Polepole, twende polepole utuambie na hili

Polepole, twende polepole utuambie na hili

Kalamu Yangu

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
1,110
Reaction score
1,077
49835DB2-2D47-4ED0-AADB-CC3B3671AA57.png






Kaka Humphrey kwanza nikupongeze kwa kazi njema unayotufanyia watanzania.Kwa kuwaanika 'wahuni' na uhuni wao , sie wasakaonge na wanywa kahawa huwa tunapata cha kujadili kila machweo.


Sauti yako ya upole na msisitizo kila unapotupa madini huwa inatumika kama rejea kwenye mazungumzo yetu.


Unaposema "marehemu" aliniita akaniambia hili na lile , tunaamini kuwa wewe mtu wa 'jikoni' kule ndani kabisa , uliwahi kuwa mkuu wa wilaya wewe( Rais wa wilaya wewe) , sitaki kusema uenezi hadi ubalozi.


Mjamaa mwenzetu, wewe Ikulu ulikuwa huoni ITV kwenye habari au kwenye vipindi vya Msigwa 'Tuliahidi tumetekeleza' wewe ulipokea wito kama vile mie niitwavyo na wateja wangu ninapouza maduveti huku nanenane; Unajua mengi bwana.


Sipo hapa kuhakiki bei ya jiko la gesi kule Havana maana 'ningegugo 'tu nikajua.


Kaka tudokezee tu kuhusu huyu bwana "Ben Sanane" yuko wapi?


Sitaki kumwamini Kabendera nahisi anaharibu tu Legasi ya Mwendazake wala sihisi kuwa Kubenea alikuwa sahihi.


Nakuamini wewe , umekuwa unatoa vinavyothibitika kama havithibitiki vinaungika 'dots'.


Kuanzia Ungwasi, Mkuu, Mlele, Kisale hadi Tarakea bado kitendawili cha Ben hakijapata jibu la kueleweka.


Tuambie hata kwa mafumbo ili kuanzia rafiki zake Malisa GJ, Mama Love pale Geita hadi mie ambaye baada ya kumuuzia sera zangu alikuwa tayari kujiunga na 'Foreva Livingi' ilisiku aache kazi awe milionea kwa biashara ya mtandao tujue nini kilimpata.


Kaka Humphrey kama hutaki tujue basi watumie hata meseji wazazi wake pale Rombo wakazike nguo zake tujue kafa.


Fanya hata bintiye ajue kuwa ni yatima, wala si lazima useme alipozikwa kama kafa, tuambie kwa mafumbo kama tuimbe tenzi kumsindikiza ama tumsubiri atarudi kama "mwana mpotevu".


Usiseme ni wahuni ama wengine waliofanya hivyo ,maana hatuna cha kuwafanya, kama walim 'pyu pyuuuTuambie tu tuache dhahania na matumaini kama binti aliyeahidiwa ndoa mwezi wa tisa ambao kila mwaka upo.


Sema tu yu hai , tufurahi ama kafa tuzirai kaka.


Alamsiki.
 
Back
Top Bottom