Polisi 16 wakamatwa Dar

Polisi 16 wakamatwa Dar

ni haki polisi na walimu kuiba au kufanya uhalifu wowote kutkana na hali duni walionayo!!!sioni kosa lao ila pia wanatutesa sana raia mtaani kila kitu kwao ni kosa ,unakuta askari anakuambia indicator ya gari lako imepinda lipa fain.

hahaha, uyo afande kapinda aisee. iyo fain unaandikiwa au ndo unampooza kiaina?
 
hakuna namna ya kuhalalisha walivhokifanya hawa ndugu zetu!
watanzania wote tuna maisha magumh lakini njia wanazotumia hawa jamaa kujikimu si sahihi..
IGP bado ana kazi kubwa sana ya kufanya, hii mitandao iko mingi sana..
 
napata shida kujua hao askari hizo tabia wamejifunza wakiwa ccp au inakuaje? isije ikawa wakufunzi wao wanawafundisha hivo afu c tunalaumu.
 
Mtoto wa miaka 9 mara.
Mwangosi
watu watatu Arusha
Wampiga dent IFM
Wamtoa ngeu mke wa Dr.Slaa
Waua mahabusu
Wanakamatwa na mafuvu
Wanakamatwa na Ndovu

etc
....bado ni hawa hawa police na tunaendelea kwa Amani ya Mungu. Tz is ......
 
huoni kosa hapo???hawa polisi wala rushwa sio wakuwatetea ipo siku watakuja kwako kukupandikiza kesi ya madawa alafu wakata hela wasikupeleke ngome.kibya zaidi hawa watu wanamtandao mkubwa sana na raia wa kawaida kwaiyo wao wakiona ishu yoyote wanaitolea macho then wanataka chajuu.kuna sekta lakini sio hii sekta kwa kweli...

Siku hizi wamebuni mbinu mbadala kaka wanatembea na mafuvu ya watu kubambikiza kesi za mauaji sijui wanayafukua makaburi gani.
 
ahaha ahaaa ahaa sasa tukiwaendekeza kisingizio mshahara hautoshi...tutabambikiziwa kesi kama hiizi nakubaka mpaka tukome
 
Angalau wamejisikia aibu, niliwahi kuandika humu kuna mfanya biashara ana duka kubwa la jumla lipo karibu na kona ya barabara ya Tandale hospitali na Kwamtogole uwa anashusha mafuta ya kula ya dili, siku ya kushusha fuso inakuja huku inasindikizwa na landcruiser za blue za polisi na wakifika dukani tu utashangaa polisi wanamiminika kutoka kila kona wengine kwa bodaboda, taxi au difenda kama kunguru wameona mzoga wanachukua chao mapema bila kificho, yaani ni aibu sana na huyo mfanyabiashara sijui anapataje faida labda kama anawapa bukubuku.

......ni nchi ya watu wadogo, nchi ya kitu kidogo........
 
kumbuka kwamba huyo mfanyabiashara halip KODI

Kama ni hivyo basi hiyo kodi ni kubwa serikali wanapaswa waangalie vizuri viwango vyao maana umati wa maaskari unaofuata ganji kuona ni mkubwa, sijui wanaambiana muda gani mtashangaa tu malandcruiser mkonga za blue yanalandalanda maeneo mara fuso lipo chini ya ulinzi mkubwa linaingia kisha bodaboda zinamwagika.
 
Mbona hao polisi ni kwaida yao, kuna askari hapo kituo cha mabatini anaitwa SAMSONI yaani huyo alishakubuhu, kafikia hatua ya kujitengenezea mishara bubu kwa baadhi ya walala hoi.
 
Utakuta na bwana mkubwa anajua na ana mgao wake!ni aibu sana Mbweni kuna chuo kikuu cha TISS linatakiwa liwe eneo safi na halina uchafu wa rushwa na kashfa kama hizo!hivi hawaogopi hata TISS?wanapitisha kule kule walipo?au sababu TISS hawana meno na wamekuwa wafanya biashara nao siku hizi?
 
Mbona hao polisi ni kwaida yao, kuna askari hapo kituo cha mabatini anaitwa SAMSONI yaani huyo alishakubuhu, kafikia hatua ya kujitengenezea mishara bubu kwa baadhi ya walala hoi.

Siku hizi wamegundua kitengo kipya cha kukusanya posho, wanawaandama wamama wanaojiuza Tandale uwanja wa fisi na Mwananyamala hospitali wanakusanya kila mlango.
 
wamechoka na maisha magumu sasa wafanyije hali ya bongoland kimaisha inaendelea kuwa gumu sana. lakini heko kamanda Kovu
 
.......Kama ambavyo majina ya wahalifu wengine ambao bado ni washukiwa yanatangazwa hadharani basi na polisi hawa nao......Tunaomba majina yao.......
 
Mkuu Mende0, ugonjwa huu wa kulindana unaofanywa na viongozi serikalini ni ukurutu usiokuwa na dawa! Kwa nini afande Kova akatae kutoa taarifa ya tukio kama hilo na kubeza taarifa inapotolewa na gazeti la Tanzania Daima kwa manufaa ya Taifa kama hausiki?

Morogoro alikuwepo mfanyabiasha jambazi aliyekuwa anaitwa Godfrey Ndosi. Huyu bwana alikuwa analindwa sana na kiongozi mmoja mstaafu wa juu kabisa ndani ya jeshi la polisi. Aliuawa mwaka 2005 alipoingia kwenye anga za wakubwa zaidi.

Waziri Nchimbi aunde kamati itakayochunguza swala hili na kuwataka askari waliokamatwa wawataje waliowatuma na kuwaongoza kwa muda wote huo wa miezi sita. Ni vizuri kamati hiyo ikaundwa na wanajeshi (JWTZ) bila ya kuwashirikisha akina afande Kova manake wao ndiyo watuhumiwa.
 
Kova bwana.....sasa hao askari hawana majina wala namba?
intelijesia yake imeona ukitaja majina wengine hawatapeleka pesa walizopata maana hao wadogo wakipata pesa katika hizo dili wanapeleka kwa wakubwa ili wa walinde ilikitokea la kutokea na ndio maana anakigugumizi kutaja majina ana chochote mpenda noti
 
Tz daima subirieni ya yule mwandishi aliyepiga trafki picha kipindi kile.
 
Sheria ichukue mkondo wake kama kwa vibaka.
 
Back
Top Bottom