watakuja kwako kukupandikiza kesi ya madawa alafu wakata hela wasikupeleke ngome.kibya zaidi hawa watu wanamtandao mkubwa sana na raia wa kawaida kwaiyo wao wakiona ishu yoyote wanaitolea macho then wanataka chajuu.kuna sekta lakini sio hii sekta kwa kweli...
 
TANZANIA DAIMA MMEFANYA KAZI NZURI SANA Kama sio hili gazeti tusingejua haya yote.
 
Hizo ishu nzuri sana,angalau ni njia bora ya kupambana na rapid inflation inayotuumiza kila kukicha,hizo tax free items ndizo zinazotusaidia tunapata bidhaa kwa bei poa,hata kodi ikilipwa hatuonagi faida yake.
 
Back
Top Bottom