IGP 'Poti' Sirro Kauli hii ya Askari wako Kituo cha Police Kawe kwa Raia aliyeibiwa Simu ni sahihi na ndiyo Maagizo yako au?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,791
Raia aliyeibiwa Simu aitwae Yusta ( Mhaya Kagera )

Afande nimekuja Kuripoti nimeibiwa Simu yangu Kituoni Kawe.

Afande wa Zamu Polisi Kawe Asubuhi Juzi

Ya aina gani na ulinunua Shilingi ngapi?

Ni ya Techno ya Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini.

Afande wa Zamu Polisi Kawe Asubuhi Juzi

Iwe mwanzo na mwisho Kutusumbua kwani Sisi huwa hatuhangaiki na Simu za Tecno tena za Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini bali huwa tunatoa Msaada kwa Raia walioibiwa Simu za maana za kuanzia Shilingi Laki Nne na Kuendelea.

Kwahiyo tusipokimbilia Kwenu kupata Msaada tukimbilie wapi?

Afande wa Zamu Polisi Kawe Juzi

Kwa Mungu wa Madhabahu yako.

Sawa Asante

Afande wa Zamu Polisi Kawe Juzi

Kwaheri na Kawasalimie Wote Kwenu.

Mkuu wa Kituo cha Police Kawe Afande Brazameni David ( Davie ) tafadhali kuwa makini sana na Askari wako hapo Kawe kwani hawakutii tu Doa kwa hili nililolileta bali na hata kwa mengineyo mabaya zaidi.

Sijajua kama Jana IGP Sirro ( Poti wangu wa Kizanaki ) alipokuja ghafla hapo Kituoni Kwako ( Kawe Police Station ) mida ya Saa 10 hivi kuelekea Saa 11 aliwakemea baadhi ya Mambo ila Kituo chako ( Afande David ) kina Matatizo mengi na ukiyachekea si tu yatakuharibia Wewe na Kituo chako hicho cha Kawe bali yatachafua hadi Jeshi lako zima la Polisi.

Halafu waonye sana Askari wako wa hapo Kawe ulipo kupenda sana Kudoea Bia ( Pombe ) za Dezo hapo Kawe katika Baa iliyo Jirani na Baa Kubwa na Maarufu ya Hipro ambapo Wakigongea ( Wakiomba ) Bia usipowapa huamua Kujimiminia Wenyewe hasa huyo Mmoja mwenye Miguu mibovu 'aliyerogwa' na Mpemba kwa Kosa la Tamaa zake, Kubambika na Kudhulumu Raia. Najua Historia yake unayo / ulishapewa.

Pigania huo Ukumbi wenu utumike Ok?
 
Wakosahihi ukiisoma loss report yao chini kabisa Kuna lines hua sizielewagi nachekaga Sana ,zinapingana na muhuri wao kuthibitisha gharama walizopokea ambazo hukana kuamini Kama imepotea au haijapotea
 
Kituo cha polisi Kawe ni shida ; aliwahi kuwepo OCS mnyakyusa mmoja sijui kama yupo alikuwa anawalinda sana majambazi wa Mbezi beach; unfortunately Jina lake nimelisahau!! Hawa OCS wa hapo kituo cha Kawe msiwaruhusu kukaa muda mrefu!!!
 
Raia aliyeibiwa Simu aitwae Yusta ( Mhaya Kagera )

Afande nimekuja Kuripoti nimeibiwa Simu yangu Kituoni Kawe.

Afande wa Zamu Polisi Kawe Asubuhi Juzi

Ya aina gani na ulinunua Shilingi ngapi?

Raia aliyeibiwa Simu aitwae Yusta ( Mhaya Kagera )

Ni ya Techno ya Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini.

Afande wa Zamu Polisi Kawe Asubuhi Juzi

Iwe mwanzo na mwisho Kutusumbua kwani Sisi huwa hatuhangaiki na Simu za Tecno tena za Shilingi Laki Moja na Elfu Hamsini bali huwa tunatoa Msaada kwa Raia walioibiwa Simu za maana za kuanzia Shilingi Laki Nne na Kuendelea.

Raia aliyeibiwa Simu aitwae Yusta ( Mhaya Kagera )

Kwahiyo tusipokimbilia Kwenu kupata Msaada tukimbilie wapi?

Afande wa Zamu Polisi Kawe Juzi

Kwa Mungu wa Madhabahu yako.

Raia aliyeibiwa Simu aitwae Yusta ( Mhaya Kagera )

Sawa Asante

Afande wa Zamu Polisi Kawe Juzi

Kwaheri na Kawasalimie Wote Kwenu.

Mkuu wa Kituo cha Police Kawe Afande Brazameni David ( Davie ) tafadhali kuwa makini sana na Askari wako hapo Kawe kwani hawakutii tu Doa kwa hili nililolileta bali na hata kwa mengineyo mabaya zaidi.

Sijajua kama Jana IGP Sirro ( Poti wangu wa Kizanaki ) alipokuja ghafla hapo Kituoni Kwako ( Kawe Police Station ) mida ya Saa 10 hivi kuelekea Saa 11 aliwakemea baadhi ya Mambo ila Kituo chako ( Afande David ) kina Matatizo mengi na ukiyachekea si tu yatakuharibia Wewe na Kituo chako hicho cha Kawe bali yatachafua hadi Jeshi lako zima la Polisi.

Halafu waonye sana Askari wako wa hapo Kawe ulipo kupenda sana Kudoea Bia ( Pombe ) za Dezo hapo Kawe katika Baa iliyo Jirani na Baa Kubwa na Maarufu ya Hipro ambapo Wakigongea ( Wakiomba ) Bia usipowapa huamua Kujimiminia Wenyewe hasa huyo Mmoja mwenye Miguu mibovu 'aliyerogwa' na Mpemba kwa Kosa la Tamaa zake, Kubambika na Kudhulumu Raia. Najua Historia yake unayo / ulishapewa.

Pigania huo Ukumbi wenu utumike Ok?
Polisi wazandiki sana
 
Kituo cha polisi Kawe ni shida ; aliwahi kuwepo OCS mnyakyusa mmoja sijui kama yupo alikuwa anawalinda sana majambazi wa Mbezi beach; unfortunately Jina lake nimelisahau!! Hawa OCS wa hapo kituo cha Kawe msiwaruhusu kukaa muda mrefu!!!
Polisi Kawe ni Majanga na Shida kubwa sana. Binafsi, ni victim wa tabia yao ya kutetea wahalifu!! Mwenye haki, unageuziwa kibao :mad:🤬🤬🤬
 
Back
Top Bottom